Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,174
Kwenye Mkutano Mkuu wa CCM wa mwaka 1995 wa kumpitisha Mkapa kugombea uraisi, Nyerere alisema haya ambayo leo ninaona ni kero kwangu sijui kwenu na wala sikubaliani naye kwenye hilo hata kidogo.
Alisemaje? Hapa ninamnukuu:-
Kiongozi anaweza kutoka popote pale lakini kiongozi bora wa kutumainiwa na taifa atatoka ndani ya CCM.
Mimi sikubaliani naye kwa sababu nimemwona JK jinsi ambavyo yupo beneti na mafisadi na anakula nao sahani moja na ndiyo maana na hata Bw. Kifimbo hapo nionavyo alichemsha.
Lakini Nyerere ana busara sana kwenye hotuba hiyo hiyo alinena yafuatayo ambayo yanagusa sasa kudondoka kwa JK na timu yake ya watafunaji wa fedha za umma. Na ninamnukuu:-
Watanzania wakikosa uongozi bora ndani ya CCM watautafuta nje ya CCM..
Si sasa yametimia .GO DR. SLAA...GO TO STATE HOUSE