Mwalimu ajitokeza jimbo la Mkono

Geza Ulole

JF-Expert Member
Oct 31, 2009
59,203
79,433
20th December 09
Mwalimu ajitokeza jimbo la Mkono

George Marato

Mwalimu mmoja wa Shule ya Msingi wilayani Musoma ametangaza rasmi kugombea ubunge kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Mandeleo Chadema, katika jimbo la Musoma vijijini ambalo kwa sasa linaongozwa na wakili maarufu Nimrod Mkono.
Akizungumza na Nipashe Jumapili juzi, Choge Magori (45), ambaye kitaaluma ni mwalimu wa shule ya msingi alisema ameamua kuingia katika kinyang'anyiro hicho katika Uchaguzi Mkuu ujao ili kusadia wananchi kapata kiongozi anayejali shida za wanyonge na kuishi nao kwa muda wote.
Alisema kitendo cha kuchagua miaka yote wabunge matajiri bila kutaja uwezo huo wa fedha wameupataje kimechangia maendeleo kuelekezwa upande mmoja huku viongozi wa chama anachotoka mbunge wakishindwa kuhoji kwa vile hawezi kufanya hivyo kutokana na maisha yao kumtegemea.
Hata hivyo, Magori hakumtaja mbunge huyo tajiri ila wazi alilenga kumsema mbunge wa sasa wa Musoma Vijijini ambaye siku zote amekuwa akitumia uwezo wake kujenga shule za msingi, sekondari, barabara na zahanati.
Magori ambaye pia ni katibu wa Chadema katika Wilaya ya Musoma Vijijini alisema wakati wa kuleta maendeleo jimboni humo kwa kutumia nguvu kazi ya wananchi ni sasa bila kutegemea msaada wa mtu mmoja hali ambayo imedai inadumaza maendeleo ya wananchi hata kushindwa kushirikishwa katika miradi hiyo.
Alisema kuwa kitu kingine ambacho kimemsukuma ni wananchi kuhitaji mbunge anayefahamu vema mazingira yao kwa mfano wananchi wanahitaji pembejeo lakini mbunge wa sasa hawezi hatambua kilio cha wananchi.
“Mbunge unamchagua hajawahi kuwa na shamba je atawezeje kujua shida ya wananchi ya pembejeo haya shule zinajengwa lakini walimu wako wapi wao wanasomesha nje ya nchi lazima na mimi niende huko nikatoe mchango wangu kusaidia wananchi hawa wanyonge,” alisema.
Wakati kiongozi huyo wa Chadema akionyesha nia hiyo tayari kuna wana CCM zaidi ya watano wanadaiwa kuanza kupitapita jimboni humo kwa lengo la kujitangaza kugombea ubunge jimbo hilo ambalo limeongozwa kwa vipindi viwili na Mkono.
Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 baadhi ya wana-CCM akiwemo aliyekuwa mwenyekiti wa jumuia ya wazazi Abiud Maregesi walijitokeza katika kura za maoni lakini Mkono aliwashinda kwa mbali pamoja na kutumia ukabila kutafuta nafasi hiyo.


NIPASHE JUMAPILI
http://www.ippmedia.com/frontend/functions/print_article.php?l=11480
 
Bora kuna mtu ameona ufisadi wa huyu Mkono! watu wanamsifia wakati inajulikana wazi utajiri wake unatokana na nini?
 
Back
Top Bottom