Mwalimu Nyerere Kiswahili Television

SolarPower

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
223
27
Wakuu,

Katika kuhakikisha kuwa tunaienzi Lugha yetu ya Kiswahili na kuieneza dunia nzima, nashauri tuanzishe kama taifa televisheni maalum ya Kiswahili kwa ajili ya kutimiza ndoto hiyo. Televisheni hiyo inapendekezwa iitwe MWALIMU NYERERE KISWAHILI TELEVISION.

Moja ya lengo lake kuu liwe ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2025 kila binadamu katika dunia hii awe na uwezo kwa kuzungumza kwa ufasaha Lugha Yetu ya Kiswahili.

Fedha za kufanikisha ndoto hii inapendekezwa zitokane na vyanzo mbalimbali. Baadhi ya vyanzo vinavyopendekezwa ni kama ifuatavyo:-

1. Kila Soda, Juice ya Chupa, Maji ya Chupa (kwa kila nusu lita) inayouzwa hapa nchini itozwe kodi ya shilingi 50 kwa ajili ya kueneza Lugha ya Kiswahili Duniani.

2. Kila gari ambalo si la Serikali lilipe Kodi Maalum ya Kiswahili ya shilingi elfu 3 kila wiki. Kwa magari ambayo ni ya Serikali kuu na serikali za mitaa, kodi yake ya Kiswahili inayopendekezwa ni shilingi milioni 5 kwa mwaka kwa gari.

3. Kila line ya simu ya mkononi iliyosajiliwa hapa nchini ilipiwe Kodi Maalum ya Kueneza Kiswahili Duniani ya Shilingi 50 kwa wiki.

4. kila bia inayozalishwa au kuuzwa hapa nchini itozwe kodi maalum ya Kiswahili ya Shilingi 200 kwa chupa/can moja yenye bia.

5. Kila Ounce moja ya Dhahabu inayozalishwa hapa nchini itozwe Kodi hii Maalum ya Kueneza Kiswahili Duniani ya USD 100.

Naomba Kuwasilisha
 
Back
Top Bottom