Mwalimu Nyerere na ukabila

Hahahha....mi nilivyosikia ni kwamba hakutaka watuwawe na tv ili wasijue yanayoendelea nje ya sehemu walipo...sasa yeye kwasababu anayo anakuja kuwadanganya ana maono haya na yale kuhusu ulimwengu unapoelekea.Siku ya pili watu wakisikia zile habari kwenye redio au sijui kwenye magazeti basi wanazidi kumwamini maana anajua mambo!!!Ntakitafuta!!!

hiyo inawezekana
but alikataza watu tv
yeye aliiona ni luxury watu kutazama tv
watu watakuwa wavivu,wasifanye kazi...

halafu enzi hizo radio za mkulima zilikuwa
zinatengenezwa hapa nchini,
kiwanda cha tv ingekuwa ishu,
so akaona bora marufuku
 
Mkuu hebu punguza porojo za mtaani kidogo......Hivi sasa kuna TV za kumwaga, hicho kiwanda cha TV Tanzania kiko wapi?.......Mbona hakukataza magari wakati nchi haikuw na kiwanda cha magari? Hivi TV zilianza lini kuonekana Tanzania?
 
Nilisikia kwamba na TV pia hakupenda watu binafsi wamiliki!Hicho kitabu kinaitwaje?!Ningefurahi kweli kukipata!!!

Nyerere alifanya mambo mengi mazuri especially kwenye issue ya usawa ila lazima tukubali kwamba alikuwa na vi elements vya udikteta. Aliminya sana uhuru wa kutoa/kupata habari ingawa yeye mwenyewe alikuwa na Runinga ikulu!!
Hauwezi ku justify altaka marais watoke kwenye makabila madogomadogo tu eti kwa sababu marais karibu wote wametoka kwenye makabila madogo!!
 
Nimekusoma na nimekuelewa!Swali...kama alichokua hataki ni walionacho kuongezewa niambie nini haswa kinachoendelea Tanzania karne hii?!Na je leo hii ukiambiwa kwamba haya makabila makubwa yakichukua nchi yatawekana sana madarakani ila maendeleo yatakuwepo (maisha mazuri kwa kila mTanzania kama wanavyosema wanamagamba) utaona bora tutawaliwe na mchanganyiko usio na muelekeo au kundi moja linalojua nini linafanya?!?!
Kipindi kile ni tofauti na kipindi hiki.., sasa kuna mchanganyiko wa makabila sio kama zamani, pia na makabila mengine yameshaamka sasa hivi sio kama kipindi kile wakati wengine walikuwa wanatambaa wengine walikuwa wanakimbia.., Therefore bila kuweka level playing field then maybe tungekuwa na makabila ya wamachinga; mabar maid, walinzi, machangu doa n.k. meaning kwamba opportunity wengine wasingezipata. Kwa kujibu swali maybe alifanya aliyoyafanya sio kwa chuki ya makabila fulani bali ni kwa kuona kuwa wengine wangemezwa.

Hizo zilikuwa enzi zile sasa hivi mambo yamebadilika na tumeshajua kuwa uongozi au uwezo hautokani na mababu zako ni kina nani bali uwezo wako... therefore hata kama akija alien mwenye uwezo wa kuongoza mimi atapata kura yangu.
 
Nyerere hajawahi kusema makabila fulani Tanzania hayastahili uongozi wa aina fulani. Umeona vyema kwani angefanya hivyo ingekuwa ni kwenda kinyume kabisa na yote aliyoyasimamia na kuyaamini. Hii ni mojawapo ya myths ambazo zimetengenezwa.

nilipochaguliwa kuwa kiranja mkuu tarehe 13/09/99,kesho yake mwalimu alifariki,kwa heshima hiyo nilimtunuku hili ktk kitabu cha rambirambi

FAIRWELL PARTY OF THE GIANT:
At this corner I stand,​
To watch the people,​
In deep grief and sorrow,​
Crying and becoming unconscious,​
Their father has slept,​
For the eternal rest:​
He is just like smiling​
As if he wants to say;​
“Viva Africa and peace​
Be to its people”​
O kinsmen don’t cry! Be happy​
And celebrate,​
Kaunda, Mandela, Mkapa and all comrades,​
This is a farewell party:​
For the front-liners’ work is over,​
Remains is our task​
To restore our victory:​
“The giant has fallen:​
The nation​
Mourns”​
Rest in eternal peace,​
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere:​
Cc 1999​
( for the first president of Tanzania and founder of the nation, the late Mwalimu Julius Nyerere.​
may the lord God grant him eternal peace, Amen)​
 
Mkuu hebu punguza porojo za mtaani kidogo......Hivi sasa kuna TV za kumwaga, hicho kiwanda cha TV Tanzania kiko wapi?.......Mbona hakukataza magari wakati nchi haikuw na kiwanda cha magari? Hivi TV zilianza lini kuonekana Tanzania?

porojo zipi.?????
mbona nguo zilikuwa hakuna na sasa nguo zipo?????\
mbona sukari na sigara zilikuwa hakuna na sasa vipo???????

hapa tunazungumza wakati wa nyerere....

nyerere mbona alizuia nguo kutoka nje ili viwanda vya ndani vitosheleze soko
na matokeo yake,watu wakatembea uchi huko mtwara mpaka mitumba ikaruhusiwa...

sera ya nyerere ilikuwa kutokuagiza vitu vya luxury
na vitu vya msingi tutengeneze wenyewe

ndio maana alikuwa na viwanda vya baiskeli,sio magari,radio,sio tv
na majembe sio matrekta

wewe ndo una porojo naona
 
Afadhali umeanza kwa kucheka kwa kuwa unajua kabisa kuwa hayo ni maneno ya mtaani kama yale ya hadithi ya "Kawawa funika kikombe". Lizzy darling, acha kusikiliza maneno ya vijiweni!
Waswahili walisema “lisemwalo lipo kama halipo laja“ in this case hatuwezi kusubiria lije ila inawezekana lilikuwepo!!!The analyst asante sana kwa mchanganuo wako!!
 
nilipochaguliwa kuwa kiranja mkuu tarehe 13/09/99,kesho yake mwalimu alifariki,kwa heshima hiyo nilimtunuku hili ktk kitabu cha rambirambi

Mwalimu JK Nyerere ambaye ndo tunayemzungumzia hapa alifariki tarehe 14/10/1999

Sasa sijui mwalimu unayemtaja kwamba alifariki siku moja baada ya wewe kukamata madaraka 13/09/1999 ni yupi??

Ama kumbukumbu yako haiko makini?
 
porojo zipi.?????
mbona nguo zilikuwa hakuna na sasa nguo zipo?????\
mbona sukari na sigara zilikuwa hakuna na sasa vipo???????

hapa tunazungumza wakati wa nyerere....

Mkuu hapa tunazungumzia policy za Nyerere kama zilifanya kazi au hazikufanya.., au Kama Nyerere aliyadhibiti makabila fulani..., ???
Kujibu maswali yako policy za ujamaa hazikufaa na sio Tanzania tu bali nchi zote zilizojaribu.

Kuhusu ukabila, maybe Nyerere hakutaka makabila makubwa kuyazidi sana makabila mengine and in so doing kuyameza mengine. Think on Nyerere's Shoes..., Tumeshamfukuza Mkoloni sababu alikuwa anawabagua wazawa, je tukiwapa nchi baadhi ya watu huoni kuwa maybe kuna uwezekano wa kutengeneza wakoloni wengine ambao tuna ngozi sawa na tumetoka sehemu moja..., Ndio ni kweli hata sasa tunao wakoloni wengine mafisadi lakini huwezi kumshambulia mtu kwa kutaka kuzuia hilo...., Kumbuka by then kulikuwa kuna shida ya undugunization ambao kwa sasa haupo.

Kumbuka makabila kama mawili ndio yalikuwa makubwa sasa haya ndio yangekuwa na viongozi tunge-end up na kuanzia president mpaka messenger kabila moja (back to ukoloni) lakini kama na haya mengine yakichanganywa basi huenda yakadilute undugunization
 
porojo zipi.?????
mbona nguo zilikuwa hakuna na sasa nguo zipo?????\
mbona sukari na sigara zilikuwa hakuna na sasa vipo???????

hapa tunazungumza wakati wa nyerere....

nyerere mbona alizuia nguo kutoka nje ili viwanda vya ndani vitosheleze soko
na matokeo yake,watu wakatembea uchi huko mtwara mpaka mitumba ikaruhusiwa...

sera ya nyerere ilikuwa kutokuagiza vitu vya luxury
na vitu vya msingi tutengeneze wenyewe

ndio maana alikuwa na viwanda vya baiskeli,sio magari,radio,sio tv
na majembe sio matrekta

wewe ndo una porojo naona
Haya, Mwalimu Nyerere hayuko madarakani tangu 1985....hivyo viwanda vya magari viko wapi? Vya TV viko wapi? Vya nguo viko vingapi? Na hivyo viwanda vya radio viko wapi?.......Acheni kumsema mzee wa watu bana... At least yeye alichukua nchi mikononi mwa wakoloni, hatukuwa na wasomi wa kutosha....hivi sasa nchi tunapeana kama peremende, wasomi kibao...tunafanya nini? Tuko wapi?.........

Na hizo nguo unazosema sasa hivi zipo bwerere, ndo hii mitumba tunayouziwa mpaka chupi? Agrrrrrr! Tunathubutu kutamba kuvaa mitumba baada ya miaka 50 ya uhuru na zaidi ya miaka 27 tangu Nyerere atoke madarakani?
 
yaani nyerere mawazo yake yalikuwa finyu mpaka na yeye yamem cost

kutokuwepo kwa tv matokeo yake hotuba zake za tv zipo mbili tu....
na zilichukuliwa akiwa sio rais...na ni itv na channel ten tu ndo wanazo....
zingine nzuri hazipo kwenye tv

kitabu ni historia ya edwin mtei kimezinduliwa hivi karibuni

waulize watu wa chadema watakupa

Signature ya invisible ina maneno kwamba ficha upumbavu wako, onyesha hekima yako.

Leo hii tunaelekea kutimiza miaka 12 tangu mwalimu alipofariki lakini bado sehemu kubwa ya watanzania wanamkumbuka na kufanya reference kwake, wanafanya reference kwa uchapaji kazi wake, wanafanya reference kwa uzalendo wake, wanafanya reference kwa uwajibikaji wake, wanafanya reference kwa uongozi wake mahiri na kila aina ya utendaji wake.

Huwezi kumlinganisha mwalimu na hawa wanamagamba wa sasahivi, mwalimu alikuwa na vision sio hawa vilaza wa sasa hivi. Wewe mwenyewe huwezi kujilinganisha na mwalimu at any level na katika jambo lolote, ni mwendawazimu tu ndiye anaweza kusimama mbele ya hadhara na kusema kwamba mwalimu alikuwa na mawazo finyu, ni mwendawazimu pekee anyeweza kufanya hivyo!!
Eti ime-mcost? imemcost nini? kufariki? hilo nalo ni jambo la ajabu?kwani mwalimu hakuwa mwanadamu?mwanadamu kufa ni lazima au wewe unadhani mwalimu alikuwa malaika?

Kama tatizo lako ni tv, ni tatizo lako binafsi, si tatizo la watanzania wengi, kuna watu ndani ya nchi hii tv sio kipaumbele kwao
Radio ndio chombo pekee cha mawassiliano kinachoweza kuwafikia hata wale walioko vijijini mno, ambao angalau wanaweza kumudu kununua kiredio cha mkulima na kusikiliza. Kwahiyo hotuba zake kutokuwepo kwenye tv sio issue kabisa as long sauti yake ipo kwenye audio, mtu akitaka kupata ujumbe wa mwalimu anaupata. Tatizo lako nadhani unapenda kuuza sura kama viongozi wako wa sasahivi wanavyopenda kuuza sura ndio maana unalalam kutokuiona sura ya mwalimu kwenye tv. Mwalimu alikuwa anajali zaidi kuchapa kazi na kuwatumikia watanzania, sio kama hawa wasanii wenu wanaopenda kuuza sura lakini utendaji na uwajibikaji ni sifuri!!
 
Haya, Mwalimu Nyerere hayuko madarakani tangu 1985....hivyo viwanda vya magari viko wapi? Vya TV viko wapi? Vya nguo viko vingapi? Na hivyo viwanda vya radio viko wapi?.......
Yaani hata vile vichache vilivyokuwepo sasa havipo..............???, lakini dont worry kuna maendeleo sasa hivi watu wengi wanaendesha magari, ajira za machinga, mabar maid zimeongezeka..., watu tuna simu za mchina za kumwaga ukienda dukani kuna choice ya vitu kibao ingawa vyote havitoki nchini..., kweli maisha bora kwa kila mtanzania...., Nyerere alituchelewesha kuiuza nchi yetu..., tungeanza kuiuza miaka kumi iliyopita nadhani tungeshaimaliza hii kazi ambayo tunaifanya sasa.
 
Nadhani tusiangalie aliyoyasema bali aliyoyafanya na impact zake; na tujiulize isingekuwa hivyo tungekuwa wapi......

Baadhi ya makabila sababu ya undugunization yangekuwa juu zaidi hata kushinda ilivyo sasa, therefore kuleta matabaka makubwa, (Chagga, Haya to name just a Few)

Maybe baada ya kuona wenzetu wa mikoa ya Mara n.k. (kulingana na what is even happening now) ilikuwa ni vema waingie kwenye jeshi to utilize their fighting spirit

Kwahiyo kwa kutumia tactics na kuona culture and strengths za kila kabila directly or indirectly aliwabana au kuwaachia katika nyanja tofauti..., sio kwamba ni mkabila bali ni kwa kufanya kile alichoamini be it good or bad...
hakuna kitu kama hicho aliweka Wakurya kumlinda madarakani ukiangalia vizuri kabila Wazanaki ni la kufikirika yaani ni sehemu ya Wakurya!
 
Mkuu hapa tunazungumzia policy za Nyerere kama zilifanya kazi au hazikufanya.., au Kama Nyerere aliyadhibiti makabila fulani..., ???
Kujibu maswali yako policy za ujamaa hazikufaa na sio Tanzania tu bali nchi zote zilizojaribu.

Kuhusu ukabila, maybe Nyerere hakutaka makabila makubwa kuyazidi sana makabila mengine and in so doing kuyameza mengine. Think on Nyerere's Shoes..., Tumeshamfukuza Mkoloni sababu alikuwa anawabagua wazawa, je tukiwapa nchi baadhi ya watu huoni kuwa maybe kuna uwezekano wa kutengeneza wakoloni wengine ambao tuna ngozi sawa na tumetoka sehemu moja..., Ndio ni kweli hata sasa tunao wakoloni wengine mafisadi lakini huwezi kumshambulia mtu kwa kutaka kuzuia hilo...., Kumbuka by then kulikuwa kuna shida ya undugunization ambao kwa sasa haupo.

Kumbuka makabila kama mawili ndio yalikuwa makubwa sasa haya ndio yangekuwa na viongozi tunge-end up na kuanzia president mpaka messenger kabila moja (back to ukoloni) lakini kama na haya mengine yakichanganywa basi huenda yakadilute undugunization
well nakuelewa sasa baada ya kuyapinga, then kwanini aliua vyama vyao vya ushirika through nationalization ambavyo ni jasho lao yaani KNCU na KCU?
 
hakuna kitu kama hicho aliweka Wakurya kumlinda madarakani ukiangalia vizuri kabola Wazanaki ni la kufikirika yaani ni sehemu ya Wakurya!
Atleast aliwapa watu kazi wanayoweza kuifanya kuliko wengine wanaowapa watu kazi sababu wasiyoiweza...., bali kuwatafutia ulaji
 
Haya, Mwalimu Nyerere hayuko madarakani tangu 1985....hivyo viwanda vya magari viko wapi? Vya TV viko wapi? Vya nguo viko vingapi? Na hivyo viwanda vya radio viko wapi?.......Acheni kumsema mzee wa watu bana... At least yeye alichukua nchi mikononi mwa wakoloni, hatukuwa na wasomi wa kutosha....hivi sasa nchi tunapeana kama peremende, wasomi kibao...tunafanya nini? Tuko wapi?.........

Na hizo nguo unazosema sasa hivi zipo bwerere, ndo hii mitumba tunayouziwa mpaka chupi? Agrrrrrr! Tunathubutu kutamba kuvaa mitumba baada ya miaka 50 ya uhuru na zaidi ya miaka 27 tangu Nyerere atoke madarakani?

Kiongozi, mwalimu alituanzishia viwanda kedekede lakini tangu amefariki tumeviua ama kuvitoa bwerere kwa wakwapuaji wanaojiita wawekezaji.

Mwalimu alitujengea kiwanda cha redio-philips arusha kimekufa, mwalimu alitujengea viwanda vya nguo-kilitex, mwatex,mutex na vingine vingi lakini vyote kwishney.
Mwalimu alitujengea reli ya kati, ona tunavyohangaika na wahindi sasahivi. Mwalimu alitujengea mitambo ya kufua umeme ya kihansi, mtera na kwingineko, angalia sasahivi mgao wa umeme unavyotuhangaisha hadi kufikia kukaa gizani masaa 16 kwa siku!! Kweli kuna watu hawana shukrani kabisa ama sijui ni chuki binafsi!!??

Halafu kweli mtu na akili yake timamu anaweza kuja kumshutumu mwalimu? yes yeye kama binadamu alikuwa na mapungufu yake kama tulivyo sisi lakini ukiangalia mambo aliyoyafanya kwa nia njema ya kuwasaidia watanzania wenzake huwezi kumlinganisha na hawa wasanii wanaouza nchi yetu huku wakijua kwamba wanaiuza!!
 
Mkuu nami nilikuwepo na nipo hadi sasa. Pamoja na kuwasweka ndani watu lakini Nyerere alikuwa akipendwa na wengi. Huwezi kupendwa na kila mtu lazima wawepo wengine ambao hawakupendi lakini kwa ujumla ni kwamba alikuwa anapendwa. Kuhusu kukoswa koswa kupinduliwa ukilinganisha na Marais wengine utakuwa hutendi haki kwa kuwa kwenye miaka ya 90s Africa ilianza kunusa demokrasia ukilinganisha na miaka ya 60s na 70s ambapo demokrasia kwa Africa ilikuwa ndoto. Kipindi baada ya uhuru kwa nchi nyingi Africa kilitawaliwa na ubabe pamoja na udikteta kwa hiyo waroho wa Madaraka waliona hakuna njia nyingine ya kuchukua hatamu za uongozi zaidi ya kutumia mtutu wa bunduki. Miaka baada ya uhuru kulikuwa hakuna chaguzi za ushindani africa, vyama vingi vya siasa vilipigwa marufuku.

Kuhusu mada ni kwamba Nyerere hakuwa mkabila wa waziwazi lakini alikuwa na vimelea vya ukabila. Hakupenda Makabila kama Wachaga ambao wengi waliosomeshwa kupitia KNCU, Wahaya kupitia KCU pamoja na Wanyakyusa (ambao sijui walipata wapi bahati ya kusoma) waje kuchukua uongozi wa juu wa nchi kwa kuwa wangekuwa na solidarity na kupeana madaraka na kuyapuuza makabila mengine kama wakurya ambao elimu yao ilikuwa chini sana baada ya wakoloni kuwaona kuwa wanaweza tu kufungua bunduki na kupiga na wala siyo kufungua kurasa za vitabu.

Ninyi nao ni wabaguzi tu kama makaburu, mnazungumzia wahaya na KCU, wachagga na KNCU na Wanyakyusa (!), hamzungumzii kabisa wasukuma kabila kubwa kabisa kupita yote Tanzania na chama chao cha ushirika enzi hizo VFCU. Maendeleo ya Chama hiki chini ya Paul Bomani kilikuwa na nguvu za kiuchumi hadi Nyerere alihofia madaraka yake. Ali hakikisha wasukuma hawapati elimu ya maana ili asijetokea mtu wa kabila hili akawa na nguvu ya kisiasa.
 
Atleast aliwapa watu kazi wanayoweza kuifanya kuliko wengine wanaowapa watu kazi sababu wasiyoiweza...., bali kuwatafutia ulaji
Kwa hiyo sentensi yako ya kwanza naomba niulize sasa mbona hakuwapa Wachagga na Wahaya kazi ambayo obviously walikua wanaiweza sana?!Kuleta maendeleo kwa kuwaachia nafasi za uongozi that is!
 
Ninyi nao ni wabaguzi tu kama makaburu, mnazungumzia wahaya na KCU, wachagga na KNCU na Wanyakyusa (!), hamzungumzii kabisa wasukuma kabila kubwa kabisa kupita yote Tanzania na chama chao cha ushirika enzi hizo VFCU. Maendeleo ya Chama hiki chini ya Paul Bomani kilikuwa na nguvu za kiuchumi hadi Nyerere alihofia madaraka yake. Ali hakikisha wasukuma hawapati elimu ya maana ili asijetokea mtu wa kabila hili akawa na nguvu ya kisiasa.
ndo maana akamtumia Bomani huyohuyo kuuwa KNCU baada ya Nyanza Cooperative Union kufa sio? Grow up acha propaganda NCU kiliuwawa na Wasukuma wenyewe kwa ubadhirifu! rekodi zipo..
 
Back
Top Bottom