Mwakyembe ageukwa

Haya yote ni majungu tu. ukitaka kupata ukweli subiri uchunguzi ufanyike.
Kwanza nikufahamishe tu kipindi kile nilikuwa na P. Chizi pale community mimi nikiwa Mwanza. Na mpinzani wetu mkubwa alikuwa PW tukafikiri nguvu ya pesa na matangazo ya bure yangetusaidia. Wapi bwana!! nafikiri ni zaidi ya hapo. Wenzangu wa sahara walikuwa kila saa hewani kuhakikisha kila mtu anafikiwa na taarifa zetu.
Unajua biashara ya usafiri wa anga sio kama wengi wetu mnavyodhania.
Unapozungumzia aviation MBA zipo 5 ungejiuliza hao wengine wapo wapi? Najua wengi waliosomeshwa na Precision huko ufaransa. Kama unakumbuka uzindizi wa ndege za PW yule balozi mfaransa alisema hilo. Hivyo huko PW zitakuwa zipo nyingi tu. nakumbuka kikao cha mwisho nikiwa community kipindi hicho mafuta hayakuwa ghali kama sasa, kile kikao tuligundua kila tuliporusha ile ndege tulitengeneza hasara ya kama milioni nane hivi. Ikaonekana ni busara kupunguza kuruka kumbe ndio tunajimaliza.
Kwa ujumla tuache ushabiki manake mtakapoletewa hati ya madai(invoice) za ndege utashangaa ni mamilioni tu.
Niwape mfano mdogo tu:
ndege ya ATC inabeba abiria 100. Kwa nauli mlizosema za 199,000 kwenda mwanza na kurudi ni (100 X 2) X 199,000 unapata kama 39,800,800.(angalizo hapo viti vyote viwe na abiria).
Mafuta kwenda na kurudi ni kama 10,000usd. kwenda na kurudi ni masaa matatu(1700 X 3) =5100usd. huduma ardhini 1000usd. ukijumlisha unapata usd 16100. hii ni sawa na (16100 x 1600) tzs 25,760,000/-
Hapo utaona tofauti ni kama milioni 14. ukitoa kodi za serikali karibia (62,000 X 200) ni sawa na milioni 12.6.
Sasa hapo hujazungumzia hoteli ya hao wahudumu, usafiri, mishahara, gharama za kutumia airport, kupaki ndege, na mengine mengi.
Kuna biashara hapo???
Tuache kukurupuka tujenge hoja kuona nini kifanyike tuwe na international airline ambayo italeta abiria hapa wa kutosha ili tufaidike kwa njia nyingine lakini sio hii ya sasa.
napita tu wandugu, ngoja niwahi mwaloni.
 
Hii ni tetesi tu, Nimeipata humu JF.

Muongo mkubwa wee.... Imagine u hear such a cooked story like this, sweeted with liars carefully formulated as if ur ab aviation expert.... of which ur not..... I am experienced flyer.... Leo Alhamis Waziri Mwakyembe kaja ATCL Terminal One kuongea na wafanyakazi woote, i was there... KAWEKA KILA KITU PUBLIC... Mpaka wafanyakazi tumeshangaaa.... Uozo ulioko ATC....
One example ... Hiii ndege iliyokodiwa....
1: hata kopi ya mkataba AG hana
2: Wizara haina Mkataba
3: ATCL walipewa waoperate 3 months free... Kumbe mkataba unaitaka ATCL wailipie hiyo ndege insurance ya miaka kadhaa huko nyuma.... Kumbe ndege inadaiwa billions of Tsh na insurance huko itokako....
Pili Katibu mkuu aliagiza ndege isiruke na wafanyakazi wa ATCL kwenda Mwanza na kurudi, eti wanasherehekea, imagine ndege inaruka free na wafanyakazi Dar - Mwanza - Dar.... UNASHEREHEKEA NINI? Chizi alikaidi amri ya Katibu mkuu....
Pili... Uteuzi wa Chizi hukufuata taratibu na kanuni za utumishi wa umma.... This does not mean or inaondoa kwamba Chizi sio aviator mzuri....
Kikao cha leo kila mmoja alishangaa na kubaki kumshangilia Mwakyembe....
So stop coming here with story ya mtu wa Stanbic....
Stanbic.... Kazi yao ni finance tu... Si ndege, period...
 
Waziri Mwakyembe ageukwa na wafanyakazi wa ATCL kwa kumsimamisha Mr. Chizi, wadai kusimamishwa kwake kwatokana na zengwe

Kuna watu cgungu mzima wamemaliza masomo na hawana kazi hao wafanyakazi ambao wanamgeuka waziri kama kweli wamekasirika waondoke wenyewe na kama wasipoondoke wafanye kazi kwa bidii na wapewe muda maalum ambapo juhudi zao zitaonekana wakishindwa kubadilika fukuza pia. Tumechoka na ubabaishaji, kila siku kukodisha ndege
 
Wale wote si wamezoea wizi na kulipwa bila kufanya kazi? Wafanyakazi mia mbili ndege mbili na kwasasa moja bado wanalipwa kama kawa, unategemea hii mianya yote ikizibwa wataacha kubwabwaja?
 
Tatizo la hii nchi kudhania kila kitu ni siasa. Hakuna utetezi kwenye suala la siasa ili wengi waseme anafaa. Inawekwa rekodi ya utendaji ya Chizi na iko clear kuwa ni mmoja wa na CEO bora afrka mashariki na ana proven records. Sasa suala la wewe unampenda Mwakyembe unatetea kila kitu alichofanya hata kama kibaya kuna siku utakuja kumpenda hata David Cameron halafu ujute kuzaliwa. Kumtoa mtu mzoefu katika uongozi wa mashirika ya ndege na kumuweka rubani kwa kuwa ana uzoefu wa kuendesha ndege ni ubazazi. Ndo maana tunachekwa na dunia nzima kwa ubwege wetu kwa kuwa kila kitu tunaweka siasa. Hebu we kilaza niambie shirika gani hapa A.Mashariki lina Boeing 737-500? Sio kukurupukia kila hoja maadam uko JF


Umeanza mada vizuri na ukaiharibu kwenye hayo maandishi mekundu. David Cameron anaingiaje kwenye mada hii. Unaruhusiwa kumpenda na kutompenda lakini usiwe na fikra tangulizi kuwa kila mtu hampendi. Na kwa siasa za nchini kwake, wananchi hawachagui mtu bali chama kwa maana wabunge na Cameron ni mmoja wa hao wabunge na pia ni kiongozi wa chama. Anachofanya ni kusimamia sera za chama chake kama kiongozi wa chama, kwa hiyo kama kuna kitu alikisema kikakukwaza, unatakiwa ujue kama hiyo ndiyo sera ya chama chake siyo yeye.
Jamani tuwe waangalifu kwenye usemaji wetu.
 
nadhani wengi wetu tumemsikia leo mh waziri akilitolea maelezo hilo..nadhani sasa inatakiwa tuwe serious kwa viongozi wanaolitia hasara taifa makusudi...tusiwaache tuu..tuwafikishe mahakamani bila ubaguzi......
 
Hivi kwa nini kuna guest wengi kuliko registered member? N a kwa nini inapokuja post mpya guest huwa wa kwanza kuibrowse kuliko registered member? TAFAKARI , CHUKUA HATUA!
There are currently 69 users browsing this thread. (29 members and 106 guests)
 
uzalendo ndani ya nchi hii unarudi sasa!mwakyembe chapa kazi,kumbuka siku zote mkweli na mpenda haki huwa na maadui wengi!mkabidhi mungu kazi yako atakusimamia na kukuongoza!
 
uzalendo ndani ya nchi hii unarudi sasa!mwakyembe chapa kazi,kumbuka siku zote mkweli na mpenda haki huwa na maadui wengi!mkabidhi mungu kazi yako atakusimamia na kukuongoza!

Mchapa kazi ndani ya serikali ya CCM, unaota nini, au huijui CCM wewe
 
Back
Top Bottom