Mwaka 2023 ulikuwa wenye joto zaidi katika historia

Wild Flower

Member
Jul 20, 2023
80
96
Kulingana na data kutoka Shirika ya Hali ya Hewa ya Copernicus, wastani wa joto la Dunia mwaka jana 2023 lilikuwa nyuzi 1.48 Celsius joto zaidi kuliko miaka iliyotangulia.

Wataalam watahadharisha mataifa kufanya mabadiliko ya haraka kutoka kwenye nishati chafu la sivyo joto litakuwa kali zaidi mwaka huu 2024 kuanzia mwisho wa Januari-Februari mwanzoni, ambapo joto linatarajiwa kuzidi nyuzi 1.5 Sentigredi.

Mabadiliko ya hali ya hewa yalisababisha joto kali, mlipuko wa volkano, ukame na moto wa misitu kote duniani, hasa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa yaliyosababishwa na binadamu na hali ya hewa ya El Niño inayosababisha joto la juu la bahari katika Bahari ya Pasifiki kando ya Amerika ya Kati. Haya yote ni ushahidi wa mwaka 2023 kuwa mwaka wenye joto zaidi.
 
Back
Top Bottom