Mwaka 1995 Nyerere alitabiri kuanguka kwa CCM!

JK, & SHIMBO. Nchi Hii sio ya kwenu. Wala nyie sio Miungu wa Tanzania kwanza hamna ubavu wa kumwaga damu yetu kunguru wakubwa nyie, Mtatoka kwa sanduku la Kura. Jeuri ya kupambana na Watanzania 40,000,000 Hmna. Mnaturingishia Amani ya Kinafki, ni sisi wenyewe ambao tumeamua kutulia kwa amani ila ninyi hakuna chochote ambacho mmeleta zaidi ya madudu. Kwanza mna nini cha ajabu ambacho hapa duniani hatujawai kukiona labda tuwaogope. Kwa Taarifa yenu na familia zenu Ikifika 31/10 Hamtaamini macho na masikio yenu.


hapo kwenye red, ya mwaka gani mkuu?
 
'Wanatuhumiwa wasinyooshewe vidole, CCM ifanye mabadiliko' Send to a friend Saturday, 30 April 2011 09:46

Fidelis Butahe
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali mstaafu, Jaji Mark Bomani, amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinapaswa kufanya mabadiliko makubwa zaidi na kwamba dhana ya kujivua gamba si kigezo cha kukijenga chama hicho.

Alisema chama hicho, kinapaswa kuacha kuwanyooshea vidole, baadhi ya wanachama wanaotuhumiwa kwa ufisadi pekee na badala yake, kifanye mabadiliko makubwa zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kutoa msaada wa Sh5milioni kwa Jeshi la Polisi (Kitengo cha mbwa na farasi), Jaji Bomani alisema CCM inapaswa kutazama mfumo wake na maadili kwa viongozi wa ngazi zote.

Mwanasheria huyo nguli nchini, alisema chama hicho pia kinatakiwa kutazama namna viongozi wake wanavyopatikana."Kinachotakiwa ni namna viongozi wa CCM wanavyopatikana, bila hivyo, kila mtu anaweza kuibuka na kusema fulani hafai, unapotaka viongozi makini lazima uwe na utaratibu mzuri wa kuwapata,"alisema Bomani.

"Hili lilitokea CCM halitoshi, linahitajika zoezi kubwa zaidi ya hilo tena kuanzia ngazi ya chini kabisa," alisisitiza.
Jaji Bomani alisema mfumo imara wa uongozi katika chama chochote cha siasa, ndio msingi wa kukiimarisha chama hicho.

"Nasema hivi kwa sababu utakuta mtu anatoka chama fulani na kuhamia kingine halafu baada ya siku chache anagombea udiwani, hii sio njia nzuri," alisema jaji huyo mstaafu.Alisema chama cha siasa, lazima kiwe na mfumo imara wenye masharti kuhusu upatikanaji wa wanachama na wagombea wa nafasi za uongozi.

Alisema njia hiyo ndio suluhisho la kuwa na viongozi waadilifu watakaokifanya chama, kuwa imara.Jaji Bomani alifika mbali zaidi na kueleza kuwa suala la Rais wa Tanzania kuwa na kofia mbili za uongozi kama Rais wa nchi na Mwenyekiti wa chama chake nalo linapaswa kutazamwa upya kwa kuzingatia majukumu mengi anayokuwa na kiongozi huyo.

"Hizi nchi zinazoendelea zina mambo mengi sana ya kufanya, ukiwa rais unakuwa mtendaji na ikumbukwe kuwa rais anakuwa na kazi nyingi za kufanya. Sasa anapokuwa rais wakati huo huo ni mwenyekiti wa chama, hilo nalo linapaswa kutazamwa upya," alisema.

Alisema katika mchakato wa kuwa na katiba mpya si vibaya kama suala hilo nalo likaangaliwa kwa mapana."Hili ni suala linalozungumzika na watu wasilionee haya hata kidogo,"alisisitiza.
 
CCM na mizaha ya ‘Ikengya na Beyalula’
ban.blank.jpg

Abdul Juma

amka2.gif
WAHAYA wana kijitabu kidogo chenye jina la watu wawili, Ikengya na Beyalula, bila shaka kwa wale waliobahatika kukisoma, watakubaliana na mimi kwa hili ninalotaka kulisema leo katika mada yangu.
Kitabu hicho kimetungwa na kuandikwa kwa lugha yao. Kwa wale ambao hawajapata bahati ya kukisoma kitabu hicho ama walikiona lakini wakashindwa kukisoma kutokana na kutoifahamu lugha ya Kihaya, basi nitawasimulia kwa kifupi.
Kitabu hicho japo kiliandikwa kikiwalenga wenzetu Wahaya lakini kina mafundisho ambayo nasi tunapaswa kuyachukua. Humo Beyalula hafurahishwi na tabia, matendo ya mwenzake Ikengya hivyo anajaribu kumhoji maswali ya msingi ya kwanini iwe hivyo, ila anaambulia majibu ya kimasihara yasiyokidhi.
Ikengya wakati wote alijibu kwa mzaha na kejeli ili kumkatisha tamaa Beyalula, ingawa mwisho wa siku aliishia kupata matatizo makubwa na hapo ndipo alipokumbuka busara ya maswali ya rafiki yake.
Hata mimi leo nilitaka kuwafananisha viongozi wetu wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vihoja vya Ikengya kwa Beyalula. Hawa wana macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii na wana akili lakini hawana busara ya kufikiri.
Pengine labda ili CCM na serikali yao wapate kutusikia na kutuelewa kuwa tumechoka, yafaa kuwakumbushe tena kauli ya Azimio la Arusha, watambue kuwa tumewachoka kwa usanii wao. Kauli yenyewe ni hii hapa:
“Tumeonewa kiasi cha kutosha, tumenyonywa kiasi cha kutosha. Unyonge wetu ndiyo ulitufanya tuonewe, tunyonywe na kupuuzwa. Sasa tunataka mapinduzi; mapinduzi kuondoa unyonge ili tusionewe tena, tusinyonywe tena wala tusipuuzwe tena”.
Serikali ya sasa ambayo ni zao la CCM, viongozi wake wanadhani kuwa Watanzania wanaishi kwa matumaini ya hadithi za ukasuku zisizokuwa na utekelezaji kwa miaka nenda rudi. Hawafikirii kuwa watu wa leo wanataka kushuhudia vitendo ndipo waamini.
Wakati tunapata uhuru mwaka 1961, hayati Mwalimu Julius Nyerere na viongozi wenzake, walijiwekea dira yao kama mkakati waliopaswa kuhakikisha wanautekeleza. Vipaumbele vyao vilikuwa ni kupambana na maadui ‘Ujinga, Maradhi na Umaskini’.
Baada ya kusonga mbele kidogo wakajitanua tena kuwa ili tuendelee tunahitaji ‘Siasa safi, Watu, Ardhi na Uongozi bora’. Serikali ya Awamu ya Kwanza hadi inaondoka madarakani walikuwa wakijipima katika mambo hayo kuona je, walifanikiwa kiasi gani?
Zikafuata awamu zingine yaani ya pili na tatu ambazo kwa kiasi Fulani zilikuwa na dira zao japokuwa zote zilianguka kwa kushindwa vibaya katika kipengele cha uongozi bora, maana ufisadi wa mali za umma uliwatawala na hivyo wakajigawia rasilimali zetu.
Awamu ya Nne licha ya kurithi maradhi yale yale ya ufisadi na kuyaongezea kasi bado imekosa dira wala vipeumbele badala yake inajaribu kugusa kila kitu, hatua inayofanya mambo mengi kushindikana.
Kipindi cha kwanza cha Rais Jakaya Kikwete, walikosa dira na kipaumbele badala yake wakabeba vibwagizo vya kaulimbiu ya Kasi Mpya, Nguvu Mpya na Ari Mpya.
Tulipoingia kipindi chake cha pili nikadhani atakuwa amejifunza chochote huku nyuma, kuwa anahitaji dira na kipaumbele lakini sivyo alivyofanya.
Rais Kikwete alichofanya ni kuboresha kibwagizo chake kikawa Ari Zaidi, Nguvu Zaidi na Kasi Zaidi kisha akataja mambo 13 eti ndivyo vipaumbele vyake. Kwa wanaoweza kuvisoma kwa makini vipaumbele hivyo, hata tukimpa miaka mingine 10 zaidi hawezi kuvitekeleza.
Hii ndiyo mizaha niliyokuwa namaanisha hapo juu kwa kutumia kitabu cha Ikengya na Beyalula. Kwamba CCM na serikali yake wamepoteza mwelekeo, wanapaswa kukiri kushindwa na kujiweka kando, badala ya kutoa majibu mepesi ya masihala na kejeli kwenye maswali magumu yanayogusa maisha ya watu.
Miaka 50 ya Uhuru ni aibu kushindwa kumtokomeza adui umaskini badala yake tunamfuga ili aongezeke zaidi. Ni fedheha na matusi kwa waasisi wa taifa hili kuwa tunakuwa maskini wakati tunaogelea kwenye utajiri usioelezeka wa kila aina ya rasilimali.
Miaka 50 baada ya Uhuru, tumeshindwa kuboresha sekta ya Afya, viongozi wetu wamezifanya hospitali za hapa nchini kuwa za walalahoi wakaparangane kwa kugawana panado na asprini. Wao wamehamia kutibiwa India, Afrika Kusini na Ulaya.
Ujio na tiba ya miujiza ya Mchungaji mstaafu Ambilikile Mwasapila kule Samunge - Loliondo na wajanja wengine wanaoendelea kujitokeza wakitumia mgongo wake, umetoa picha kamili ya hali mbaya ya afya tuliyonayo wote kuanzia viongozi wetu.
Kama tungewaelewa wakina Nyerere, bila shaka kwa miaka 50 yote, viongozi wetu wangehakikisha serikali inakuwa na hospitali makini zenye dawa na kila aina ya huduma ya afya.
Kamwe kasi hii ya kukimbila Loliondo isingekuwa namna hii kama hospitali zetu zingekuwa zinaaminika.
Miaka 50 ya uhuru, CCM na serikali yake wanadhani kupambana na adui ujinga ni kuwa na shule nyingi zisizo na vitendea kazi wala walimu ilimradi tu watoto wetu wakusanyike na kupigia michapo.
Kwenye kisa hiki cha CCM kuwa kama Ikengya na Beyalula kwa kupoteza muda mwingi kujitapa kuwa wamevua gamba wakati maisha ya watu ni magumu, bei za vyakula na baidhaa muhimu hazishikiki, kweli maendeleo yetu yatapatika chini ya chama hiki?
Serikali ya sasa ina ufisadi wa kutisha, na kwa kuwa inatokana na zao la CCM bila shaka chama hicho kinapaswa kujipima kwa busara kuwa tatizo lao halipo kwa watu watatu kama tunavyoimbiwa huku nje.
Kujivua gamba ni kututajia wamiliki wa Kagoda, Meremeta, Kiwira, Mwananchi Gold Mine, Deep Green Finance, wezi wa EPA waliobembelezwa warejeshe fedha walizoiba na uchafu mwingine wote kisha washitakiwe haraka iwezekanavyo.
Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, ilishindwa kuwawajibisha vigogo wa chama na serikali waliotuletea kampuni ya mfukoni ya kufua na kusambaza umeme ya Richmond baadaye Dowans halafu eti watu wale wale wanatanua vifua na kufungua vinywa vyao bila aibu kuwa wamejivua gamba na wanajisafisha.
Beyalula alimuuliza Ikengya; mbona unakula kiporo cha watoto? Jibu lake lilikuwa kwamba alikuwa anajaribisha kuona kama meno yalilala mdomoni.
CCM nao wakiulizwa kwanini serikali yenu imeshindwa kupambana na ufisadi, Rais Kikwete alitujibu eti kuwakamata wote na kuwashtaki, nchi itayumba.
Kama watu tunao, ardhi ipo tena ya kutosha hadi wageni wamejitwalia wanafanya watakavyo, siasa ipo ingawa siyo safi kiasi hicho kwani mojawapo ya sababu ya kupwaya kwa viongozi wetu ni kutokana na kupata uongozi katika njia za giza.
Hapa ndipo tunapoteza hitaji la uongozi bora. Je, tutaendelea kama wenzetu?
Kwa wale wadadisi wa kujisomea historia ya dunia, sina shaka wamemsoma Lee Kuan Yew. Huyu alizaliwa Septemba 16, 1923 nchini Singapore. Amekuwa Waziri Mkuu wa kwanza kuiongoza nchi yake, huyu ni waziri mkuu aliyeweka rekodi ya dunia kwa kutawala muda mrefu.
Alikiongoza chama chake cha People’s Action Party (PAP) kikashinda chaguzi mara nane toka mwaka 1959 hadi 1990 alipoachia ngazi.
Kiongozi huyu alijiwekea sifa moja kubwa ya kuiondoa nchi yake kiuchumi kutoka dunia ya tatu hadi dunia ya kwanza. Kwa hiyo Singapore iliyokuwa nafasi kama Tanzania mwaka 1959, leo ni moja ya taifa tajiri.
Ukisoma zaidi tunu na mbinu alizotumia Lee Kuan Yew kuifikisha nchi yake katika dunia ya kwanza, utabaini kuwa alijitenga na ushikaji, uswahiba, kujuana, mtandao na kila aiana ya ukaribu na marafiki zake hadi wengine kulazimika kuwatia gerezani. Je, sisi tatizo la kutokuendelea kwetu lipo wapi? Tafakari!



h.sep3.gif

Niachie ujumbe: 0788452350 na mpyafikra@yahoo.com
 
Kaptula ya CCM imechanika makalioni!
ban.wazo.jpg

Juvenalis Ngowi

amka2.gif
KIASI cha kama miaka miwili hivi iliyopita niliwahi kuandika makala nikasema kwamba kaptula la Chama Cha Mapinduzi (CCM) limetoboka makalioni. Kama kawaida nilipata ujumbe kutoka kwa wasomaji kupitia simu ya mkononi, kila mmoja akiwa na maoni yake. Wengi walikubaliana nami kwamba sasa ni muda wa CCM kutafuta vazi jipya ijisitiri. Wachache walitofautiana nami. Hiyo ni sehemu ya mjadala.
Baada ya kuona yanayoendelea ndani ya chama hiki kilichozeeka nikakumbuka makala yangu hiyo na sasa naweza kusema kwa hakika kwamba kaptula la CCM limechanika makalioni na dawa pekee ni kununua kaptula jipya ijisitiri.
Kuliko kununua nguo mpya tunaona wakizidi kujifunua wenyewe. Wanasema wanavua gamba. Uvuaji gamba huo umetuonyesha matobo mengi kwenye kaptula ambayo hapo awali huenda hatukuwa na hakika au hatukuyajua kabisa.
Hawana ubishi kuhusu uwepo wa uchafu na matobo kwenye vazi lao. Mjadala ni nani mchafu? Katibu Mkuu wa CCM Willison Mkama anatuambia kwamba wao hawakutajana majina. Bali Nape Nnauye anasema majina yalitajwa ila Mkama ndiye hakuwepo kwenye kikao!
Hata katika mjadala huo ambao wanatofautiana wao kwa wao bado kuna jambo moja. Wanakiri wote kuwa kuna uchafu. Tofauti yao ni ikiwa walitajwa wachafu ni akina nani au la. Lakini kwetu sisi hoja ni kwamba uchafu ukikaa mahali huchafua sehemu hiyo. Kama kuna wachafu ndani ya CCM basi CCM nayo imechafuka.
Kwa mara ya kwanza wametuthibitishia kwamba kuna ufisadi kwenye chama. Ila hoja ya walio wengi ni kwamba haiwezekani mafisadi wakawa watu watatu tu wanaotajwa kwenye mikutano ya Nape. (Edward Lowassa, Andrew Chenge na Rosatam Aziz). Kuwataja watu hawa inawezekana ni kutuonyesha tobo kwenye kaptula ya CCM, tutaona nini tukichungulia kwenye tobo? Kinachofanyika sio kujisitiri bali ili kujisitiri CCM inapaswa ilete matumaini ya kesho yenye nafuu.
Kuna watu wanaosema wapinzani hawana ajenda mpya zaidi ya ufisadi. Sitaki kuingia kwenye mjadala wa uongo au ukweli wa hili. Ila katika hili la kujivua gamba, tunaweza nasi kuhoji ukiacha hili la ufisadi wamekuja na jipya lipi? Donda la ufisadi ni kali na linaumiza wengi bali sio tatizo pekee.
Je, wanataka kutuambia kwamba wakishawatimu wabaya wao, sasa tutaanza kushuhudia maisha bora kwa kila Mtanzania? Sikushangaa niliposoma makala kwamba CCM sasa wanacheza muziki wa chadema. Hii ni kutokana na ukweli kwamba vita hii ya ufisadi haikuasisiwa na CCM.
CCM wameidandia wakidhani wanaweza kuficha matobo ili wajisetiri lakini kwa bahati mbaya ndio wamezidi kujionyesha walivyo. Kwamba kuna CCM nyingi ndani ya CCM moja. Wachambuzi waliposema kwamba CCM si moja, Yusuf Makamba, aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CCM enzi zile akiwa na nafasi hiyo alibisha na kusema ni uongo. Lakini haya tunayoyashuhudia sasa ndicho tulichokuwa tukikisema wakati ule.
Tatizo ni kwamba wanazungumza lugha ile tuliyozungumza ila kwa namna tofauti. Wanakubali kuna tatizo lakini hawataki kuangalia tatizo lilipoanzia. Kama wanataka kujivisha nguo watuambie walikuwa wapi wakati hao mapacha watatu wakifanya wanayotuhumiwa? Serikali ilikuwa likizo? Tuhuma zao zinaanzia lini? Haya ni maswali muhimu kujibiwa ili tujue kwamba kama ni uchafu tumeutoa wote.
Kwa Watanzania wengi unapozungumzia kinachodaiwa ufisadi wa mapacha hawa watatu, mawazo yetu yanapelekwa moja kwa moja kwenye suala la rada, Richmond na mambo ya EPA kabla ya kufikiria kingine chochote. Je huu ndio ukweli? Kama huu ni ukweli ilifikiaje hapo? Chama, serikali vilikuwa wapi? Mwenyekiti wake wakati huo alikuwa nani na alifanya nini?
Hebu fikiria hoja ya rada. Ililalamikiwa kwa kiwango kikubwa hadi katika bunge la Uingereza. Lakini ilinunuliwa. Hivi katika akili ya kawaida kabisa tunaweza kuaminishwa kwamba ni mmoja au wote watatu walifanya uamuzi huo wenye makengeza kununua rada ambayo hata nje ya nchi walishaona tunapigwa changa la macho? Maamuzi ya ununuzi wa rada kwa mfano, yaliwahi kupingwa na kikao chochote cha chama? Kama ndio ni kikao kipi na ilikuwa lini?
Kwa nini mambo haya yanazungumzwa sasa? Maswali haya haya unaweza kujiuliza kwenye mambo ya EPA na Richmond. Kama ni hawa watatu waliofanya mambo hayo chama kilikuwa wapi?
Sasa kwa CCM kukubali kwamba kuna uchafu ulifanyika na wakashindwa au wakakataa kuzuia hilo ni tobo jingine kwenye vazi lao. Jambo moaj la msingi ni kwamba ukiacha Riohmond, madudu mengine ya ufisadi yanayolalamikiwa kwa nguvu hivi sasa yalianza katika utawala wa awamu ya tatu.

Hivi chama kimeangalia historia na kujua nani aliwezesha kipi kifanyike? Lakini je wamejiuliza nani walifaidi matunda ya madudu haya? Sitaki kurudi nyuma hadi wakati wa azimio la Zanzibar la 1992. Tukirudi huko nani atakuwa na ujasiri wa kujidai kusafisha chama bila yeye kujikuta akiwa sehemu ya uchafu wa kusafishwa?
Salama yetu ni kizazi kipya kisichokuwa na mawaa. Kama CCM itaendelea kushika madaraka ya nchi hii, viongozi watarajiwa ni hawa waliko kwenye jumuiya ya vijana wa CCM (UV-CCM). Kwa malumbano tuliyoyaona hivi majuzi baina yao wao kwa wao unaweza kweli kuona dalili za viongozi bora? Maana hata wao vazi lao lina matobo.
Lakini tukiamua kuamini kwamba sasa CCM wanavua vazi lao lenye matobo na kuvaa jipya, vipi serikali? Maana chama kileteleza, je na serikali nayo? Serikali haina magamba ya kujivua? Ni ngumu kufikiria namna ambavyo mambo haya yangetekelezeka bila utendaji wa moja kwa moja wa viongozi wa serikali.
Pengine hapa ndipo pa kutazama kwa uangalifu mkubwa wakati wa kuandika katiba mpya. Kinga zinazofikia mahali pa kumlinda anayetuhumiwa kijinufaisha mwenyewe bado zinapaswa kuwepo katika katiba? Sheria zetu zinaruhusu serikali nayo kujivua gamba?
Tunapozungumza chama kinachosema kinajibadilisha huku serikali yake ikiwa ni ile ile ni sawa na timu yenye wachezaji wabovu halafu unabadili kocha! Haya mambo yanapaswa kufanyika kwa pamoja.
Sitashangaa kwamba mwanzo na mwisho wa yote haya ikawa ni hotuba za majukwaani kwamba wamevua gamba badala ya kutuonyesha mbadala wa gamba ni upi. Kwa kuangalia haya yote nakubaliana na makala yangu mwenye niliyoiandika zamani kwamba kaptula la CCM limetoboka makalioni. Wanunue jipya ili kujisitiri.



h.sep3.gif

kevinmakyao@hotmail.com
0784 265072
 
Tumechoka kuchakachuliwa
ban.maswali.jpg

Ansbert Ngurumo

amka2.gif
NIMECHUNGUZA na kugundua kwamba serikali bado inafanya njama kuhujumu mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya. Haitaki kujifunza. Inang'ang'ania uchakachuaji wa mchakato.
Imejiingiza katika harakati chafu za kutumia vituo kadhaa vya televisheni kutetea udhaifu wa muswada wa mabadiliko ya katiba ambao umepigiwa kelele, umepingwa na hatimaye kunyofolewa bungeni.
Serikali ina hasira. Na sasa inafanya njama za kulipiza kisasi kwa mbwembwe.
Kabla ya kukataliwa na wananchi, muswada huo uliokuwa umewasilishwa katika Mkutano wa Tatu wa Bunge Dodoma kwa Hati ya Dharura, uligundulika kuwa na kasoro nyingi za msingi. Wananchi wakaukataa, serikali ikalazimika kuuondoa ili iufanyie marekebisho na kuuwasilisha tena bungeni kwenye kikao cha Bunge cha Juni mwaka huu.
Lakini sasa serikali hiyo hiyo imejiingiza katika kazi chafu ya kumwaga na kusambaza kile kile kilichokataliwa na wananchi, kwa nia ya kuwaghilibu, kama njia ya kupuuza mapendekezo ya msingi ya wananchi.
Kama ambavyo ilitumia vyombo hivyo vya habari kuhadaa wananchi katika mgogoro wa uchaguzi wa Meya wa Arusha kati ya CHADEMA na CCM, ndivyo inavyofanya sasa kuhusu muswada huu, baada ya kuaibishwa bungeni.
Kuna vielelezo viwili vya haraka haraka. Cha kwanza ni kauli ya Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Sinde Warioba, aliyenukuliwa na gazeti moja akisema: "hakukuwa na haja ya kupeleka Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Marekebisho ya Katiba wa mwaka 2011 kwa wananchi kwa kuwa wabunge ni wawakilishi wao."
Hii ni kauli ya kushangaza na isiyotarajiwa kutoka kwa mwanasheria wa viwango vyake, maana mzee Warioba aliongeza kuwa wanaokataa muswada huu hawalitakii mema taifa hili.
Nataka kushawishika kwamba alikuwa hajausoma muswada wenyewe. Kama aliusoma, halafu akaibuka na kauli hii, naomba nikiri kwamba mzee Warioba amezeeka, amechoka. Aachwe apumzike!
Alisema: "Hivi naomba mjihoji kwanza, hasa nyie waandishi wa habari, ni mara ya kwanza kuwa na ‘bill (muswada)' nchini? Kwa nini huu uwe mgumu, kwa nini wananchi ndio waamue wakati Bunge lipo kwa ajili yao? Wabunge ni wawakilishi wa wananchi, ni muswada gani wa Katiba ulipelekwa kwa wananchi hivi?"
Mzee Warioba amegeuka mateka wa historia. Hataki kuitumia kujifunza mbinu mpya. Anataka kuendelee kunakili makosa ya kihistoria yaliyotebdwa huko nyuma. Hajasiki vema kauli ya wananchi. Wamesema "hatutaki." Bahati nzuri, serikali imesikia, na imeng'amua hilo. Ndiyo maana imeuondoa muswada bungeni, ingawa kwa shingo upande.

"Shingo upande" hiyo ndiyo inamfanya Waziri wa Sheria Celina Kombani azungukie vituo kadhaa vya televisheni kila asubuhi, kuomba vipindi vya kusemea yale ambayo wananchi wameshamwambia hawayataki.
Na hiki ndicho kielelezo cha pili. Kombani anang'ang'ania kauli ya ile ile ya muswada uliokataliwa.
Baada ya kumsikiliza zaidi ya mara mbili, nimehisi kwamba kitu pekee anachojaribu kutetea ni mamlaka ya rais katika kusimamia mchakato huo kwa jinsi walivyoona wao. Na kwa bahati mbaya, Kombani anang'ang'ania kujadili hoja ya rais kuunda tume ya kukusanya maoni ya wananchi.
Kinachowashinda Warioba na Kombani ni uelewa wa kawaida kwamba wananchi wanakerwa na usimamizi na uendeshaji wa mchakato.
Wananchi hawasemi rais asihusike kuunda tume, bali asipewe kauli ya mwisho. Wanataka kauli ya mwisho iwe ya wananchi wenyewe kupitia kura ya maoni.
Lakini kabla lhawajfika kwenye hatua hiyo, wanataka waridhike kwamba mchakato utakaowafikisha huko unazingatia maoni na matakwa yao. Wanataka mchakato unaojali hofu zao na matumaini yao.
Wanapinga kuunda katiba mpya kwa staili ile ile iliyounda katiba za zamani zinazolalamikiwa. Hawaombi serikali iwahusishe, bali wanadai haki yao ya kuandika katiba mpya inayotokana na utashi wao. Warioba na Kombani hawalielewi hili?
Wananchi wanataka mamlaka ya rais kuunda tume yasitokane na hiari yake binafsi, kama ambavyo muswada huu unadokeza. Wanataka muswada uzae sheria ya kumlazimisha na kumwekea misingi na vigezo vya kuunda tume hiyo.
Kwa jinsi kifungu cha tano cha sehemu ya pili ya muswada, kinavyosema, rais halazimiki kushauriana na mtu yeyote anapounda tume hiyo.
Walichotuletea kina Kombani kwenye muswada ni kile kile cha huko tulikotoka. Na huko tulikotoka, anakosifia Mzee Warioba, ndiko kumezaa katiba za mwaka 1961, 1962, 1964, 1965 na 1977. hizi ndizo tunazolalamikia, na huko siko tunakotaka kwenda. Warioba na Kombani hawalitambui hilo?
Nakubalina na hoja sahihi za Celina Kombani katika kujadili kifungu cha 9(2) kinachozungumzia tunu za kitaifa ambazo tunapaswa kuzienzi.
Zilizotajwa ni Muungano wa Tanganyika na Zanzibar; nguzo tatu uza dola (utendaji, mahakama na bunge); urais; Serikali ya Mapinduzi Zanzibar; Umoja wa kitaifa; uchaguzi wa kidemokraisa wa mara kwa mara; kukuza utu na heshima ya mwanadamu, na utawala wa sheria; serikali kutoshikamana na dini; na uhuru wa mahakama.
Wapo waliotafsiri kwamba kifungu hicho kinatuzuia kuyajadili masuala hayo. Lakini baadhi ya wataalamu wa sheria – na sasa nimemsikia Kombali akizungumza lugha kama yao – wanasema mambo haya yanajadilika, isipokuwa wanaoyajadili hawaruhusiwi kuyavunja.
Hapo napo panahojika. Maana sheria yenyewe ya kuandikakatiba ndo inaandaliwa. Bado hatujakubaliana mambo hayo ya msingi. Serikali imejuaje kwamba hayo ndiyo tutakayotaka kuenzi,na hakuna mengine? Na imejuaje kwamba tutaafikiana na serikali juu ya mfumo wa kuyaenzi?
Naamini sehemu ya utata huu wa tafsiri imetokana na lugha iliyotumika kuandaa muswada - Kiingereza. Hakieleweki kwa kila mtu kwa kiwango kile kile. Tukumbuke pia imetumika lugha ya kisheria ambayo haieleweki kwa kila mtu.
Vile vile, muundo wa maneno yalitoyumika haukuondoa mwanya wa utata wa tafsiri.
Lakini serikali ilikurupuka kuweka hitimisho kabla ya mchakato na mjadala kuanza.
Serikali iache watu wajadili hoja kutoka pande zote. Kwa mfano, kama yupo anayedhani kwamba Muungano si muhimu, ajenge hoja. Kama atakuwa na hoja za kutushawishi sisi tunaotaka Muungano usivunjwe, tutamsikiliza. Kama hana hoja ya kutushawishi tutampuuza.
Lakini kuwazuia watu kujadili masuala nyeti kama haya, ni hatua ya kupandikiza mbegu mbaya ya ulalamishi na uchonganishi, ambayo inaweza kuhatarisha amani ya nchi huko mbele ya safari. Mchakato huu una lengo kuu moja: kuwawezesha wananchi kuandika katiba yao.
Tume itakayoundwa itaratibu maoni ya wananchi – mazuri na mabaya. Itapima na kufanya uchambuzi baada ya wananchi kutoa maoni yao. Itayafanyia uchambuzi na kuyachuja kwa vipaumbele.
Tume ndiyo inapaswa kuchambua, lakini muswada huu, kwenye kifungu cha 16(3), unampa rais mamlaka ya kupokea ripoti ya tume na kuamua lipi liingizwe na lipi likataliwe.
Kwa maana hiyo, rais anapewa mamlaka ya kukataa, kupindisha au kubadilisha maoni ya wananchi. Rais amepewa uhuru wa kuamua lipi liende, lipi libaki. Hiki ndicho wananchi wanakataa. Warioba na Kombani wanashindwa kuelewa hata hili?
Kifungu cha 13 (2) kinampa tena rais mamlaka ya kuteua katibu wa tume. Maana yake ni kwamba katibu huyo atawajibika kwa rais aliyemtuma. Huko nyuma, tumejaribu mfumo huu katika tume zote zilizowahi kuwapo, lakini tumeishia kunung'unika.
Tusisahau kwamba mamlaka haya ya rais, na uteuzi wa aina hii, ndiyo sababu ya serikali kugoma kurekebisha au kufuta sheria mbaya zaidi ya 40 zilizoainishwa kwenye Tume ya Nyalali miaka 19 iliyopita. Badala yake, hata sasa zinatungwa nyingine mbaya kama zile, au zaidi ya zile.
Uteuzi huo na mamlaka hayo ndiyo sababu za mapendekezo ya Tume ya warioba kushindwa kutekelezwa. Mzee Warioba mwenyewe, mara kadhaa, aliilalamikia serikali ya Rais Mkapa kwa kupuuza ushauri wa Tume yake.
Mtindo huo ndiyo uliosababisha yalimpata Jaji Robert Kisanga katika Tume ya White Paper. Wananchi wamejifunza kutokana na makosa hayo ya kihistoria. Hawataki turejee huko, maana tume zinazowajibika kwa rais hazizai matunda yaliyotarajiwa.
Wanakataa kujifunga minyororo kwa kutegemea maoni, uzoefu na hekima binafsi ya rais. Wananchi waliokwishang'atwa na ‘nyoka' huko nyuma, wana haki ya kuogopa hata mjusi. Warioba na Kombani hawalioni hilo?
Kuna kituko kingine. Kifungu cha 21(1) kinampa rais mamlaka ya kuteua wajumbe wa Bunge la Katiba. Hii ni dhambi ambayo tumekuwa tunaitenda huko nyuma. Wananchi wanasema hatupaswi kurudi huko. Wanataka Bunge la katiba lichaguliwe na wananchi wote kwa kura, kama tunavyofanya wakati wa uchaguzi mkuu. Na liwe kwa ajili hiyo tu. Likishamaliza kazi yake linakufa!
Kama serikali inaona ni muhimu kupiga kura kwenye uchaguzi wa madiwani, wabunge na rais wanaodumu kwa miaka mitano tu, kwanini inashindwa kutambua kwamba tuna haki kubwa zaidi kupiga kura kuchagua wajumbe wa Bunge la Katiba, ambayo ni mwongozo na nguzo ya taifa?
Kwanini Warioba na Kombani wanaendekeza mazoea ya huko tulikotoka, ambako rais aliligeuza bunge lililokuwapo kuwa Bunge la katiba? Mchakato wa wakati ule, kama ulivyokuwa wa Zanzibar mwaka jana, ni mchakato-dola, unaotekeleza matakwa ya watawala. Kwanini Warioba na Kombani hawatambui kwamba wananchi wanataka mchakato-raia wa kupata katiba mpya?
Ajabu nyigine. Katika sehemu ya nne, kifungu 28(2) kinazuia wadau wa mchakato kufanya kampeni ya kuhamasisha wananchi kupiga kura ya maoni ya kuunga mkono au kukataa muswada.
Badala yake, muswada unataka tume ya uchaguzi ndiyo ifanye kampeni hiyo. Sasa kama tume inayosimamia uchaguzi, itafanyaje kampeni huku yenyewe ndiyo mwamuzi? Warioba na Kombani hawalioni hilo?
Niliwahi kudokeza huko nyuma. Nitarudia hapa. Kiinimacho kilichofanyika Zanzibar mwaka jana kilishindwa kuzaa katiba ya wananchi. Ya Zanzibar, kwa mtindo ulioileta, ni katiba ya watawala.
Mchakato uliotumika Zanzibar ni sawa na huu unaopendekezwa na serikali sasa katika katiba ya Muungano. Ndiyo maana hata kura ya maoni ilipopigwa Zanzibar, wanasiasa na wadau wengine walizuiwa kufanya kampeni, bali rais aliye madarakani alihamasisha watu wapige kura ya "ndiyo."
Kwa hiyo, ilikuwa kampeni ya upande mmoja. Watawala walikuwa wanahamasisha wananchi wapitishe "kitu cha wakubwa." Matokeo ya mchakato wa aina hii hauwezi kuzaa katiba ya wananchi.

Na hiki ndicho wananchi wanachokataa. Wanataka katiba yao, iliyoandaliwa katika mchakato usiofanana na wowote katika ile tuliyowahi kuwa nayo. Warioba na Kombani hawalielewi hili?
Nchini Kenya, wananchi, kwa mfano, wananchi walidai katiba mpya tangu mwaka 1964 lakini, kama ilivyo kwetu, hawakupitia mchakato rahisi, na iliwachukua muda mrefu.
Harakati zenye mashiko juu ya katiba mpya zilianza katika siku za mwisho wa madaraka ya KANU (dada yake CCM katika harakati za kupigania uhuru), mwaka 2002.
Kati ya 2003 na 2005, Kenya imekuwa na mchakato uliozaa miswada mitatu – Muswada wa Ghai, Muswada wa Bomas na Muswada wa Wako.
Katika yote, muswada wa Bomas ndiyo ulikuwa unawakilisha maoni ya wananchi. Lakini Rais Mwai Kibaki aliwageuka wananchi, akatumia mwanya wa vifungu vinavyofanana na vya muswada wetu nilivyotaja hapo juu na vingine, kupuuza maoni ya umma.
Akamtumia waziri wake wa sheria, Moses Wako, kupitia upya maoni ya wananchi (muswada wa Bomas) ili kutengeneza muswada unaowafaa wakubwa uliojulikana baadaye kama Muswada wa Wako.
Bahati nzuri, Wakenya walibaini njama za Rais Kibaki. Wadau wakagawanyika. Serikali ikameguka. Walipofanya kampeni na kupiga kura ya maoni, wananchi wakaibwaga serikali. Muswada wa rais ukakwama!
Inamshangaza na kumsikitisha sana mzee Warioba kuona serikali inasitisha muswada mbaya wa aina hii. Anashangaa kuona wananchi wanahojiwa katika suala linalogusa uhai wa maisha yao.
Anasikitika kuona wananchi wamekuwa na uwezo wa kuona kasoro zote walizoona, ,ambazo serikali haikuziona (hata hivyo ndiyo iliyoziasisi). Anashangazwa na wasiwasi wa wananchi juu ya haraka ya serikali kupitisha muswada mchafu kwa hati ya dharura.
Hajajua wananchi wamepata wapi nguvu hii. Hajajua kuwa wananchi wamechoka kuishi na kuongozwa kwa mfumo wa kale. Haelewi kwanini wananchi wenye mtazamo mpya hawataki mawazo mapya, na wangependa mchakato mpya. Tumsaideje?
Ndiyo, nakubaliana naye. Hii si mara ya kwanza kwa serikali kuleta muswada. Kwa hiyo? Tutumie mbinu za kale kupata katiba mpya?
Ndiyo, Bunge ni chombo cha uwakilishi wa wananchi. Lakini ni mara ngapi (naye ameshuhudia) Bunge hili hili likishindwa kuwakilisha wananchi?
Mara ngapi Bunge hili limetunga sheria mbovu? Mara ngapi limetumika kutia mihuri miswada michafu ya serikali, kupuuza maoni ya wananchi na kukumbatia maoni ya chama chenye wabunge wengi? Mara ngapi limetumika kama kamati ya chama?
Ndiyo, hakuna muswada wa katiba uliowahi kupelekwa kwa wananchi. Ndiyo maana tumeishia kuwa na katiba yenye viraka. Na ndiyo maana wananchi wameendelea kudai katiba mpya. Wananchi wamechoka kuchakachuliwa! Warioba na Kombani hawana uwezo wa kuliona hili?



h.sep3.gif

 
Kebehi za kashililah na Tundu Lissu huchoki?
ban.blank.jpg

Prudence Karugendo

amka2.gif
KATIBU wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, hakuwatendea haki wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tukitilia maanani kwamba kutenda haki ni kumpa mtu stahiki yake bila ya msukumo wowote mwingine ulio nje ya maamuzi.
Mfano, mwizi asipoitwa mwizi, pengine kwa kumfichia aibu hiyo, si kumtendea haki, sawa na ilivyo kwa asiyekuwa mwizi kumuita mwizi. Kutekeleza haki ndiyo njia pekee ya kuiendesha jamii katika hali ya utulivu, amani, uelewano na upendo, hiyo ni njia rahisi na salama.
Wakati akiongea na waandishi wa habari, siku ya Jumatano ya juma lilipita, juu ya masuala mbalimbali ya mwenendo wa Bunge la sasa, Dk. Kashililah alionyesha shaka juu ya umakini wa wabunge wetu na uelewa wao katika kuzifuata taratibu zilizopo kutimiza wajibu wao.
Mambo aliyoyataja kama kikwazo kwa wabunge walio wengi kushindwa kutimiza wajibu wao, ni pamoja na wabunge kutozielewa kanuni za bunge, wabunge kutopenda kusoma nyaraka mbalimbali wanazopewa ili kujiweka katika nafasi ya kushiriki mijadala kwa ufasaha.
Kupendelea kuuliza maswali yasiyo ya lazima, kwa mtazamo wake, anayoyachukulia kuwa ni ya kupoteza muda tu.
Kauli hizo za Dk. Kashililah zimenifanya nitilie shaka uelewa wake juu ya chombo ambacho yeye ni katibu wake (Bunge). Sababu anaonekana kulichukulia Bunge kama kitu cha kufanya mambo ilimradi tu.
Yaani, kadri nilivyomuelewa Kashililah, wabunge wakutane wafanye mambo kimyakimya, bila kuhoji wala kulalamikia lolote kisha waondoke zao wakiwa wamepewa sifa ya kutunza muda vizuri.
Hiyo kweli ndiyo inayopaswa kuwa sifa ya wabunge wanaowawakilisha watu walio na matatizo ya kila aina?
Inapaswa ieleweke kwamba Bunge ni mkusanyiko unaowakilisha mkusanyiko wa watu wa nchi nzima.
Fikiria mkusanyiko wa watu wa nchi nzima walio na matatizo ya kutoka kila sehemu ya nchi unavyoweza kuudhibiti ili uendeshwe katika hali ya minong'ono tu.
Kwahiyo basi pale, Bungeni, si mahali pa kunong'ona, maana hapafanyiki uchawi, pale ni mahali pa kuweka kila kitu wazi ili kama yapo mahitaji yatolewe ufafanuzi na kupatiwa ufumbuzi wa wazi bila ya usiri wa aina yoyote.
Dk. Kashililah anapowataka wabunge kufuatilia masuala yanayohusu majimbo yao kimya kimya ana maana gani?
Je, kama wabunge wanaweza kufuatilia masuala kimya kimya kwa kuwaona kila wanaohusika na mahitaji ya majimboni kwao, pale Dodoma wabunge wanakutana kufanya kitu gani?
Si wangekuwa wanapita mawizarani na kwingineko kufuatilia yale waliyotumwa na wapiga kura wao bila kupoteza muda na gharama za kuwaweka pale Dodoma?
Kwa nini tupoteze muda na kuingia gharama za bure kuwaweka pamoja wabunge wasiotakiwa kuongea wala kuuliza lolote?
Mbali na hilo, nasema Kashililah hakuwatendea haki wabunge kwa kuwaweka fungu moja na kuwakebehi kiujumla katika kile kilichoonekana kama kutaka kuwafichia aibu wale aliokuwa amewalenga.
Kashililah anadai eti wabunge hawaelewi Kanuni za Bunge. Anataka tuamini kwamba wabunge wetu wote hawaelewi Kanuni za Bunge! Ina maana tuna wabunge mbumbumbu?
Katika kuendelea kuwakebehi wabunge wetu akasema kwamba alitoa kompyuta, "lap top" 20 baadaye eti zikaja kukutwa zimemwagiwa bia na soda wakati zikiwa hazijatumika! Nani atanikatalia kwamba hayo si matusi ya rejareja kwa waheshimiwa wabunge?
Ninachojiuliza ni kwamba kwa nini hakuwataja wabunge wasioelewa kanuni za bunge ili ikiwezekana wapiga kura wao, kama ni wazalendo wa kweli, wasiweze kuwarudisha tena bungeni na hivyo kulipunguzia taifa mzigo?
Vilevile, kwa nini hakuwataja aliowapa kompyuta wakashindwa kuzitumia na kuishia kuzimwagia sijui chai na bia ili tukawaelewe? Kwa nini anataka kutumia mifano ya wachache kuwadhalilisha wabunge wote?
Yeye akiwa Katibu wa Bunge kwa nini hakusema wabunge wanaoonyesha udhaifu ni wa chama gani ili tukawasute na kukisuta chama chao?
Kukificha chama kinacholeta wabunge dhaifu kwa gharama ya kuwatoa kafara wabunge wote kunamnufaisha nani? Je, yeye naye hajioni kuwa ni mzigo kwa mantiki hiyo?
Kwa upande mwingine Kashililah naye kajionyesha udhaifu wake, katika maongezi yake kaonyesha ilivyo gharama kumpatia kila mbunge kompyuta ya mapajani "lap top", akiwa amesahau kwamba kila mbunge anapatiwa shangingi (gari), hivyo kama sio vichekesho ni kitu gani?
Serikali yenye uwezo wa kumpatia kila mbunge shangingi lenye thamani ya makumi ya mamilioni ya shilingi, ione tatizo la kuwapatia wabunge hao vifaa vya kuhifadhia nyaraka nyeti kwa njia ya kisasa kwa kuhofia gharama!
Kumbe gharama zinatazamwa katika mambo yaliyo nyeti tu, lakini kwa mambo ya anasa hapo gharama hazitiliwi maanani! Ndiyo maana mashangingi yanaonekana ni bei rahisi kuliko kompyuta!
Kwa upande mwingine, si ajabu mizigo ya makaratasi ya nyaraka wanayopewa wabunge badala ya lap top, ikawa na gharama kubwa zaidi kuliko hata lap top ambazo Kashililah anashangaa inawezekanaje kila mbunge apewe ya kwake.
Kitu kingine, Kashililah kajiingiza kwenye mashambulizi ya kijinsia, kazishambulia nafasi za viti maalumu. Kaenda mbali kiasi cha kuwaita akina mama wa viti maalumu kuwa ni mzigo bila kuitolea maelezo tofauti iliyopo kati ya wabunge wa viti maalumu na wabunge wa majimbo au wale wa kuteuliwa na rais.
Mimi naamini kwamba kama wapo wabunge wa viti maalumu wasiojishughulisha ni sawa na wabunge wa majimbo wasiojishughulisha, wapo wengi tunawafahamu. Si haki kuwadhalilisha wabunge wote wa viti maalumu kuwa ni mzigo.
Vilevile si haki kuwalinda wabunge wasiowajibika, wasiofuata kanuni za bunge, wasio na muda wa kusoma nyaraka, kwa kuwachukulia wabunge wote kuwa ni dhaifu.
Njia hiyo haiwezi kutusaidia kulirekebisha bunge letu kwa vile ugonjwa unafichwa makusudi ili kuwaondolea fedheha wanaoingia bungeni wakiwa waathirika wa uzembe, tutalitibu vipi tatizo lao na kuliweka Bunge letu katika muonekano tunaoutaka? Siri hiyo anayo Katibu wa Bunge.
Hapa nataka nitoe mifano inayoonyesha kwamba Dk. Kashililah kaamua kuwatoa kafara wabunge wote ili kuwalinda watu fulani.
Kuhusu wabunge kusoma nyaraka, inaeleweka kwamba miongoni mwa wabunge wachache wanaosoma nyaraka kwa umakini ni wale wa upinzani
Aliyekuwa mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa, inadiwa ndiye alikuwa kinara wa kusoma nyaraka mbalimbali ndiyo maana kila kukicha alikuwa akiiumbua serikali

Ukimuondoa Slaa, ambaye sio mbunge kwa sasa, Freeman Mbowe, Tundu Lissu, John Mnyika, Zitto Kabwe ni miongoni mwa wabunge wachache wasomaji wa nyaraka, Kashililah anaposema kwamba wabunge hawasomi nyaraka kweli amewatendea haki hao?
Kwa upande wa Kanuni za Bunge, kanuni hizo zimevurugwa mara ngapi katika Bunge hili ili kuwanufaisha wale wasioweza kuzitumia kanuni hizo jinsi inavyotakiwa?
Mfano tulimuona mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, alivyotumia Kanuni ya Bunge kutaka muongozo wa Spika lakini badala ya Spika kumpa mwongozo akampa vitisho na vikwazo.
Lema aliviruka vikwazo hivyo, Spika akatengua kanuni ili kuwanufaisha wasioweza kwenda sambamba na kanuni hizo. Sikumsikia Kashililah akiliongelea hilo.
Majuzi hapa ilitokea mbunge mmoja anayependa kujituma sana anapokuwa bungeni, Tundu Lissu, akawa anahangaika kuchangia marekebisho ya vifungu vya Muswada wa Sheria ya Utawala wa Mahakama, mwenzake mmoja akamuuliza Tundu Lissu kuwa wewe huchoki?
Nilijua kuwa swali hilo lilitoka kwa mmoja wa wabunge wanaoamini kwamba bungeni ni mahali pa kupumzika na kustarehe. Hivyo mbunge anapowajibika bungeni huku mwenzake akimshangaa, nani kati ya hao wawili anayepaswa kuingia kwenye kebehi za Kashililah? Au Katibu wa Bunge hayo hayaoni?
Kwa upande wa viti maalumu nataka nitoe mfano wa wabunge wawili, Halima Mdee na Christowaja Mtinda. Wakati Halima Mdee akiwa mbunge wa viti maalumu ni mbunge gani, hata awe wa jimbo, kwa upande wa akina mama, tukiusema ule ukweli, aliyekuwa anawajibika kama kijana yule?
Ndiyo maana wananchi wa Kawe wakaamua kumchomoa Halima kwenye viti maalumu na kumkabidhi jimbo. Ni uchaguzi sahihi kwa wana jimbo wa Kawe.
Mbunge wa pili ninayetaka kumuangalia kwenye viti maalumu ni Christowaja Mtinda. Mbunge huyo anaonekana jimboni kuliko hata mbunge wa jimbo.
Wana jimbo wanamtumia vizuri sana huku wengine wakiwa wamejisahau wakidhani kwamba ndiye mbunge wao wa jimbo.
Kawaida wabunge wengi wakichaguliwa, wale wanaokuwa na makazi yao vijijini wanayahamisha na kuyaleta mijini, lakini Christowaja Mtinda yeye kafanya kinyume. Yeye alikuwa mkazi wa Dar es Salaam kabla ya kuwa mbunge, lakini baada ya kuwa mbunge wa viti maalumu kaamua kuhamia jimboni kwake Singida.
Muda mwingi anautumia akiwa jimboni kwake. Wakati wabunge, wengi wao wakiwa ni wa majimbo, wakihamia mijini, hasa jijini Dar es salaam, Christowaja, mbunge wa viti maalumu, katoka mjini na kuhamia kijijini. Sasa Kashililah kusema kwamba mtu huyo ni mzigo kamtendea haki?
Nilipoongea naye mbunge huyo, Christowaja Mtinda, kuhusu kauli hiyo ya Kashililah, alikuwa na haya ya kusema.
Anasema nafasi za viti maalumu anazichukulia kama maandalizi kwa akina mama ya kuwapa uzoefu wa kisiasa ili hatimaye waweze kusimama majimboni kupambana na wanaume kwa kujiamini.
Anaongeza kwamba iwapo misingi ya uanzishwaji wa nafasi hizo inazingatiwa haoni ni namna gani nafasi hizo zinaweza kuleta utata.
Christowaja anasema kwamba mwanamke anayepata nafasi hiyo inambidi ajiulize ameitumiaje kwa muda wa miaka mitano kujijengea ujasiri wa kukabiliana na changamoto za kiuongozi na za kisiasa, amewezaje kujenga hoja za msingi kwa maslahi ya nchi zilizo nje ya itikadi za vikundi (vyama vya siasa).
Mbunge huyo wa Viti Maalumu kupitia CHADEMA, anaongeza kwamba wabunge wa viti maalumu ni wabunge wa mkoa mzima wakishughulikia kero, hususan za makundi maalumu kama ya wanawake na watoto, na mambo mengine ambayo aghalabu yanawekwa pembeni na wabunge wa majimbo.
Kwahiyo anasema kwamba wabunge wa viti maalumu wanaziba mapengo yanayoachwa majimboni.
Lakini hata hivyo, Christowaja anakiri kwamba si wabunge wote wa viti maalumu wanaozitumia nafasi hizo vizuri kama alivyoeleza hapo juu.
Anasema wapo wabunge ambao badala ya kuzitumia nafasi hizo kujiandaa kuyashika majimbo wao wanazigeuza mahali pa kupumzikia.
Anasema hiyo ndiyo sababu ya baadhi yao kuwemo kwenye nafasi hizo kwa zaidi ya vipindi vitatu bila ya kuwa na mpango wa kwenda majimboni. Kwa hilo anawapongeza CCM ambao wameamua kuweka ukomo wa vipindi viwili tu katika viti maalumu.
Mbunge huyo msomi wa kiwango cha juu, anasema kwamba mzigo ni kitu ambacho hakina utashi, akili, busara wala hisia, ni kitu kinachongoja kusogezwa au kubebwa tu.
"Kutufananisha sisi wanawake wa viti maalumu na mzigo ni matusi makubwa", anasema Christowaja. Anaona kwamba kwa hilo Kashililah kakurupuka, kama hakunukuliwa vibaya.
Eti kama kauli yake ilikuwa inamaanisha kiutendaji, basi kuna wabunge wa majimbo ambao yeye, Christowaja, anaona ndio mzigo mzito kwa wapiga kura na walipa kodi kuliko mtazamo wa Kashililah ulivyo.
Christowaja anasema huwezi kuacha kumtazama mbunge ambaye kazi yake bungeni ni kusinzia muda wote, ukawaona wanawake wa viti maalumu wanaochakarika bungeni kuwa ndio mzigo kwa nchi kwa vile hawana majimbo.
Kwa hali yoyote ilivyo Kashililah hakuwatendea haki wabunge, hususan wa viti maalumu. Itabidi atafute muafaka nao.


h.sep3.gif

prudencekarugendo@yahoo.com
0784 989 512
 
Eti mafisadi wa magazetini hawakamatwi!
ban.nasema.jpg

Christopher Nyenyembe

amka2.gif
WIKI hii Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa hapa nchini (Takukuru), Dk. Edward Hosea alipokuwa akihojiwa na Shirika la Habari la Uingereza (BBC) kupitia Idhaa yake ya Kiswahili namna taasisi hiyo inavyolalamikiwa kwa kushindwa kupambana na mafisadi hakukosa jibu.
Kimsingi mahojiano hayo yaliyofanywa na BBC yalitokana na mawazo tofauti ya wananchi kuwa Takukuru imeshindwa kupambana na mafisadi wanaopigiwa kelele kila siku na hatua iliyofikiwa na chama tawala (CCM) ya kujivua gamba na kuwataka mafisadi ndani ya chama hicho wajiondoe ni usanii.
Dk. Hosea hakupata shida ya kujibu swali aliloulizwa kwa nini taasisi yake haiwachukulii hatua watu wanaotajwa kujihusisha na vitendo vya ufisadi hali ambayo imewasukuma zaidi wanaharakati ambao baadhi wamekuja na mawazo ya kupendekeza taasisi hiyo ivunjwe kwa kuwa hakuna kazi inayofanya.
Anachoweza kujibu anasema kuwa "hawa mafisadi wanaotajwa ni mafisadi wa magazetini" ni mafisadi wa magazetini ambao vyombo vya habari ndiyo vinavyoandika lakini Takukuru haiwezi kabisa kufanyia kazi mafisadi wa magazetini, wao wana utaratibu wa kuchunguza na kuwachukulia hatua za kisheria.
Jambo la kushangaza, Hosea anasimama hadharani na kutamka kuwa mafisadi wanaotajwa na wengine waliojiuzulu kwa tuhuma kama hizo ni mafisadi wa magazetini ambao taasisi hiyo haina muda wa kuwashughulikia na hawaoni haja ya kuhangaika nao.
Majibu hayo ya mkurugenzi huyo kwa upande mmoja yanaweza kuwa na sababu za kitaalamu katika uchunguzi na kuwanasa mafisadi lakini kwa upande wa pili hathamini mchango wa vyombo vya habari kwa maana ya kuhabarisha, kuelimisha na kutahadhalisha umma juu ya masuala maovu ndani ya taifa.
Kauli ya Dk. Hosea kuwa mafisadi wanaotajwa magazetini haipaswi kuachwa hivi hivi ikapita kwa mawazo yake binafsi au ikawanyima wananchi haki ya kuamini kuwa haya yanayoandikwa na vyombo vya habari ni ya uongo, uchochezi na kwamba kinachoandikwa na kutangazwa hakiwezi kuisaidia Takukuru.
Ikumbukwe kuwa mara kadhaa Takukuru imekuwa ikifanya kazi zake kwa kutumia vyombo vya habari vinavyoaminika kwa umma lakini linapokuja suala la mafisadi hapo ndipo kauli ya kilichoandikwa hakina maslahi na kulinda hadhi ya Takukuru inayolalamikiwa kwa kushindwa kuwabana mafisadi hata kama wanatajwa na vyombo vya habari.
Dk. Hosea anakumbuka jinsi sakata la Rada lilivyoweza kuiletea heshima taasisi hiyo japokuwa kwa upande mwingine wa shilingi kulionekana dhahiri nia ya kutaka kuwalinda watendaji wa serikali waliohusika na njama za kuiibia serikali kwa kuinunua rada kwa bei ya juu kuliko thamani halisi.
Vyombo vya habari viliandika sana suala la Rada na hatua za kiuchunguzi zilielekeza kuwa ipo siku nchi itashinda na kurudishiwa ziada ya fedha zilizotaka kuibiwa na wajanja, Dk Hosea alipata wakati mgumu juu ya hilo, alikuwa akijibu maswali ya wana habari lakini hakuna siku aliyosimama na kusema kuwa habari za rada ni za magazetini.
Hajawahi kutamka hivyo kwa kuwa alijua wazi kazi na majukumu ya vyombo vya habari ambavyo havipaswi kunyamazishwa na kuacha kuandika habari vikisubiri Takukuru iseme ndipo habari zao ziandikwe na kwa maana hiyo utendaji wa vyombo vya habari hauwezi kuwa na tija kwa kusubiri mtoa habari ajiridhishe kwa maslahi yake.
Kwa kujua kuwa pande zote za taasisi hiyo na tasnia ya habari vinafanya kazi yenye lengo moja ili kuhakikisha kuwa maovu yanakemewa na wahusika wanachukuliwa hatua na vyombo vyenye mamlaka ya dola, hakuna chombo chenye dhamira nzuri kuhusu mafisadi na wananchi hawategemei kuwa na mafisadi wa magazetini.
Ili kuweza kujiridhisha kwa hilo,Takukuru hawana sababu ya kumhukumu mtu au kumtia mtu hatiani kwa tuhuma za ufisadi bila kuwa na ushahidi wa kutosha japokuwa ushahidi wa kimazingira unaweza kuwa msingi madhubuti wa kumshauri Rais Jakaya Kikwete kuwa hawana ushahidi wa kutosha kuhusu mafisadi hawa lakini kwa kutajwa kwao mazingira yanaonyesha ni mafisadi.
Hiyo inaweza kuwa hatua ya kwanza na kuangalia msaada wa taarifa ambazo Takukuru wanazipata kutoka kwenye vyombo vya habari, kazi kubwa ya Takukuru ni kutumia taarifa hizo kama chanzo cha awali cha kuwawezesha kuanza kuchunguza tuhuma zinazomhusu mtu fulani au kiongozi fulani kuliko kujibu kwa mkato kuwa hao ni mafisadi wa magazetini ambao taasisi hiyo haiwezi kupoteza muda kuwafuatilia.
Kama ilivyo Takukuru haiwezi kufanya kazi kwa kukurupuka lazima wajiridhishe kwa kina,kwa namna ya kuchunguza, kupeleleza na kuwa na ushahidi wa kutosha kuhusu watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi na pengine kuweza kumshauri Rais Kikwete kuwa hawa wanaotuhumiwa kwa ufisadi bado wanashikilia madaraka ya umma waliyopewa hivyo inakuwa vigumu kuwachunguza.
Kwa kuwa inakuwa vigumu kuwachunguza watuhumiwa hawa ni jukumu la Rais kwa ushauri alioupokea kutoka kwa Hosea hawezi kumdharau, rais anapaswa kupokea ushauri huo na kuwawajibisha watuhumiwa wa ufisadi ambao bado wameshikilia nyadhifa serikalini lakini hilo naona halitendeki.
Hatua ya kuwasimamisha kazi watendaji wa umma kungeisaidia zaidi Takukuru kufanya kazi zake vizuri na inakuwa vigumu kwa hawa wanaotajwa kwa ufisadi bado wanaendelea na majukumu yao serikali na kuwa na madaraka ya juu kwenye chama chao au kuendelea na ubunge kwenye majimbo yao walioweza kupata ushindi kwa kutoa rushwa.
Hizo zinaweza kuwa mbinu mbadala za kuifanya Takukuru ya Dk Hosea ionekane kuwa ina meno lakini watu wanaiona kuwa ni kibogoyo kwa kuwa wanaolalamikiwa kwa ufisadi na kuandikwa na vyombo vya habari hawaguswi kwa kuwa eti wameandikwa magazetini,ni mafisadi wa magazetini.
Dk Hosea anapaswa kutambua kuwa waandishi wa habari nao kwa upande wao wanafanya kazi kwa kuzingatia misingi ya taaluma yao, wakisongwa na maadili ya kazi, sheria na uadilifu bila kuwa na chembe chembe za chuki na uongo juu ya taarifa zao kwa kuwa nao wana nafasi kubwa ya kuchunguza ni habari ipi inapaswa kuandikwa kwa kuzingatia haki na kulinda heshima za watu bila kuwaonea.
Takukuru ivione vyombo vya habari kuwa ni dira madhubuti kwao na chanzo muhimu cha taarifa zinazoweza kuisaidia taasisi hiyo kufanya kazi zake vizuri na ikiwezekana kujenga mtandao wa kimawasiliano utakaokuwa na masilahi kwa taasisi hizo mbili kwa maana ya kuwafanya wananchi kuwa na taarifa sahihi na zisizokuwa na utata.
Ushirikiano mzuri kati ya Takukuru na Vyombo vya habari kimsingi kutawawezesha wananchi kujua hatua za msingi zinazochukuliwa dhidi ya mafisadi kwa maana halisi kuwa Takukuru haitoi hukumu wala vyombo vya habari havihukumu,masuala yote ya kisheria yanaishia mahakamani,hivyo ni jukumu la vyombo hivi kujikita zaidi kwenye uchunguzi wa kina kuliko kutofautiana.
Inawezekana, Dk. Hosea kapitiwa kidogo anapowaita mafisadi hawa kuwa ni wa magazetini na kusahau kuwa vyombo vya habari ni mshirika mkuu wa Takukuru na kama ukweli huo haupo basi mapambano dhidi ya rushwa yatakuwa magumu, Dk Hosea na timu yake wanapaswa kujipanga na kuamini kuwa hakuna mafisadi wa magazetini, wachape kazi, mafisadi wapo na wanajulikana.



h.sep3.gif

 
Kama taifa tumepotea, tunahitaji kujitafuta!
ban.nundu.jpg

Deus Bugaywa

amka2.gif
KAMA ilivyo umuhimu wa kujitambua kwa mtu mmoja mmoja, ajijue yeye ni nani, ana ndoto na malengo gani katika maisha haya, na atayafikia vipi malengo hayo, ili kwamba kuishi kwake katika ulimwengu huu usiwe upotezaji wa muda ndivyo ilivyo kwa taifa.
Kujitambua ni moja ya silaha muhimu kwa ukombozi uwe wa mtu binafsi, kikundi au taifa, bila utambuzi huo ni vigumu sana kujua wewe ni nani, unatoka wapi na unakwenda wapi.
Tena ni vigumu kujua kama njia unayopita ni sahihi au siyo sahihi, kwa sababu ili kujua kama uko kwenye njia sahihi na mwendo wako ni sawa ni lazima kwamba utambua unakwenda wapi bila hivyo njia na mwendo wowote kwako utakuwa sawa, utajiona unakwenda kwa sababu tu unatembea na siyo kwa sababu unaelekea kule uliko dhamiria kufika.
Kama taifa letu, tuliwahi kujitambua na kujua sisi ni taifa la namna gani, tunakwenda wapi, kwa sababu gani na kwa namna gani. Hakika wakati huo tulikuwa ni wasafiri ambao pamoja na kamba tulikuwa tunapita katika msitu mnene wenye kiza, lakini tulitambua kwamba hiyo ni sehemu ya kutufikisha kule tunakoelekea.
Juhudi zetu kama taifa na za mtu mmoja mmoja zilielekezwa kwenye ujenzi na uimarishaji wa safari yetu hiyo, tulikuwa ni wasafiri tuliokuwa na dira na mwongozo, hata kama safari ilikuwa ngumu lakini tulijua tunakokwenda.
Inawezekana Ujamaa hakuwa sehemu sahihi ya kuelekea, (hili nalo linahitaji mjadala), lakini tulitambua kwamba kama Watanzania tumedhamiria kujenga siasa ya ujamaa na kujitegemea.
Na ili kufika huko tuliweka misingi ambayo ndiyo ilikuwa njia yetu ya kutufikisha kwenye Taifa lenye ndoto. Tulikubaliana kwamba ili tufike huko ni lazima kwanza tuheshimu na kutambua utu wa binadamu kwa msingi kwamba binadamu wote ni sawa na ndugu.
Katika msingi huo hakutarajiwa Mtanzania amnyonye ndugu yake, binadamu yeyote yule, au atumie umaskini wa ndugu yake kujinufaisha yeye huku ndugu yake akiwa anaogelea katika lindi la umaskini.
Misingi hiyo pia ilijengewa dira na maadili ambayo ilitaka kwanza watu wanaopata fursa ya kuwaongoza Watanzania wenzao watambue kwamba vyeo hivyo ni dhamana na wanapasa kutumia vyeo kwa faida na maslahi ya umma, cheo hakikutakiwa hata kidogo kitumike kama nafasi ya kujipatia maslahi binafasi.
Miiko ya viongozi ililenga katika kuhakikisha kwamba manahodha wa Ngalawa yetu ( Tanzania ) wanashika usukani kwa mujibu wa misingi yetu inayotuongoza ili kuwawezesha kuwapatia nafasi ya kutumia uwezo wao wote kwa ajili ya Tanzania na kuwaepusha na migongano ya maslahi.
Hiyo ilikuwa Tanzania ile, sisemi ndiyo ilikuwa njia sahihi zaidi, la hasha, kama ilikuwa njia sahihi au ni kinyume chake, hilo si sehemu ya mjadala leo, lakini ninachosisitiza hapa ni umuhimu wa kujitambua na kuwa na dira kama taifa.
Leo tumekuwa taifa lisilo mbele au nyuma kwa sababu hakuna anayeweza kukueleza kwa uhakika hasa sisi ni taifa la namna gani na Tanzania ya ndoto yetu ni ipi. Tuko tu kama kondoo waliopotea ambao kila mmoja anaelekea njia yake mwenywe.
Kwa stahili hii ni rahisi sana hata kwa mbwa mwitu kukamata kondoo mmoja mmoja na kuwamaliza wote bila wenyewe kujijua kuwa wana adui ambaye anawashambulia kama kasi ya umeme.
Ndiyo maana wengine wetu tunadhani ni muhimu wakati huu ambapo taifa lipo katika mjadala wa kuandika katiba mpya, kujiuliza maswali ya msingi na ambayo baada ya mjadala wa kina na wenye tafakuri makini usiongozwa na jazba wala ushabiki, ili yatupatie majibu ya changamoto za msingi zinazotukabili.
Ni muhimu kujadili na hatimaye kuifanya katiba yetu itamke sisi ni nani kama taifa, tumedhamiria kujenga taifa la aina gani, na zaidi tuwe na maadili ya kitaifa ambayo yanatakiwa yaandikwe kwenye akili za kila Mtanzania, ili utashi umuwezeshe mtu kutambua kwamba hiki ninachokifanya ni kinyume cha maadili ya Utanzania au la.
Matatizo mengi tuliyo nayo sasa kwa kiasi kikubwa yanatokana na kukosekana kwa maadili ya Utanzania kiasi kwamba maslahi ya taifa yamekuwa ni jambo ambalo halieleweki vyema, kwa sababu kila mtu amekuwa na tafasiri yake.
Tukishakuwa tumejitambua, tutaweza kuanzia hapo sasa kujenga taifa ambalo litakuwa na matumaini, ambalo hata mantiki ya kupokezana vijiti kwa viongozi na kizazi hadi kizazi itakuwa na maana kwa sababu kuja kwa kiongozi mpya kutamaanisha tu kutumia mbinu mpya za kulisaidia taifa kufika kule tulikodhamiria.
Kinyume na sasa ambapo mabadiliko ya mawaziri katika wizara yanatosha kabisa kusababisha mabadiliko ya mitaala, vitabu vya kiada na vitu vingine muhimu katika ujenzi wa taifa.
Tukiweza kufika mahali kutambua kwamba sisi ni taifa la aina gani, tunataka kujenga Tanzania gani huko tunakokwenda, maana yake ni kwamba hata mitaala ya kufundishia itakuwa ina lenga kuwajenga watoto wetu katika misingi hiyo.
Kwa hiyo katika hali ya kujitambua kama hiyo hatutarajia kabisa kwamba waziri abadili mtaala wa elimu kwa sababu ambazo hazileweki au kwa sababu tu ana dili la mchapishaji fulani wa vitabu kwa hiyo anabadili mtaala ili yeye na swahiba wake wapate pa kuuzia vitabu.
Misingi hiyo pia itasaidia kuleta nidhamu ya kitaifa, kwamba hata katika mfumo wa vyama vingi tuliomo sasa misingi hii itasaidia kuimarisha umoja wetu wa kitaifa, tutategemea sera za vyama zitofautiane katika namna kutekeleza jinsi ambavyo wataifikisha Tanzania huko tulikoamua kufikisha na siyo kucheza na dira au misingi hiyo ya taifa.
Ni bahati njema kwamba sasa tunaazimisha miaka 50 ya uhuru ni fursa nzuri kutafakari ni kwa jinsi gani tumefika hapa, na hiyo itusaidie kuamua ni jinsi gani Tanzania ya miaka 50 au 100 ijayo itakavyokuwa.
Na katika kuamua dira na misingi ya kama taifa, ni muhimu kuzingatia kwamba hili bado ni taifa la wakulima, wafanyakazi na wachuuzi, haya bado, kama ilivyokwa miaka ya mwanzo ya uhuru ni makundi yanayowakilisha idadi kubwa ya Watanzania lakini pia ni makundi ya wananchi wanyoge wanaohitaji ukombozi wa kiuchumi.
Usawa wa binadamu na kuepuka matabaka, hasa hili linalokuwa kwa kasi sasa la wenye nacho na wasiokuwa nacho, kwa ajili ya kudumisha amani na mshikamano wetu kama taifa.
Amani siku zote na popote haiji kwa sababu ipo, ni matokeo ya haki, mahali pasipokuwa na haki hata kama leo kuna amani tele, ni suala la muda tu amani hiyo itakuwa mashakani, kwa hiyo haki ni jambo jingine la msingi la kusisitiza katika ujengaji wa misingi ya Tanzania ya ndoto zetu.


h.sep3.gif

Mungu ibariki Tanzania
0754449 421, drbugaywa@yahoo.com
 
Ridhiwani kujiamini huku kunatoka wapi?
ban.isango.jpg

Josephat Isango

amka2.gif
WENGI tunamjua mdudu panya mara nyingi ukimuona anatafuna vitu ndani ujue anajiamini na shimo lake lipo karibu, panya huyo hana wasi wasi anajua huko anakokimbilia adui yake hawezi kumfikia, wala kumsumbua kwa namna yoyote.
Sijui kama wanafalasafa mtakubaliana nami pia kuwa ukiona kobe yuko juu ya mti, ujue kuna mtu kampandisha, maana kobe kwa asili yake hawezi kupanda mti.
Hivi karibuni mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM) Ridhiwani Kikwete alitoa siku 14 kwa viongozi wa siasa nchini Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk Willibroad Slaa na Mchungaji Christopher Mtikila kukanusha madai yao ya kuwa yeye ni tajiri bilionea.

Nimejuliza Ridhiwani amepata wapi ujasiri wa kuwapa watu muda wa kuthibitisha mali zake? Anajiamini nini? Ridhiwani anatania Watanzania kwa kuwa anajua hatuwezi kuandamana kuchukua mali zetu alizojipatia kifisadi? Je anatumia Urais wa baba yake kuwa atalindwa, hatapelekwa popote, ndio maana anawapangia watu muda?
Tumjadili Ridhiwani, tunahoji huyu kijana ni nani hasa? "Ridhiwani Kikwete ni nani" amekuwa akituhumiwa kuwa na kundi lililo vuruga uchaguzi ndani ya jumuiya ya UVCCM miaka michache iliyopita?

Ndiye anayetuhumiwa kuwa chanzo cha vurugu ambazo zilisababisha Mwenyekiti wa UVCCM Masauni aachie ngazi mapema mwaka jana.
Kana kwamba haitoshi kijana huyu aliwahi pia kutajwa kuhusika na sakata la kuenguliwa kwa mgombea ubunge fulani kwa sababu ya kutokuwa Mtanzania. Uraia wake ulitiliwa mashaka.
Anajiamini kuliko mawaziri na marais wote waliowahikutajwa kuwaibia Watanzania, na hawakuwahi kumshtaki Dr. Slaa, zaidi ya kubaki na kauli kuwa ni mpinzani.

Ridhiwani anajiamini kuliko baba yake, kuliko Edward Lowassa, Andrew Chenge, Rostam Aziz, Benjamin Mkapa, Nimrodi Mkono, Basili Mramba, Daniel Yona, Gray mgonja na watuhumiwa wengine wa ufisadi waliowahi kutajwa? Je, anapata wapi ujasiri huu?
Hatuwezi kuacha kuhoji huyu kijana ni nani? Je, ni nafasi aliyonayo ndani ya UVCCM? Kama ni hivyo mbona wapo wajumbe wengi ambao hawasababishi vurugu kama hizi. Mbona wengine hawatuhumiwi kwa ubilionea wa haraka kama ilivyo kwake?
Ridhiwan anatuhumiwa kujitajirisha kwa kutumia mgongo wa nafasi ya Urais anayoshikilia baba yake, Rais Jakaya Kikwete kwamba licha ya kutoka shule juzijuzi, kijana huyo hivi sasa ni bilionea.
Ridhiwan bila woga akarudi kuwakemea wazee hao kuwa anawapatia wiki moja wathibitishe? Hebu tumuulize je, iwapo Dk. Slaa na Mchungaji Mtikila wakithibitisha utawaambia nini watanzania?
Mali zinazodaiwa kujulikana na Watanzania wanaziona hata Dk. Slaa asipozitaja, pamoja na mashamba yaliyoko Burka Arusha ambayo kupatikana kwake kuna utata, na hili mpaka Dk. Slaa akutajie? Jamani hata jengo ulilolinunua miezi michache iliyopita pale Kimara unapoelekea Bonyokwa, na hili mpaka Dk. Slaa ataje?
Itakuwaje siku ukitajwa kumiliki kampuni ya mabasi, kuhusishwa na tenda za magari ya jeshi? Kwanini Ridhiwani unawakejeli Watanzania? kwanini anadhalilisha Ikulu? Tena kwa kejeli, kebehi na utani mwingi?
Watanzania hawajaweza kujiuliza hivi ujasiri huu wa kuwapa watu siku saba hadi 14 kuthibitisha ubilionea wake ameupata wapi? Hata watuhumiwa wa ufisadi wakubwa waliowahi kutajwa akiwemo Rais Kikwete hawajawahi kutoa siku hizo wala hawajawahi kwenda mahakamani kushitaki?
Pamoja na kutoa siku hizo Dk Slaa amejitokeza amesema uende mahakamani, tunasubiri kwa shauku kubwa ili uithibitishie dunia kuwa unaonewa? Na kama usipoenda mahakamani maana yake umekubali tuhuma za ubilionea ambazo Dk. Slaa na Mchungaji Mtikila wamezitoa.
Ujasiri wa kifisadi usio na tija wala heshima kwa walalahoi, itafika wakati Watanzania watadai mali zao, tena watachukua kwa maandamano ujasiri huu wa kuwapa watu siku je, utakuwepo?
Ridhiwani anatumia mwanya huo kujibu kwa kejeli, kwa kuwa ana hoja zifuatazo, iwe ni bilionea au sio bilionea, yeye yupo juu ya sheria kwa kuwa baba yake ni Rais. Iwe amejipatia mali kwa njia isiyo halali au kwa kupitia mgongo wa Ikulu au kufanya biashara kwa kutumia nembo ya Ikulu anajua kuwa atalindwa na vyombo vyote vya usalama.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) itamsafisha na polisi watamlinda hivyo atakuwa salama. Ridhiwani anajua wapo watu walioiba tena wazi wazi na wametuhumiwa na Dk. Slaa na viongozi wengine lakini serikali haijawachukulia hatua hata kidogo na wanaendelea kuvinjari mtaani.
Ridhiwani anajua kuwa hata wezi wa EPA waliiba na wakarudisha kiasi fulani baba yake akawaficha hakuwataja, aliwastahi. Sasa kama Baba yake aliwastahi wezi wengine waliojipatia mali isivyo halali, itakuwaje kwa mtoto wake kipenzi?
Hapo si ndio atakaa naye na kugonganisha glasi kumwambia safi mtoto mzuri? Ridhiwani anajua hata Baba yake anatajwa katika ufisadi hivyo naye anafanya vile vile, kama methali zinavyosema, mtoto wa nyoka ni nyoka, na mwana wa mhunzi asiposana hufukuta. Inawezekana anaiga jadi ya baba?
Ridhiwani anajua kuwa hata akikiri hadharani kuwa ni bilionea, hakuna wa kumfanya kitu, kwani wapo waliowahi kutajwa kumiliki vijisenti, bado wanaendelea kutesa, na Watanzania kwa jadi yao wanapewa majina kuwa ni watulivu na wapenda amani.
Hivyo hata ukiwadhulumu au ukajipendelea, hawawezi kunung'unika. Ni wapole japo wamepigika. Ndiyo maana kwa sasa Kenya, Uganda na Rwanda wanalalamikia mfumuko wa bei za vyakula, na mafuta lakini Tanzania ni kimya tu.
Je, wadhani Ridhiwan hajui kuwa Watanzania si wakulalamika hata mkiwadhulumu miaka yote? Anajua wazi kuwa watasahau muda si mrefu na ataishi kwa amani. Anajiamini! Hakuna wa kumtisha, ndiyo maana anatoa siku 14.
Ridhiwani anasema "Hapa mjini unaweza kumuona mtu amevaa suti ukadhani ya kwake kumbe ameazima. Mimi nina marafiki wengi, huwa wananiazima magari yao nitembelee, juzi juzi hapa nilikuwa na Benz ya rafiki yangu….jamani miundombinu ya mjini si mnaijua?
Kejeli gani hii ya mtoto wa rais? Tangu lini mtoto wa rais akaanza kuwa omba omba wa kuazima magari? Usalama wa Ikulu uko wapi ikiwa mtoto wa rais anaweza kuingia na kila gari la rafiki yake?
Na yeye huwa anawaazima nini? Au yeye huwa anapokea tu huwa hatoi? Inawezekana? Je, tuelewe kuwa Ridhiwani anatumia magari ya kifahari ya watu ili ajipatie umaarufu? Ni ya kina nani hao wanaompatia magari na ni kwa malengo yapi hasa?
Kama haitoshi narudia tena niliwaahidi ushirikiano na endapo watataka ili kuthibitisha yote hayo waliyosema na hata yale wanayoyasikia, wakithibitisha habari walizopewa ni za uongo basi wasisite kuueleza umma," anasema Ridhiwani.
Tangu lini kijana wa CCM akatoa ushirikiano kwa Dk. Slaa? Kejeli hizi za Ridhiwani za nini? Mbona anatufedhehesha Watanzania? Je, ni kwa kuwa hatuna mkate, anatukejeli kwa keki anazokula zinazotokana na kodi zetu?
Baada ya hapo, Rashidi aliondoka kuelekea gerezani (japo alikuwa anapinga unyonyaji na ukandamizaji) lakini alisema "Yana Mwisho haya". Rejea Riwaya ya KULI,
 
Asante kaka tumesoma tumeelimika pia Mungu akupe nguvu kwa kututoa gizani kwa kuzijua habari ambazo hatukuzijua hapo mwanzo.
 
Nyerere aliwahi kusema yeye si malaika amefanya mambo ya MAZURI na ya KIJINGA,watu wengi hawajui mambo ya kijinga ni yapi;
Mimi naona moja ya kauli ya kijinga ya huyu Mzee ni kusema hakuna Rais mzuri atakaye toka nje ya ccm.Alikuwa analea wizi ndani ya chama kwa kuwasifu akina Mkapa,JK,LOWASA,ROSTAM na mafisadi wote wanaoinajisi nchi yetu sasa.Hata 1995 JK alikuwa hafai kwa jinsi nchi ilivyokuwa hebu fikiria kama leo ni hivi je 1995 ingekuwaje.Kwa ujumla hakuna kiongozi msafi ndani ya ccm ya sasa kuanzia mwenyekiti wao kama yupo mtajeni tumjadili madudu yake,yaani jamaa(ccm) wanakera na kutia hasiri mambo ya msingi ndio wanafanyia mzaha na ni sawa na mwanaume aliyeuchi kudai anunuliwe kofia badala ya suruali eti KICHWA KINAONEKANA MAPEMA.
 
Kwenye Mkutano Mkuu wa CCM wa mwaka 1995 wa kumpitisha Mkapa kugombea uraisi, Nyerere alisema haya ambayo leo ninaona ni kero kwangu sijui kwenu na wala sikubaliani naye kwenye hilo hata kidogo.

Alisemaje? Hapa ninamnukuu:-



Mimi sikubaliani naye kwa sababu nimemwona JK jinsi ambavyo yupo beneti na mafisadi na anakula nao sahani moja na ndiyo maana na hata Bw. Kifimbo hapo nionavyo alichemsha.

Lakini Nyerere ana busara sana kwenye hotuba hiyo hiyo alinena yafuatayo ambayo yanagusa sasa kudondoka kwa JK na timu yake ya watafunaji wa fedha za umma. Na ninamnukuu:-


Si sasa yametimia………………….GO DR. SLAA...GO TO STATE HOUSE

Marekebisho kidogo hapo kwenye red. Inapaswa kusomeka kuwa "SASA YAMETIMIA". Naliona Taifa sasa linaelekea kwenye neema fulani hivi. Neema ambayo itarejesha mali zote zilizo porwa na mafisadi na marafiki zao, neema ambayo itarejesha njia kuu zote za uchumi kumilikiwa na umma. Oooh, Mungu isaidie CDM Mungu wape ujasili Watanzania.
 
Mwakani patachimbika bila jembe. Kwa nafasi ya ubunge natabiri wabunge wengi wa ccm hawatarudi , ijapokuwa bado kuna uwezekano wa ccm kuwa na idadi kubwa ya wabunge

Lakini sasa kwa nafasi ya uraisi kwa upande wa ccm wanaweza wakapoteza kitakacho wasaidia tu ni uwepo wa wabunge wengi watakao wapata hivyo kwa mujibu wa katiba watafanikiwa kupata waziri mkuu , kwani katiba inatamka wazi kwamba waziri atatokana na chama chenye wabunge wengi.

Kutokana na data za 2010 raisi alipata
kura 61% huku wabunge wa ccm bungeni wapo 75% ina maanisha kwamba ni rahisi sana kwa ccm kupoteza kiti cha uraisi kuliko bunge kuwa na 50% kwa 50%.

Nguvu kidogo sana zinahitajika ili kubeba kiti cha uraisi makamanda.

Viva chadema , vivaaa
 
....

Si sasa yametimia………………….GO DR. SLAA...GO TO STATE HOUSE
Hacha uvurugaji....hatujaamua bado sisi kama UKAWA kupendekeza nani wa kutuwakilisha. Subiri muda ukifika utataarifiwa. Kama una nia njema ya ukombozi wa Watanzania...usingemaliza andishi lako namna hiyo...unatafuta sehemu ya kuvuruga nguvu ya UKAWA. Kama una nia njema futa kipengele hiki kwenye post yako.
 
Kwenye Mkutano Mkuu wa CCM wa mwaka 1995 wa kumpitisha Mkapa kugombea uraisi, Nyerere alisema haya ambayo leo ninaona ni kero kwangu sijui kwenu na wala sikubaliani naye kwenye hilo hata kidogo.

Si sasa yametimia…
Bado hayajatimia ila yatatimia Ocober 25!.

Pasco
 
Back
Top Bottom