Mwamuzi Ramadhani Kayoko kuwa 'Pilato' mechi ya Yanga vs Simba

Joseverest

JF-Expert Member
Sep 25, 2013
52,030
69,483
SIKU chache baada ya Mwanaspoti kufichua juu ya waamuzi waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya kuchezesha mchezo wa Kariakoo Derby utakaofanyika April 30, 2022 katika dimba la Benjamin Mkapa saa 11 jioni, huku kikao kizito kikifanyika, ukweli umebainika kwamba mwamuzi Ramadhan Kayoko amepewa kazi hiyo.

Hadi Kamati ya Waamuzi inakaa kikao majina matano ndiyo yalikuwa yakipigiwa kura lakini mwisho wa yote, Kayoko ameonekana kupata asilimia kubwa na kupewa jukumu hilo la kumaliza ubishi kwa wababe hao wa soka nchini.

Awali, katika majina hayo matano, lilikuwa jina la Sasii na Abdalla Mwinyimkuu yaliyopewa nafasi kubwa, huku wengine wakiwa ni Hance Mabena, Emmanuel Mwandembwa na Abel William.

Hata hivyo, kikao kilichomalizika katikati ya usiku mwingi kikihusisha Kamati ya Waamuzi, kililiongeza jina la Kayoko na mwishoni mwamuzi huyo kijana akafanikiwa kuwabwaga wenzake.

Taarifa ambazo Mwanaspoti imezinyaka, ni kwamba Kayoko atasimama katikati huku akisaidiwa na Frank Komba (Dar es Salaam), Mohamed Mkono (Tanga), wakati Elly Sasii (Dar es Salaam) atakuwa mwamuzi wa mezani.

Rekodi zinaonyesha kuwa, Kayoko mara ya mwisho kuchezesha dabi ilikuwa Septemba 25, 2021 kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii, akisaidiwa na Frank Komba, Soudy Lila na Sasii aliyekuwa mezani, Yanga ilishinda bao 1-0 likifungwa na Fiston Mayele dakika ya 12.

Mwamuzi huyo ndiye aliyechezesha pia ile dabi ya nusu fainali Kombe la ASFC 2019-2020 iliyopigwa Julai 12, 2020 mchezo ambao waamuzi sita walihusika ni; Komba, Mpanga, Nadeem Aloyce, Abdalah Mwinyimkuu na Abubakari Mturo, na Yanga ikapoteza kwa mabao 4-1.

Pia alichezesha katika mchezo wa kilele cha Siku ya Mwananchi Agosti 29, mwaka jana wakati Yanga ikipoteza kwa mabao 2-1 mbele ya Zanaco kwenye Uwanja wa Mkapa.

Kayoko ambaye alikuwa mwamuzi bora wa msimu wa mwaka 2019/20 hajahusika sana kuchezesha kwenye ratiba ya Ligi Kuu msimu huu hasa michezo inayowahusu wababe hao wa soka la Bongo.

Katika michezo 19 iliyocheza Simba, Kayoko hajachezesha mchezo hata mmoja wakati Yanga iliyocheza michezo 20, Kayoko amechezesha mchezo mmoja wakati ikiichapa bao 1-0 Geita Gold Machi 6, mwaka huu.

Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza waamuzi wasaidizi alikuwapo Fedrinand Chacha, Makame Mdogo wakati mwamuzi wa akiba akiwa Wilson Masea.

Katika dabi iliyopita Desemba 11 timu hizo zilipotoka suluhu, mwamuzi wa kati alikuwa, Sasii akisaidiwa na Mpanga, Hamdani Saidi pamoja na Ahmada Simba.

Hili ni pambano la 108 kwa timu hizo katika ligi ya Bara tangu mwaka 1965, lakini ni la 12 kupigwa ndani ya Aprili tangu mwaka 1982.

CHANZO: Mwanaspoti

SOMA PIA: Refa wa Simba, Yanga ajadiliwa usiku mnene Dar
View attachment 2203563
 
๐‘ฒ๐’‚๐’‘๐’†๐’˜๐’‚ ๐’Ž๐’†๐’„๐’‰๐’Š ๐’š๐’‚ ๐’Œ๐’†๐’”๐’‰๐’ ๐’•๐’†๐’๐’‚
 
Huyu komba kila.mechi ya Simba na yanga anakuwa mwamuzi wa pembeni na pia aliruhusu mpira uliotoka nje urudishwe ndani yanga wakafungua siku ya mechi ya yanga na Azam Cha ajabu hajapewa adhabu yoyote
 
SIKU chache baada ya Mwanaspoti kufichua juu ya waamuzi waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya kuchezesha mchezo wa Kariakoo Derby utakaofanyika April 30, 2022 katika dimba la Benjamin Mkapa saa 11 jioni, huku kikao kizito kikifanyika, ukweli umebainika kwamba mwamuzi Ramadhan Kayoko amepewa kazi hiyo.

Hadi Kamati ya Waamuzi inakaa kikao majina matano ndiyo yalikuwa yakipigiwa kura lakini mwisho wa yote, Kayoko ameonekana kupata asilimia kubwa na kupewa jukumu hilo la kumaliza ubishi kwa wababe hao wa soka nchini.

Awali, katika majina hayo matano, lilikuwa jina la Sasii na Abdalla Mwinyimkuu yaliyopewa nafasi kubwa, huku wengine wakiwa ni Hance Mabena, Emmanuel Mwandembwa na Abel William.

Hata hivyo, kikao kilichomalizika katikati ya usiku mwingi kikihusisha Kamati ya Waamuzi, kililiongeza jina la Kayoko na mwishoni mwamuzi huyo kijana akafanikiwa kuwabwaga wenzake.

Taarifa ambazo Mwanaspoti imezinyaka, ni kwamba Kayoko atasimama katikati huku akisaidiwa na Frank Komba (Dar es Salaam), Mohamed Mkono (Tanga), wakati Elly Sasii (Dar es Salaam) atakuwa mwamuzi wa mezani.

Rekodi zinaonyesha kuwa, Kayoko mara ya mwisho kuchezesha dabi ilikuwa Septemba 25, 2021 kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii, akisaidiwa na Frank Komba, Soudy Lila na Sasii aliyekuwa mezani, Yanga ilishinda bao 1-0 likifungwa na Fiston Mayele dakika ya 12.

Mwamuzi huyo ndiye aliyechezesha pia ile dabi ya nusu fainali Kombe la ASFC 2019-2020 iliyopigwa Julai 12, 2020 mchezo ambao waamuzi sita walihusika ni; Komba, Mpanga, Nadeem Aloyce, Abdalah Mwinyimkuu na Abubakari Mturo, na Yanga ikapoteza kwa mabao 4-1.

Pia alichezesha katika mchezo wa kilele cha Siku ya Mwananchi Agosti 29, mwaka jana wakati Yanga ikipoteza kwa mabao 2-1 mbele ya Zanaco kwenye Uwanja wa Mkapa.

Kayoko ambaye alikuwa mwamuzi bora wa msimu wa mwaka 2019/20 hajahusika sana kuchezesha kwenye ratiba ya Ligi Kuu msimu huu hasa michezo inayowahusu wababe hao wa soka la Bongo.

Katika michezo 19 iliyocheza Simba, Kayoko hajachezesha mchezo hata mmoja wakati Yanga iliyocheza michezo 20, Kayoko amechezesha mchezo mmoja wakati ikiichapa bao 1-0 Geita Gold Machi 6, mwaka huu.

Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza waamuzi wasaidizi alikuwapo Fedrinand Chacha, Makame Mdogo wakati mwamuzi wa akiba akiwa Wilson Masea.

Katika dabi iliyopita Desemba 11 timu hizo zilipotoka suluhu, mwamuzi wa kati alikuwa, Sasii akisaidiwa na Mpanga, Hamdani Saidi pamoja na Ahmada Simba.

Hili ni pambano la 108 kwa timu hizo katika ligi ya Bara tangu mwaka 1965, lakini ni la 12 kupigwa ndani ya Aprili tangu mwaka 1982.

CHANZO: Mwanaspoti

SOMA PIA: Refa wa Simba, Yanga ajadiliwa usiku mnene Dar
View attachment 2203563
Mbona mechi zingine hakuna presha za waamuzi

Sent from my LM-Q730 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom