Mwalimu achapwa vibao na wanafunzi baada ya kutoshiriki mgomo

Gumzo

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
211
7
MWALIMU mmoja wa jinsia ya kike aliyefahamika kwa jina moja la Kahimba wa shule ya msingi ya Kambarage iliyopo Kata ya Msamala katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma amajeruhiwa vibaya kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili na kundi linalodaijwa kuwa ni la wanafunzi wa shule hiyo ambao wanadaiwa kuwa na hasira baada ya walimu wengi wa shule hiyo kutoonekana eneo la shule kufuatia mgomo wa chama cha Walimu (CWT).

Akizungumuza na waandishi wa habari hizi Mjini Songea mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kambarage Adolfina Ndunguru alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo alidai kuwa ni udhalilishaji mkubwa kwa mwalimu kupigwa na wanafunzi.

Ndunguru alisema kuwa yeye pamoja na walimu wenzake hawakuweza kufika kwenye eneo la shule kwa kuwa wao ni walimu ambao wamekubaliana kugoma kutokana na Serikali kushindwa kutimiza ahadi yao wanayodai.

Alifafanunua kuwa inadaiwa kundi la wanafunzi lilipomuona mwalimu Kahimba kwenye eneo la shule hiyo lilimvamia na kuanza kumpiga mawe sehemu mbalimbali za mwili na baadaye alifanikiwa kukimbia.

Kwa upande wa baadhi ya walimu wa shule za msingi, Sekondari na Chuo cha Ualimu cha Songea kilichopo Manispaa ya Songea ambao wameomba majina yao yahifadhiwe walisema kuwa mgomo utaendelea mpaka Serikali itakapo ridhia kuwalipa madai yao hasa ikizingatiwa kuwa wao wanafanyakazi katika mazingira magumu.

Waandishi wa habari walifanikiwa kutembelea baadhi ya shule za Msingi na sekondari ambazo zilikuwa hazina walimu kabisa na kwamba wanafunzi wa shule hizo wakiwa wamezagaa mitaani huku wakiinung`unikia Serikali kwa kuto watendea haki walimu wao ambao alikuwa wakiwaandaa wanafunzi katika Mitihani ya kumaliza Elimu ya Msingi na sekondari.
 
Cha msingi hakuuliwa, na ujumbe umefika kwa wale wote wenye tabia za umimi, uoga na kujipendekeza.
 
Hawa watoto hawana adabu maana kugoma au kutokugoma ni haki ya mhusika. Wametenda kosa la jinai sana kiasi cha kupaswa kuchukuliwa hatua za kisheria. Mie nalaani kitendo hiki ingawa wengi watakishabikia.

Leo wamempiga mwalimu kesho watawapiga wazazi wao. Kama wana hasira kwanini wasiwaadhibu wale wanaowanyima walimu haki zao hadi wagome wakati wao wanatanua wakiongezeana ulaji ukiachia mbali kutumia mabilioni kutanua nje na wake zao?
 
Sasa si uende mahakamani? Povu la nini??
 
wamefanya vizuri,wamewarahisishia walimu maana mgomo unaelekeza wakae nyumbani,sasa yeye alienda skuli kufanyaje?????
 
Amepata alichokuwa anakitaka,hakukukuwa na dawa zaidi ya hiyo
 
wamefanya vizuri,wamewarahisishia walimu maana mgomo unaelekeza wakae nyumbani,sasa yeye alienda skuli kufanyaje?????
kwahiyo mnataka tuamini kuwa wanafunzi hawataki kuwaona walimu mashuleni?.

Dah..wabongo kwa siasa.kila issue wanawekamo na politics mwishowe issue inashughulikiwa kisiasa.matokeo yake ni watu wa kawaida ndo wanaadhirika.
 
Hiyo ni dhambi na itawaandama...Leo wameanza kupiga walimu... kesho watapiga wazazi wao.
 
kuna shule wanafunzi 6 wamesimamishwa kwa kosa la kumpiga mawe mkuu wa shule.mambo yalekua kama hayo.
 
Mgomo wa walimu ndiyo kwanza umeanza kushika kasi zaidi. Wale walimu waliokuwa wakifundisha wakati wenzao wamegoma wajiunga rasmi kwenye mgomo hivyo tunaiomba serikali/policcm wakalinde majengo na samani za shule kwa kuwa hakuna walimu isitoshe wengi wamepangisha mitaani/mjini na wale wanaoishi shuleni hawaonekani.

Naona wamekwenda kujificha kutokana na vitisho vinavyotolewa na serikali. Naona hao waliojiunga na mgomo wameelemewa na vipindi. Hebu fikiria masomo tisa kwa kila darasa kwa madarasa saba inawezekana kwa hao ambao hawajagoma? Hao wanaofundisha hawana ujuzi wa masomo hayo yote ila wanataka waonekane na wakubwa kuwa mshahara wanaolipwa unatosha.

Hivi leo serikali ikukubali kutekeleza matakwa ya walimu wao hawataongezewa? Kwa mfano wao wasipoongezewa watafanyaje? Nawaomba washiriki kwenye mgomo wasitumie mgongo wa wenzao.
 
Back
Top Bottom