Mwalimu Nyerere na ukabila

Nadhani tusiangalie aliyoyasema bali aliyoyafanya na impact zake; na tujiulize isingekuwa hivyo tungekuwa wapi......

Baadhi ya makabila sababu ya undugunization yangekuwa juu zaidi hata kushinda ilivyo sasa, therefore kuleta matabaka makubwa, (Chagga, Haya to name just a Few)

Maybe baada ya kuona wenzetu wa mikoa ya Mara n.k. (kulingana na what is even happening now) ilikuwa ni vema waingie kwenye jeshi to utilize their fighting spirit

Kwahiyo kwa kutumia tactics na kuona culture and strengths za kila kabila directly or indirectly aliwabana au kuwaachia katika nyanja tofauti..., sio kwamba ni mkabila bali ni kwa kufanya kile alichoamini be it good or bad...
 
Ukweli ni kwamba Nyerere alikuwa dikteta kwa definition ya udikteta ya Ulaya Magharibi (by then). Ila kwa viwango vya Africa kwa wakati huo Nyerere alikuwa nafuu sana kulinganisha na viongozi wengine Madkiteta wa Africa ambao walikuwa wakiwaua wapinzani wao kwa maelfu. Nyerere alikuwa akiwanyima uhuru wapinzani wake kwa kuwapeleka huko vijijini na hawakutakiwa kufika mjini kujua nini kinaendelea. Mfano Kasanga Tumbo na Mzee Mapalala! Alikuwa Dikteta ila alikuwa si muuaji kama madikteta wengine wa Afrika wa enzi zake.

Ni kweli kabisa, kwa jinsi hali ya Siasa ya Bara la Afrika ilivyokuwa kipindi kile baada ya Uhuru kulikuwa hakuna namna nyingine bali kuongoza nchi kwa misingi ya "Udikteta" ili kuweza kuwaunganisha wananchi na kufikia lengo moja la Maendeleo..

Binafsi sijawahi kukutana na maandishi au maneno ya Nyerere kuhusu kukataza makabila makubwa ya kipindi kile kushika nafasi za juu za madaraka, ila inaingia akilini kuwa iwapo haya makabila yangekamata madaraka ya juu basi kwa kiasi kikubwa nafasi za upendeleo zingeelekezwa kwao kuliko kwa makabila mengine.. Tuchukulie mfano tangu enzi za Nyerere mpaka leo hii, ni makabila gani yanayoongoza kwa kushika nyadhifa Serikalini? Makatibu wakuu wa wizara? Wakuu wa vyuo vikuu, Shule za Sekondari n.k....
 
Mkuu nami nilikuwepo na nipo hadi sasa. Pamoja na kuwasweka ndani watu lakini Nyerere alikuwa akipendwa na wengi. Huwezi kupendwa na kila mtu lazima wawepo wengine ambao hawakupendi lakini kwa ujumla ni kwamba alikuwa anapendwa. Kuhusu kukoswa koswa kupinduliwa ukilinganisha na Marais wengine utakuwa hutendi haki kwa kuwa kwenye miaka ya 90s Africa ilianza kunusa demokrasia ukilinganisha na miaka ya 60s na 70s ambapo demokrasia kwa Africa ilikuwa ndoto. Kipindi baada ya uhuru kwa nchi nyingi Africa kilitawaliwa na ubabe pamoja na udikteta kwa hiyo waroho wa Madaraka waliona hakuna njia nyingine ya kuchukua hatamu za uongozi zaidi ya kutumia mtutu wa bunduki. Miaka baada ya uhuru kulikuwa hakuna chaguzi za ushindani africa, vyama vingi vya siasa vilipigwa marufuku.

Kuhusu mada ni kwamba Nyerere hakuwa mkabila wa waziwazi lakini alikuwa na vimelea vya ukabila. Hakupenda Makabila kama Wachaga ambao wengi waliosomeshwa kupitia KNCU, Wahaya kupitia KCU pamoja na Wanyakyusa (ambao sijui walipata wapi bahati ya kusoma) waje kuchukua uongozi wa juu wa nchi kwa kuwa wangekuwa na solidarity na kupeana madaraka na kuyapuuza makabila mengine kama wakurya ambao elimu yao ilikuwa chini sana baada ya wakoloni kuwaona kuwa wanaweza tu kufungua bunduki na kupiga na wala siyo kufungua kurasa za vitabu.

Sina haja ya kubishana kuhusu nyerere, lakini wewe mwenyewe jijibu kuhusu hayo makabila uliyoyataja, Jee, ndio hao hao? halafu ongeza waislaam ambao aliwafunga masheikh wao wakubwa woote, hakuna sheikh wa kiislaam aliyekuwa maarufu ambae hajaonja joto la chuki za nyerere. Ukisha waongeza hao na wafuasi wao, ongeza na watu kama Mwamwindi walikuwa wangapi? halafu ongeza wafuasi wakina Kambona, Kasela Bantu, Bibi Titi na walio kama hao, ukipata jibu. Utajaza mwenyewe.

Hakuna kipindi Tanzania ilikuwa kwenye furaha kama katika uongozi wa Mwinyi, akipita tuu njiani watu walikuwa wakishangilia Ruksa, Ruksa, Ruksa, umesha jiuliza kwanini?
 
kuna story ameandika edwin mteikwenye kitabu chake ukiisomana ukisikia uvumi kuwa alikuwa na matatizo ya kama ugonjwa hivi wa mentall hivi unaweza connect the dotsmfano nyerere alikuwa impulsive sanaanalipuka lipuka mno....kwenye kitabu mtei anasema aliwapeleka wazungu wa imf ikulu,nyerere badala hata ya kuwasikilza na kukataa,akasusa kuonana nao.wakati mwanzo alikubali waje ikulu.yaani aibu tupu,mtei akamkuta nyerere yuko nje ya ikulu kanuna hataki hata kuongea...na ukichanganya na jinsi zoezi la vijiji vya ujamaa lilivyopelekwayaani watu walihamishwa wakapelekwa kwenye mapori waanzishe hivyo vijiji wengine wakaliwa na simbana ukiangalia mfano sera yake ya marufuku magari,ni baiskeli tuunaweza ona
Nilisikia kwamba na TV pia hakupenda watu binafsi wamiliki!Hicho kitabu kinaitwaje?!Ningefurahi kweli kukipata!!!
 
Nadhani tusiangalie aliyoyasema bali aliyoyafanya na impact zake; na tujiulize isingekuwa hivyo tungekuwa wapi......Baadhi ya makabila sababu ya undugunization yangekuwa juu zaidi hata kushinda ilivyo sasa, therefore kuleta matabaka makubwa, (Chagga, Haya to name just a Few)Maybe baada ya kuona wenzetu wa mikoa ya Mara n.k. (kulingana na what is even happening now) ilikuwa ni vema waingie kwenye jeshi to utilize their fighting spiritKwahiyo kwa kutumia tactics na kuona culture and strengths za kila kabila directly or indirectly aliwabana au kuwaachia katika nyanja tofauti..., sio kwamba ni mkabila bali ni kwa kufanya kile alichoamini be it good or bad...
Alichoamini kama hakikua kizuri alifanya kwa faida ya nani?!?!Nani anaejua kwa uhakika kwamba angeruhusu hayo makabila kuongoza huo “undugunization“ ungetawala?!
 
kwenye kitabu mtei anasema aliwapeleka wazungu wa imf ikulu,
nyerere badala hata ya kuwasikilza na kukataa,akasusa kuonana nao.
wakati mwanzo alikubali waje ikulu.
yaani aibu tupu,mtei akamkuta nyerere yuko nje ya ikulu kanuna hataki hata kuongea...

Hapo penye bold pameniacha sina mbavu..
Ina maana jamaa aliamua kuwaachia Ikulu mradi tu asionane nao?
Ina maana alikuwa tayari hata kunyeshewa na mvua mradi asiingie kwenye Ofisi yake mwenyewe?
LOL..........
 
Kwa kweli Nyerere alikuwa Na mawazo ya Ujamaa, alitaka kujenga nchi ya usawa, Nyerere alikuwa Mzalendo wa kweli, Japo sehemu kubwa ya Watu aliowaamini wengi walikuwa watu wa Musoma, Mfano siku za mwanzo wa utawala wake alikuwa karibu sana na mdogo wake Marehemu Joseph Nyerere, Mtu kama Butiku ni msaidizi wake wa muda mrefu sana na ni ndugu yake wa Karibu, Lakini Pia hata shemeji yake Lawrence Gama ambaye alikuwa Mume wa dada yake Sophia nyerere hakumsahau wakati wote, Hata Sohia Nyerere alipofariki Gama aliendelea kuwa karibu na Mwalimu.Hawa ni baadhi ya Jamaa zake wa karibu.Lakini Pia nyerere alikuw muoga sana wa Makabila makubwa, alikuwa anaogopa nchi isije ikamezwa na Makabila makubwa. Na ni kweli baadhi ya makabila hayaangushani, hiyo tunajua wazi na mifano tunayo, japo yapo makabila ambayo mtu akiwa juu hataki wengine wamfuate anataka awakanyage chini na waendelee kumsujudia, Mifano tunayo.
Ukabila ni sumu tunaona Kenya, Rwanda na Burundi.
 
Sina haja ya kubishana kuhusu nyerere, lakini wewe mwenyewe jijibu kuhusu hayo makabila uliyoyataja, Jee, ndio hao hao? halafu ongeza waislaam ambao aliwafunga masheikh wao wakubwa woote, hakuna sheikh wa kiislaam aliyekuwa maarufu ambae hajaonja joto la chuki za nyerere. Ukisha waongeza hao na wafuasi wao, ongeza na watu kama Mwamwindi walikuwa wangapi? halafu ongeza wafuasi wakina Kambona, Kasela Bantu, Bibi Titi na waliokama hao, ukipata jibu. Utajaza mwenyewe.

Zomba. Hata Sheikh Yahya na AMNUT, Sheikh Nurdin Hussein (Mwenyezi Mungu Awarehemu) na wengine wengi wanayajua machungu ya Nyerere. Mada iliyokuwa mezani ni ukabila nami nimechangia kwenye ukabila siyo udini manake ukiongelea masheikh unaongelea udini. Kama ni mada ya udini basi iwekwe tuiongelee.
 
Aisee nyie watu hapo juu............

Hebu mwacheni mzee wa watu apumzike kwa amani.....

Nyerere baba wa taifa langu............. The African Hero.............RIP mzee wangu. Usifufuke manake ukifufuka ukakuta waliyoyafanya hawa watu uliowaachia hii nchi, hakika utakufa tena! Ubazazi, ubaradhuli na wizi mtupu!
 
Nilisikia kwamba na TV pia hakupenda watu binafsi wamiliki!Hicho kitabu kinaitwaje?!Ningefurahi kweli kukipata!!!

yaani nyerere mawazo yake yalikuwa finyu mpaka na yeye yamem cost

kutokuwepo kwa tv matokeo yake hotuba zake za tv zipo mbili tu....
na zilichukuliwa akiwa sio rais...na ni itv na channel ten tu ndo wanazo....
zingine nzuri hazipo kwenye tv

kitabu ni historia ya edwin mtei kimezinduliwa hivi karibuni

waulize watu wa chadema watakupa
 
Alichoamini kama hakikua kizuri alifanya kwa faida ya nani?!?!Nani anaejua kwa uhakika kwamba angeruhusu hayo makabila kuongoza huo "undugunization" ungetawala?!

Nadhani kuna tofauti kati ya mtu anapokupa sumu akidhani kwamba anakupa dawa na yule anayekupa sumu ili akuuwe.., wa kwanza hata kama anafanya baya anadhani anafanya zuri..., Kuhusu nani anadhani for sure.... history can tell us ndio sababu mpaka sasa watu wengi wanadhani kwamba mmasai ndio mlinzi mzuri au mkurya ndio mwanajeshi mzuri, ni kutokana na culture na historia za makabila. Kuhusu undugunization huo upo mpaka sasa and by then kuna makabila machache ambayo ndio yalikuwa na wasomi na wajuaji so give them power kungekuwa na uwezekano mkubwa wa mwenye nacho kuongezewa na asiyenacho kunyanganywa so maybe he was just putting a level playing field.

A good leader ni yule anayefanya what he believes in he just takes action, hakuna kubahatisha..., saying that sio kwamba nasema the guy was an Angel la Hasha., lakini alifanya what he really thought was good kuliko viongozi wa sasa ambao wanatupeleka shimoni huku wakijua.
 
Mkuu nami nilikuwepo na nipo hadi sasa. Pamoja na kuwasweka ndani watu lakini Nyerere alikuwa akipendwa na wengi. Huwezi kupendwa na kila mtu lazima wawepo wengine ambao hawakupendi lakini kwa ujumla ni kwamba alikuwa anapendwa. Kuhusu kukoswa koswa kupinduliwa ukilinganisha na Marais wengine utakuwa hutendi haki kwa kuwa kwenye miaka ya 90s Africa ilianza kunusa demokrasia ukilinganisha na miaka ya 60s na 70s ambapo demokrasia kwa Africa ilikuwa ndoto. Kipindi baada ya uhuru kwa nchi nyingi Africa kilitawaliwa na ubabe pamoja na udikteta kwa hiyo waroho wa Madaraka waliona hakuna njia nyingine ya kuchukua hatamu za uongozi zaidi ya kutumia mtutu wa bunduki. Miaka baada ya uhuru kulikuwa hakuna chaguzi za ushindani africa, vyama vingi vya siasa vilipigwa marufuku.

Kuhusu mada ni kwamba Nyerere hakuwa mkabila wa waziwazi lakini alikuwa na vimelea vya ukabila. Hakupenda Makabila kama Wachaga ambao wengi waliosomeshwa kupitia KNCU, Wahaya kupitia KCU pamoja na Wanyakyusa (ambao sijui walipata wapi bahati ya kusoma) waje kuchukua uongozi wa juu wa nchi kwa kuwa wangekuwa na solidarity na kupeana madaraka na kuyapuuza makabila mengine kama wakurya ambao elimu yao ilikuwa chini sana baada ya wakoloni kuwaona kuwa wanaweza tu kufungua bunduki na kupiga na wala siyo kufungua kurasa za vitabu.

MKuu hiyo red hata kama ni kweli ulitakiwa utumie mins nyingine ya kufikisha ujumbe, so mkuu naomba ututake radhi :msela:
 
Zomba. Hata Sheikh Yahya na AMNUT, Sheikh Nurdin Hussein (Mwenyezi Mungu Awarehemu) na wengine wengi wanayajua machungu ya Nyerere. Mada iliyokuwa mezani ni ukabila nami nimechangia kwenye ukabila siyo udini manake ukiongelea masheikh unaongelea udini. Kama ni mada ya udini basi iwekwe tuiongelee.

Soma mstari wa kwanza wa mada tajwa na tazama post niliyoijibu mimi, nilijibu kuhusiana na kupendwa kwa nyerere ambako mtowa mada ame "depict", mimi nikasema hajapendwa na wengi, wewe ukajibu ulichojibu, mimi nikakupa hesabu ndogo ya makundi ambayo hayana sababu ya kumpenda nyerere na hili unaloandika hapo juu linaongezea katika hayo makundi. My point is, nyerere hakupendwa na wengi kama mtoa mada anavyofikiria. Mengine nilimwambia atajaza mwenyewe.
 
Aisee nyie watu hapo juu............Hebu mwacheni mzee wa watu apumzike kwa amani.....Nyerere baba wa taifa langu............. The African Hero.............RIP mzee wangu. Usifufuke manake ukifufuka ukakuta waliyoyafanya hawa watu uliowaachia hii nchi, hakika utakufa tena! Ubazazi, ubaradhuli na wizi mtupu!
Sindio aliodhani wataiweza kazi!?Angerudi aone ni kwa kiasi gani alidanganyika/jidanganya!!!
 
yaani nyerere mawazo yake yalikuwa finyu mpaka na yeye yamem costkutokuwepo kwa tv matokeo yake hotuba zake za tv zipo mbili tu....na zilichukuliwa akiwa sio rais...na ni itv na channel ten tu ndo wanazo....zingine nzuri hazipo kwenye tvkitabu ni historia ya edwin mtei kimezinduliwa hivi karibuniwaulize watu wa chadema watakupa
Hahahha....mi nilivyosikia ni kwamba hakutaka watuwawe na tv ili wasijue yanayoendelea nje ya sehemu walipo...sasa yeye kwasababu anayo anakuja kuwadanganya ana maono haya na yale kuhusu ulimwengu unapoelekea.Siku ya pili watu wakisikia zile habari kwenye redio au sijui kwenye magazeti basi wanazidi kumwamini maana anajua mambo!!!Ntakitafuta!!!
 
Nadhani kuna tofauti kati ya mtu anapokupa sumu akidhani kwamba anakupa dawa na yule anayekupa sumu ili akuuwe.., wa kwanza hata kama anafanya baya anadhani anafanya zuri..., Kuhusu nani anadhani for sure.... history can tell us ndio sababu mpaka sasa watu wengi wanadhani kwamba mmasai ndio mlinzi mzuri au mkurya ndio mwanajeshi mzuri, ni kutokana na culture na historia za makabila. Kuhusu undugunization huo upo mpaka sasa and by then kuna makabila machache ambayo ndio yalikuwa na wasomi na wajuaji so give them power kungekuwa na uwezekano mkubwa wa mwenye nacho kuongezewa na asiyenacho kunyanganywa so maybe he was just putting a level playing field.A good leader ni yule anayefanya what he believes in he just takes action, hakuna kubahatisha..., saying that sio kwamba nasema the guy was an Angel la Hasha., lakini alifanya what he really thought was good kuliko viongozi wa sasa ambao wanatupeleka shimoni huku wakijua.
Nimekusoma na nimekuelewa!Swali...kama alichokua hataki ni walionacho kuongezewa niambie nini haswa kinachoendelea Tanzania karne hii?!Na je leo hii ukiambiwa kwamba haya makabila makubwa yakichukua nchi yatawekana sana madarakani ila maendeleo yatakuwepo (maisha mazuri kwa kila mTanzania kama wanavyosema wanamagamba) utaona bora tutawaliwe na mchanganyiko usio na muelekeo au kundi moja linalojua nini linafanya?!?!
 
Ni kigezo gani kinatumika kutambua Nyerere alipendwa au hakupendwa na watu wengi?

Mimi naamini Nyerere alipendwa na watu wengi kuliko rais yeyote aliyepata kutokea Tanzania.

Naamini pia ni Miongoni mwa viongozi mashuhuri Afrika waliopendwa na kuheshimika sana na waafrika.........Ukimuondoa Mandela, Nyerere anafunika vibaya....Anaweza fatiwa na kina Nkrumah, Lumumba, Samora na viongozi wa sampuli hii (wapigania uhuru)………Hawa wa siku hizi ni kama makapi tu.

Kwa Tanzania hii, hakuna kama Nyerere!.......Ndio maana pamoja na kuwa ameshatangulia mbele ya haki, bado watu wanazikumbuka busara zake na wanamkumbuka kwa mema mengi aliyoyafanya, tofauti na maraisi wastaafy wengine ambao hata huwa hawakumbukwi kwa mema zaidi ya mabaya.
 
Hahahha....mi nilivyosikia ni kwamba hakutaka watuwawe na tv ili wasijue yanayoendelea nje ya sehemu walipo...sasa yeye kwasababu anayo anakuja kuwadanganya ana maono haya na yale kuhusu ulimwengu unapoelekea.Siku ya pili watu wakisikia zile habari kwenye redio au sijui kwenye magazeti basi wanazidi kumwamini maana anajua mambo!!!Ntakitafuta!!!
Afadhali umeanza kwa kucheka kwa kuwa unajua kabisa kuwa hayo ni maneno ya mtaani kama yale ya hadithi ya "Kawawa funika kikombe". Lizzy darling, acha kusikiliza maneno ya vijiweni!
 
Imekuwa vizuri umeuliza jambo hili. Hata mimi niliwahi kujiuliza sana swala hili lakini nilichokuja kugundua baada ya kutafiti sana ni nivi; Kwanza watanzania wengi bado tuna mentality nyingi za kikabila na kidini na kwa kuwa uwezo wetu wa kujifunza mambo mengine kwa undani ili kukwepa mitazamo hiyo michafu imeshindikana basi kila tunachoshindwa kukielewa majibu yake huwa dini au kabila.
Fuatilia hata milolongo ya threads za kuponda ufisadi. Utagundua dini inavyoingizwa ndani kama jibu rahisi kwa maswali magumu. Watu wengi tumeshindwa kujua ni kwa nini hakuna rais mchaga, mhaya wala mnyakyusa wakati makabila haya yana watu wengi na walijaaliwa kuziona shule mapema na kuzipenda. Kwa kuwa sababu zinaanzia wakati wa mapambano dhidi ya mkoloni na sisi hatupendi wala kuweza kusoma maelezo marefu tumeshindwa kujua hasa ni kwa nini haijatokea watu hawa kuingia madarakani wakati makabila madogo kama Zanaki, lile la Mkapa na wakwere wameweza kufika huko.
Kwa sababu hiyo hiyo tumeshindwa kujua kuwa kwa mujibu wa aina fulanifulani za mfumo wa siasa wasomi wengi huwa hawakimbilii sana Ikulu na wanashindwa kuwavutia wachaguaji maana wachaguaji/wapigakura wengi ktk nchi zetu hizi hata kufikia miaka ya karibuni wamekuwa watu wa kuahidiwa yasiyowezekana na kuhongwa chumvi na si kusikia ukweli na kuupima. Ninavyojua mimi wasomi wengi hawawezi uongo mwingi isipokuwa hawa wa siku hizi wa CCM.
Kwa sababu za ujinga wetu tumeamini kwamba maadamu mwalimu alikaa muda mrefu madarakani na hata baada ya kuondoka hajaacha mrithi kutoka miongoni mwa wasomi hawa basi alikusudia wasifike ikulu eti kwa kuwa wanapendeleana sana wakiwa katika nafasi. Inawezekana katika baadhi ya maeneo watu wanapendeleana kweli lakini tunapoanza kulaumu idadi ya wasomi katika sekta fulani wakati hatuhamasishi jamii zetu kujibidisha huu unakuwa uzumbukuku.
Mwalimu hakuwa hivyo na ninawaomba hata watawala watarajiwa kama CDM wanaosingiziwa kuwa wakabila wasiwape nafasi watu wajinga kusema ndiyo maana mwalimu aliwakwepa wakati si kweli.
:hug:I love myself, I love my family and I love my Country Tanzania (na hata itakapobakia Tanganyika).:hug:
Habari zenu jamani?!

Naomba nianze kwa kusema ukweli kwamba mimi sikuwepo kipindi cha utawala wa Mwl na hata alipofariki nilikua mdogo sana hivyo sikuwahi kujua kwanini watu wengi walikua wanampenda sana huku bado kukiwa na mambo mengi hasi yanayosemwa juu yake.Nafurahi kwamba mwaka huu nimeweza kutumia muda wangu kiasi nikasoma vitabu kadhaa kumhusu...makusanyo ya hotuba zake pamoja na vitabu alivyoandika mwenyewe.Kutokana na niliyoyasoma niliridhika kwamba sifa zote anastahili...pia kukosolewa maana yeye kama mtu mwingine yeyote yule makosa hatuwezi tuyakwepa.

Katika vitu ambavyo Mwl alivisimamia haswa ni usawa.Hakutaka kabila moja lijione/jisikie liko juu ya jingine na kutengeneza matabaka.Sasa swali langu nnaloomba mnisaidie ni hili....ule msemo au sijui niyaite madai ya kwamba Mwl aliwahi kusema makabila fulani hayafai kupewa uongozi wa juu wa nchi ni wa kweli au ni propaganda za waliomchukia?!Nauliza hivi kwasababu niliyoyasoma juu yake hayaendani kabisa na madai haya...na wala haileti maana kusikia kwamba aliyepigania usawa ndie aliyekua wa kwanza kutengeneza matabaka lilipokuja swala la uongozi!!!

Naomba majibu kama yapo yawe na vielelezo na yasiwe maneno ya kusikika na kufikirika tu ili tusiojua tujifunze kitu.
Asanteni!
 
Nadhani kuna tofauti kati ya mtu anapokupa sumu akidhani kwamba anakupa dawa na yule anayekupa sumu ili akuuwe.., wa kwanza hata kama anafanya baya anadhani anafanya zuri..., Kuhusu nani anadhani for sure.... history can tell us ndio sababu mpaka sasa watu wengi wanadhani kwamba mmasai ndio mlinzi mzuri au mkurya ndio mwanajeshi mzuri, ni kutokana na culture na historia za makabila. Kuhusu undugunization huo upo mpaka sasa and by then kuna makabila machache ambayo ndio yalikuwa na wasomi na wajuaji so give them power kungekuwa na uwezekano mkubwa wa mwenye nacho kuongezewa na asiyenacho kunyanganywa so maybe he was just putting a level playing field.

A good leader ni yule anayefanya what he believes in he just takes action, hakuna kubahatisha..., saying that sio kwamba nasema the guy was an Angel la Hasha., lakini alifanya what he really thought was good kuliko viongozi wa sasa ambao wanatupeleka shimoni huku wakijua.

Well said Kiongozi!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom