MWALIMU: Uliza kuhusu kituo ulichopangiwa

mimi nimepangiwa Handeni DC - Tanga .... sasa nitajuaje kitoa shule yangu hapo mkuu !!!!

hata mm ni huko huko, ila kunashida ya maji balaa umeme ni baadhi ya maeneo, hali ya hewa ni nzuri ila vumbi lake ni jekundu sana watu wa kule ni wakarimu ila ukileta dharau utaisoma wanamambo ya kichawi sana
 
naomba mtu yeyote anaeijua hili eneo viziri anisaidie mana hapa naona manyota nyota tu.....
 
jamani nimepangiwa tanga handeni sijui chochote kuhusu huku naombeni mniambie kukoje ili nijipange vizuri
 
umeme maji samaki hali ya hewa poa sana karibu musoma vijijini uwezi fananisha na sehemu kame kama bahi
Ndugu yangu kapangiwa huko. Toka Musoma Mjini mpaka Makao Makuu ya Musoma DC ni mwendo wa saa ngapi kwa bus? Nauli ni shilingi ngapi? Hali ya mvua ipoje? Rutuba ya ardhi ipoje?
 
Jamani nimepangiwa mkoa wa kigoma wilaya ya buhigwe shule inaitwa bwafumba. Naomba anaepafahamu vizuri anisaidie yafuatayo
1.nauli kutoka kigoma mjini
mpaka wilaya ya buhigwe ni kiasi gani? 2. Nauli kutoka makao makuu ya buhigwe mpaka ilipo shule ya bwafumba ni kiasi gani? 3. Hapo bwafumba kuna nyumba za kupanga? 4. Hapo bwafumba upatikanaji wa huduma kama maji, hospital na mitandao ya simu ukoje?
NAOMBA KUJUZWA TAFADHALI
 
kwa ufupi kaliua ni wilaya mpya ambayo ndo inayoendelea kwa ss chakua na maji vinapatkana kwa bei ndogo sana .
haina mistu mikubwa bali kuna vichaka vya hapa na pale.
karibu ujionee mwalim wetu

Asante kwa kunfahamisha mkuu
 
Mwenzako alikuwa analia hapa ofcn sababu ya kupelekwa musoma. Jambo baya anataka kutoa RUSHWA ili abadilishwe kituo.
Kwako benjamini, musoma niliwahi kuishi pale hata kufika vjjn, ukienda jaribu kuwa mbunifu na mchakalikaji baada ya masaa ya kazi.
kwa anaefahamu wilaya ya Musoma tafadhali naomba dondoo. Musoma DC ni ile ya mini au vijijini? Mdogo wangu kapangwa Musoma DC.
 
Tandahimba ni wilaya inayopatikana Mkoa wa Mtwara, unapotaka kwenda waweza panda mabasi ya Dar-Tandahimba mfano wa basi ni TANDAHIMBA XPRESS (Bovubovu hivi) au upande basi linaloenda Masasi kutokea Dar then shuka Mtama (Kwa Bwana Mkubwa) hapo utapata mabasi ya huko, changamoto ya huko ni barabara mbovu tu ndo maana hata mabasi yanayokwenda huko ni yale ya tripu moja Dar Tripu gereji.

Hivi wananchi wa huko kwanini wanaendelea kuikumbatia ccm hadi leo 52 years!!
Napata uchungu sana sana nikisoma comments humu jinsi nchi ilivyo choka
 
Back
Top Bottom