Mwalimu Mmoja wanafunzi 652

Chilisosi

JF-Expert Member
Oct 19, 2008
3,051
747
Oparation Sangara Mkoani Morogoro imekutana na shule yenye wanafunzi 652 na Mwalimu mmoja tu. Shule hiyo ipo katika Kijiji cha Kadodo Kata ya Luale, Mvomelo Mkoani Morogoro. Hii ndo hali halisi ya elimu Tanzania baada ya miaka 50 ya uhuru chini ya utawala wa kifisadi wa CCM.
Wakati Chadema wapo kwenye Oparation Sangara vuguvugu la mabadiliko vijijini na mjini hadi kwa Watanzania wanaoishi nchi za nje, CCM wao wanaandaa BBQ Party na Vinywaji vingi kwa wanachama wake walioko nchi za nje
. Mfano ni yanayojili katika Tawi lao la North London Uingereza

Habari ni kwa hisani ya
CHADEMA BLOG UK: Mwalimu mmoja wanafunzi 652
 
Samahani umesema, huyo ni nani? .... Mwl. mkuu?, ni mkuu wa nani? au mwanafunzi mkuu? ...mwl. wa nidhamu?... mwl. wa taaluma?.. mwl wa zamu? au ....?.. Hii Tanzania Bana ...nikiendelea kuumiza kichwa kwa yote ya miaka 50 nitapata pressure tu! ... ngoja nikalale!....
 
Chadema walichukua jukumu gani kuisaidia hiyo shule?
Ndugu mwanakijiji, Hata hatua ya Kutupatia hii taarifa inatosha, Inatusaidia kujua hali halisi ya watanzania wenzutu hasa walioko vijijini kabisa. Mi naamini kwa Kuileta hii shule mbele ya jamii ni msaada tosha kwani naamini wahusika watapata habari na kulifanyia kazi! sio kazi ya chadema kupeleka walimu kule ni kazi ya serikali ya CCM.
 
Back
Top Bottom