Mvula: Kasi ya Ukuaji wa Deni la Taifa na Kushuka Mauzo ya Nje Kunatishia Uchumi Wetu

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
610
1,540
Kasi ya ukuaji wa Deni la Taifa na kushuka kwa mauzo nje; hali ya uchumi wetu inatishia maendeleo ya watu.

Utangulizi
Kutokana na taarifa ya tathmini ya uchumi wa nchi yetu kwa mwezi Novemba mwaka jana 2022 iliyotolewa na Benki Kuu ya Taifa (BOT) inaonyesha kukua kwa kasi kwa deni la taifa.

Takwimu zinaonyesha ndani ya mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu kasi ya deni la taifa limeongezeka kwa Trilioni 21 kufikia Shilingi Trilioni 90.35 huku tukiona kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi umeendelea kukua kwa asilimia 4.5. kukua kwa deni la kumeibua mjadala kutoka makundi mbalimbali.

Sisi, ACT Wazalendo ilifanya uchambuzi wa ripoti tathimini ya uchumi ya mwezi Novemba 2022 iliyotolewa Disemba na Benki Kuu, pamoja na mambo mengine tumeona tuzungumzie maeneo mawili ambayo ni; Kasi ya ukuaji wa Deni la Taifa na kasi ya uingizaji wa bidhaa kutoka nje na kushuka kwa mauzo yetu kwenda nchi zingine.

A: Kasi ya ukuaji wa Deni la Taifa
Kwanza, ACT Wazalendo tumetafakari kuhusu kasi ya ukuaji wa deni la Taifa na hoja yetu kubwa ni kasi ya ukuaji wa Deni la Ndani inatishia maendeleo ya watu, uwezo wa nchi kujihudumia na kudorora kwa uchumi.

Ripoti ya Bank kuu ya mwezi inaonesha kuwa hadi kufikia Novemba 2020 deni la ndani la Serekali lilikuwa Trilioni 15.9 Novemba mwaka 2021 deni la ndani lilikua Shilingi Trilioni 18.6 na mpaka kufikia Novemba 2022 deni la ndani limefikia kuwa Trilioni 26.6 hili ni ongezeko ambalo halijawahi kutokea kwa zaidi ya miaka 20 katika Nchi yetu.

Takwimu zinaonyesha kuwa Novemba 2005 (Rais Mkapa anatoka Madarakani); Deni la nje la lilikuwa Dola za Marekani Bilioni 8.1 (Sawa na Tsh. Trilioni 9.8) na Deni la Ndani lilikuwa Trilioni 1.7. Wakati Kikwete anatoka madarakani mwaka 2015; Deni la nje lilikuwa dola za Marekani 15.4 (Sawa na Trilioni 33.2) na Deni la Ndani lilikuwa 7.9.

Miaka mitano ya Rais Magufuli hadi Machi 2021 deni la Nje lilikuwa dola za kimarekani Bilioni 24.4 na Deni la ndani lilikuwa Trilioni 16.1. Wakati wa Rais Samia Deni la Nje ni dola za kimarekani 27.5 na Deni la dani Trilioni 26.6 hadi mwezi Novemba 2022.

Kiwango hiki cha Deni la ndani ni asilimia 30 ya deni zima la Taifa, kwa Nchi za uchumi wa chini (Low-income countries) kama yetu uwiano wa Deni la ndani kwa Deni la Taifa haupaswi kuzidi 20% Hivyo, tunaona kwa muda wa mwaka mmoja, kasi ya ukuaji wa deni la ndani ni kubwa sana kuliko wakati wowote ule katika historia ya Nchi yetu. Mwenendo wa kukua kwa deni linaathari zifuatazo;

Nchi inatumia sehemu kubwa ya makusanyo yake kwenda kuhudumia deni badala ya kutoa huduma kwa wananchi. Kwasababu masharti yake yanakuwa ya papo kwa papo (muda mfupi).

Ukitazama taarifa za Benki Kuu zinaonyesha kila mwezi tunatumia bilioni 900 kwa ajili ya kulipa deni la Serikali, kati ya fedha hizo deni la ndani ni wastani Bilioni 600.5

Kutokana na masharti ya mikopo ya ndani kuwa ni ya muda mfupi Serikali inalazimika kuingia sokoni kukopa zaidi ili kulipa madeni (hatifungani) yaliyoiva.

Serikali na Sekta binafsi kugombania fedha jambo linalopelekea kuiminya sekta binafsi kupata mikopo kutokana na taasisi zinaona zinafaidika kwa rahisi kuikopesha Serikali kuliko sekta binafsi.

Ongezeko la utitiri wa kodi, tozo, ushuru na makato kwenye bei za mazao ya wakulima
Kucheleweshwa kwa malipo ya mafao na pensheni za wastaafu ambao ni wanufaika/ wanachama kutokana na fedha nyingi ambazo Serikali haijazilipa kwa taasisi hizo.

Ni rai yetu kuwa kwa mwaka huu wa fedha katika mpango wa bajeti ni muhimu Serikali kuja na mkakati wa namna ya kupunguza kwa kiwango kikubwa deni la ndani ili kuwaondolea mzigo wananchi wa kuminywa kupitia utitiri wa kodi, tozo, ushuru na makato ya bei za mazao kwa ajili ya kulihudumia deni.

Aidha, tunatoa wito kwa Serikali kupunguza Deni la ndani kwa kulipa kwa mkupuo madeni ya ndani na hatifungani ili kuweka uwiano daiwa.

B: Mauzo ya bidhaa nje ni kidogo sana kuliko bidhaa tunazoingiza

Suala lingine la uchumi wetu ambalo halijazungumzwa kabisa huku athari zake zikiwa ni kubwa zaidi ni uwiano wa bidhaa tunazouza nje na bidhaa tunazoingiza ndani.

Kwa mujibu wa taarifa ya Benki Kuu kwa mwaka ulioishia Novemba 2022 tuliuza nje bidhaa zenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 11 wakati huo tulitumia kiasi cha Bilioni 16 kununua bidhaa kutoka nje. Mwenendo huu wa uchumi wa nchi yetu umepelekea kuwa na upungufu wa bilioni 5 hali ambayo haijatokea kwa miaka 20 (mara ya mwisho ya kuwa na upungufu mkubwa kati ya mauzo ya nje na ndani ilikuwa mwaka 2000) katika historia ya nchi yetu. Athari za Mwenendo huu ni zifuatazo;

Kuingiza mfumuko wa bei unaotokana na kupanda kwa bei za bidhaa sehemu zinakochukuliwa (imported inflation)
Kupungua kwa akiba ye fedha za kigeni jambo linalopelekea kushuka kwa thamani ya shilingi dhidi ya dola ya Marekani kutokana na kutumia dola nyingi sana kupata bidhaa za nje wakati tunapata dola kidogo sana tunapouza bidhaa zetu nje ya nchi.

Kushuka kwa uwezo wa nchi kuagiza bidhaa kutoka nje kutoka miezi saba mwaka 2021 mpaka miezi minne sasa ambapo ni chini kiwango cha Jumuiya ya Afrika Mashariki na SADC ambapo wameweka miezi 4.5 na 6.

Katika kuleta uwiano mzuri wa mauzo ya nje na kupunguza kasi ya uagizaji wa bidhaa kutoka nje, Serikali inapaswa kuchukua hatua za haraka; kwanza, kuongeza uuzaji wa bidhaa za kilimo kwa kuongeza thamani ya mazao kama vile korosho yaani kuuza korosho iliyobanguliwa inaweza kuongeza mauzo ya nje Shilingi Trilioni 1.16, sobean kwa kuuza China ambapo ndani ya Miaka 2 inaweza kutupatia Trilioni 2.3. Hivyohivyo kwa mazao kama ya ufuta, mbaazi, kahawa na pamba.

Kwa ujumla, ACT Wazalendo tumetafakari mwenendo wa deni la taifa na biashara ya nje hivyo tunaitaka Serikali ichukue hatua zifuatazo;

i) Kuweka nguvu kubwa Mchuchuma na Liganga ili kusafirisha chuma na kupata chuma cha ndani mfano ripoti ya Benki Kuu inaonyesha tuliagiza chuma kwa Shilingi Trilioni 1.63 mwaka 2022 kuanzia Januari mpaka sasa.

ii) Serikali ipunguze uwiano wa mikopo ya kibiashara kwenye deni la Serikali hadi kufikia asilimia 20. Hatua hii itapunguza mzigo wa Serikali kugharamia madeni, na hivyo kuipa unafuu Serikali kugharamia sekta zingine za Maendeleo ya wananchi kama vile afya, elimu, maji, umeme na kilimo.

iii) Serikali ipunguze matumizi ya bidhaa zisizo za ulazima kutoka nje ya nchi ili kuleta uwiano wa kibiashara na kukuza uzalishaji wa ndani kama vile malighafi za miradi mikubwa kama vile Reli na Bwawa la Kufua Umeme la Mwalimu Nyerere hakuna sababu za kuagiza chuma nje wakati tunaweza kukipata ndani ya nchi yetu.

iv) Kwa hatua za muda wa kati, tunaitaka Serikali iharakishe Mradi wa kusindika Gesi wa Lindi (LNG) ili kuongeza uwezo wa kuuza bidhaa nje ambao utaongeza fedha za kigeni.

Hitimisho
Tumeona viongozi wa Serikali wakijitokeza mara kwa mara kubeza watu wanaohoji mwelekeo huu usioridhisha wa uchumi wa nchi yetu.

Tunaendelea kutoa rai kuwa Mwenendo wa uchumi wetu sio nzuri kama Serikali haitochukua hatua stahiki kukabiliana na hali hii itaumiza wananchi wake.


Imetolewa na:
Ndugu Emmanuel L. Mvula
emmauel.mvula@yahoo.com
Msemaji wa Sekta ya Fedha na Uchumi
ACT Wazalendo
15 Januari.
IMG_0124.JPG
 
Mnawapigia tu 🐐🐐🐐🎸

Nothing will happen! Na maisha yataendelea tu kuwa magumu kadiri siku zinavyokwenda.

Maana siku zote sikio la kufa, halisikii dawa.
 
Halafu Mvulla ni lawyer....Leo anafanya economic analysis, au ndio a jack of all trades
 
Nawakubali sana ACT kwenye kujenga na kuchambua hoja kuliko chama Chochote hapa nchini
Mkiendelea hivi mna kura yangu 2025

Btw ni kweli uchumi wetu upo hataran kina Mwigulu wapambane kuinua uchumi sio kupiga kelele tu
 
Hii analysis ni nzuri na itakuwa imefanywa na Zitto Kabwe ila kwa sababu za kinafiki na kulambishwa asali amechelea kuiweka yeye kwenye public domain ili kutowachukiza watawala wanaowalambisha asali!

Mvula namfahamu vizuri na Zitto namfahamu vizuri tangu UDSM !

Zitto lazima afahamu kuwa hakuna kitu Viongozi tulionao wanaweza kufanya kwenye mambo ya uchumi wa Chuma na Makaa ya mawe tuliyonao Mchuchuma ,Liganga na Ruvuma .

Tuna Chuma na tuna Makaa ya mawe lakini muulize hata Waziri Mkuu Mhe.Majaliwa kama Serikali ina mpango wowote wa maana hapo.

Yeye anachoweza kufanya ni kwenda kwenye Chuma na Makaa ya mawe na kusema Rais Mama Samia amenituma nije kuangalia hiki Chuma na Makaa ya mawe basi!
 
ACT hamfai kuwepo kwenye ulingo wa sisa Tanzania maana mmeungana na wadhalimu na michwa itafunayo rasilimali za nchi bila huruma
 
Back
Top Bottom