Mwana wa Mohammed Ali akiwa Kinshasa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,320
33,125
Lilikuwa pambano la kipekee, ambalo bara la Afrika halijabahatika kushuhudia tena kwa miaka 35.
Tarehe 30 mwezi Oktoba, 1974, mabondia maarufu Mohammed Ali na George Foreman walitandikana jijini Kinshasa, katika nchi ambayo wakati huko ilikuwa ikijulikana kama Zaire - sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
20091031190629tatiana_mohammed_ali.jpg

Khaliah Ali akiwa na Katibu mkuu wa wizara ya michezo, Barthelemy Okito, wakati alipozuru Kinshasa.

Mwaka huu Kongo imepata ugeni unaokumbushia mpambano huo, Khaliah Ali, binti na mtoto wa mwisho wa Mohammed Ali, alizuru Kinshasa na kujiunga na wanandondi kusherekea kumbukumbu la pigano hilo la kihistoria.
Khaliah Ali, alishangiliwa na wanandondi wengi katika uwanja wa Tata Rafael kwa jina maarufu “Rumble in the Jungle” kwenye sherehe ya kumbukumbu ya pigano baba yake Mohammed Ali alimtandika George Foreman kwenye uwanja huo miaka 35 iliyopita.
Bi Khaliah Ali, ambaye alikuwa bado mchanga wakati baba yake akitoana jasho na George Foreman, alizuru vyumba na sehemu mbali mbali za uwanja huo. Na alipofika katika chumba kilichotengwa kwa ajili ya baba yake, alibubujikwa na machozi.
“Ni hali yenye harara kuzuru mahali ambapo baba yangu aliwahi kupigina hapa Congo. Singeliweza kuzuia machozi yangu nilipo ona picha za baba na mababu zangu hapa. Nakukutana na Waziri wa michezo na wanandondi hapa ilitugusa sana. Ni muhimu kwangu kuwapatia yale mliyompatia baba yangu wakati alipopigana hapa,” alisema Khaliah.
Hata hivyo, ziara yake iliambatana na madai kuwa wakati Mohammed Ali alipokuwa Kinshasa aliwaahidi wanandondi kuwa atawasaidia kuchangia kuendeleza ndondi za DRC wakati huo ikijulikana kama Zaire.
Wanandondi hao wanadai mpaka sasa Mohammed Ali hajatekeleza ahadi hiyo. Lakini katibu mkuu wa wizara ya michezo, Barthelemy Okito, ndiye alichukua fursa ya ziara ya Khaliah Ali kuomba amkumbushe baba yake kuhusu ahadi hiyo.
“Mohammed Ali, baba yake Khaliah alikuwa akisema kuwa ana mizizi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na barani Afrika. Nilikutana na wanandondi hapa ambao walisema kuwa Mohammed Ali, aliwaahidi kusaidia maendeleo ya ndondi hapa nchini. Na tutatumia ziara ya mtoto wake kumkumbusha kuhusu ahadi hiyo.”
20091031190538kinshasa_stadium.jpg

Hapa ndipo "Rumble in the Jungle" ilipofanyika, uwanja wa Tata Rafael mjini Kinshasa.

Si wanandondi peke yao waliokuwa wakitegema kutumia ziara hiyo kuomba usaidizi. Meneja mkuu wa uwanja wa Tata Rafael, anategemea kuwa ziara ya mtoto wa Mohammed Ali inaweza kuwasaidia kupata msaada ya kukarabati uwanja wao.
Uwanja huo umekuwa katika hali duni sababu umeachwa baada ya uwanja mwingine mkubwa wa Kinshasa, “Stade des Martyrs”, kujengwa kutokana na uhusiano kati ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na China.
Kabla ya kuwasili Kinshasa na kuzuru uwanja wa “Rumble in the Jungle” ambapo baba yake alimdunda George Foreman katika raundi ya nane kwa knockout, Khaliah, alizuru Lubumbashi ambako anafadhili kituo kimoja cha kusaidia kinadada na wanawake wasiojiweza.



http://www.bbc.co.uk/swahili/highlights/story/2009/11/091102_khaliah_ali_mohammed.shtml
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom