Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akutana na Rais Kikwete

Nampongeza cardinal kwani kwenye kuumwa, tofauti huwa hazina nafasi...mie ni Chadema lkn kwa hili semeni msemavyo....nyie ccm fanyeni dhihaka lkn sio kwa kujuliana hali.
 
Acha ujinga ww kumbuka huyu ni kiongozi wa nchi au hata mzazi wako unamtusi hivyohivyo
 
Tumefika pabaya sana kama nchi. Yaani kiongozi wa dini kuonana na rais raia tunaona ni tatizo!!! Wanaongea mema tu. Wangeweza onana kimya kimya kama wangekuwa na nia mbaya.

Ni tatizo tena tatizo kubwa kabisa. Pengo ni kiongozi wa RC Tanzania ambao ndiyo wanaomiliki Mkombozi Bank na hela za kifisadi zimepitia kwenye bank hiyo huku wanufaika wengine wakiwa na maaskofu na padre wa kanisa hilo, hivi unafikiri kwa nini watu wasihisi pengine pamoja na mambo mengine pengine Pengo ameenda kujipendekeza kwa JK ili benk yao iendelee kupeta?
Maaskofu wamepata mgawo wa hela za kifisadi mpaka leo kanisa halijatoa tamko lolote unafikiri sisi waumini tutaendelea kuwaamini? Kama viongozi wa dini wanashiriki dili za kifisadi mimi nawaona ni sawa sawa tu na mafisadi wengine. Wa-RC wanatakiwa wagome kutoa sadaka mpaka Kilaini na mwenzake Nzigilwa warudishe hela za Watanzania.
 
Ni Bahati mbaya sana kwamba Viongozi wengi wa dini wamegeuka kuwa wanasiasa na kuishia kupokea fedha chafu zinazozalilisha kanisa na utu wetu. Nilitegemea Pengo awe ameshamwajibisha Askofu Kilaini kwa kupokea chafu kupitia Benki ya Mkombozi ambayo ni Mali ya Kanisa Katoliki. Safari hii hatununuliki hata makanisani.. Tumechoka Ma CCM.

Mkuu taratibu za kanisa kiutawala hazimruhusu pengo kuwajibika askofu yeyote hapa nchini.Kila Askofu anawajibika kwa pope.Nadhani Vatican wanazo taarifa na they are working on it
 
Ni tatizo tena tatizo kubwa kabisa. Pengo ni kiongozi wa RC Tanzania ambao ndiyo wanaomiliki Mkombozi Bank na hela za kifisadi zimepitia kwenye bank hiyo huku wanufaika wengine wakiwa na maaskofu na padre wa kanisa hilo, hivi unafikiri kwa nini watu wasihisi pengine pamoja na mambo mengine pengine Pengo ameenda kujipendekeza kwa JK ili benk yao iendelee kupeta?
Maaskofu wamepata mgawo wa hela za kifisadi mpaka leo kanisa halijatoa tamko lolote unafikiri sisi waumini tutaendelea kuwaamini? Kama viongozi wa dini wanashiriki dili za kifisadi mimi nawaona ni sawa sawa tu na mafisadi wengine. Wa-RC wanatakiwa wagome kutoa sadaka mpaka Kilaini na mwenzake Nzigilwa warudishe hela za Watanzania.

nchi yao hii nyie wengine mpo kwa bahati mbaya!
 
Kikwete kama anataka uongozi wake uwe mgumu sana ajiweke mbali na kanisa takatifu itamgharimu mpaka mwisho Wa safari yake ya urais.
 
hela za kifisadi zimepitia kwenye bank hiyo huku wanufaika wengine wakiwa na maaskofu na padre wa kanisa hilo, hivi unafikiri kwa nini watu wasihisi pengine pamoja na mambo mengine pengine Pengo ameenda kujipendekeza kwa JK ili benk yao iendelee kupeta?
Right. Rugemarila alishaliweka sawa kanisa kabla hajapitisha fedha benki ya kanisa. Tibaijuka kaulizwa na Rais, kwa nini pesa ziliingia kwa jina lako na sio la shule inayopewa msaada, akasema ndio sharti la mtoa fedha. Sasa jiulize, kwa nini Rugemarila alilazimisha pesa isipitie benki yoyote kama sio hela chafu? Kanisa Katoliki limetakatisha fedha ndo maana maaskofu wamelipwa.


8E9U5018.jpg
Mara ya mwisho alionekana ofisini mwaka 2010 kama hiyo desk calender inavyosema. Tunataka kumuona zaidi akifanya kazi za nchi, sio kila siku ni mikutano na Mama yake Ray C na Mama yake Hashimu na Diamond na maaskofu wanao abet money laundering.

Julius Nyerere alikuwa mkatoliki aliyenusurika kupigwa risasi Saint Peters lakini alipachukulia Ikulu kuwa patakatifu kuliko kanisani, wa kina Pengo wa wakati huo hawakuwahi kukanyaga Ikulu kiholela holela. Tragically, Ikulu ya sasa ni pango la walanguzi.

Halafu ni kwa sababu tu nchi yetu bado hafifu kwenye tasnia ya habari na uhuru wa kusambazwa taarifa za nchi. Kiongozi wa Uingereza, kwa mfano, akikutana na mtu ikulu haitoshi kusema tu alienda kumjulia hali, angeulizwa wewe na Polycarp Pengo mliongelea nini? Ukisema alinijulia hali wanakuuliza "nini kingine?" Halafu udanganye uone!
 
Tunataka kauli pengo! Vp kuhusu msaidizi wako kuhusika katika hili?
Kilaini siyo msaidizi wa Pengo, wote hao ni wateule wa Papa, na Pengo alishasema hawezi kuliongelea hilo kwani mwenye mamlaka juu ya Kilaini ni Papa mwenyewe.
 
kama kumpa pole tu,kunaitaji usiri mkubwa wakutokuwa na mtu yeyote karibu wa kusikia yale yanayozungumzwa, huo ni uongo na Kikwete asifikirie watanzania wa sasa ni mambumbumbu hata wale wa upande wake wanakaa tu, kimya kwa sababu yuko madarakani, lakini akae akijua kwamba hila zote anazotufanyia lazima atazijutia mara tu atakapotoka madarakani. sisi kina gogo la shamba kazi yetu ni kubainisha kila kitu wazi usipofuata tunayokuambia utakuja kujuta
 
Mnajiuliza na kujijibu wenyewe. Roman Catholic church will always be powerful bila ya kujali mashambulizi ya walugaluga

Hata hivyo siku zote mko powerful katika kila aina ya ouvu. Nyie kwenu mnabariki dhambi tu. Kazi ipo kwakweli.
 
Back
Top Bottom