Mvua yaua wawili mkoani Kigoma

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Watu wawili wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa mara baada ya kupigwa na radi wakati mvua kubwa ikinyesha.

Akizungumza leo, Novemba 9, 2020, kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma, James Manyama amesema tukio hilo lilitokea Novemba 8 mwaka huu, majira ya saa tano asubuhi wakati mvua hiyo iliyoambana na radi kunyesha katika Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Amesema Khalifan Yassin (16), mwanafunzi wa darasa la sita, alifariki na kwa kupigwa na radi huku mwili wa mtu anayedhaniwa kuwa na umri wa miaka 10 hadi 11 ukiokotwa kando kando ya mto kata ya Kibirizi. Hata hivyo mpaka sasa bado hajatambulika.

Amesema mvua hiyo iliyokuwa ikinyesha kwa kuambatana na radi iliwajeruhi wanafunzi watatu wa shule ya sekondari Jehad.

"Wanafunzi hao kwa sasa wawili wanaendelea vizuri, walipatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa ya Maweni na kuruhusiwa kwenda nyumbani. Mmoja yupo chini ya uangalizi wa madaktari kutokana na hali yake kuwa mbaya," amesema Manyama.
 
Watu wakifa kwa radi na mvua, vyombo vya habari haraka sana hutoa taarifa kwa umma.

Ila watu wakifa kwa amri ya kaisari kule Zanzibar/Mara/Mtwara. Vyombo vya habari hukaa kimya kama hawajui.

Hii ndio tafsiri sahihi ya neno "UNAFIKI WA VYOMBO VYA HABARI".
 
Back
Top Bottom