Idimi
JF-Expert Member
- Mar 18, 2007
- 14,970
- 10,462
Ndugu wanajamvi, katika pita pita yangu nimekutana na majina fulani fulani maarufu ambayo taasisi mbalimbali zimepewa, ambayo kusema kweli sijajua asili ya majina hayo, na nahisi huenda ni ya watu fulani waliokuwa maarufu sana ama viongozi, kama ilivyo kwa Mandela road ama Sam Nujoma road.
Mfano, ukifika katika hospitali ya taifa pale Muhimbili (MNH) kuna majina kama Mwaisela, Sewa Haji, Kibasila n.k. Hali kadhalika jina la Mwaisela ni jina la bweni katika shule ya Sekondari moja iliyo wilaya ya Mufindi kule Iringa, ambapo pia kuna bweni la Mkwawa katika shule hiyo hiyo. Jina la Tambaza sijajua linatokana na asili gani pia.
Naomba kuelimishwa asili ya majina haya na mengine mengi pia.