Kumekuwa na mjadala na ubishani wa kimtazamo katika suala la muundo siyo tu wa kiutawalawa dola (Serkali) lakini pia muungano wetu. Kwa kweli mambo haya mawilihayawezi (muundo wa utawala na muundo wa muungano) kutenganishwa.
Kwa upande wa muundo wa utawala kuna ambao wanapendekeza mfumo wa majimbo ambao utatoa mwanya kwa watu kujitawala na kujiamulia mambo yao ya kimaendeleo ikiwemo ya kijamii na uchumi. Serkali kuu ikibaki na masuala muhimu ya kitaifa na pia kuratibu maendeleo ya jumla kwa nchi nzima. Ninakumbuka hii ilijaribiwa miaka ya sabini (wakati wa Chama kimoja) katika mfumo wa sasa kwa sera za madaraka mikoani ingawa haikufanikiwa sana.
Lakini wapo watu wanaofikiria kuwa mfumo huu utaligawa taifa na hivyo kupigia chepuo muudo wa sasa ambao unagawa nchi katika mikoa, wilaya, tarafa, kata na vijiji lakini utawala ukiendelea kuongozwa kupitia Serkali kuu (Dar es Salaam) kwa mambo yote.
Kwenye muungano kuna maoni tofauti ya mfumo wake. Kuna wanaowaza kuwa tuendelee na mfumo wa Serkali mbili kama ilivyo sasa lakini tutatue kero zinazoonekana kuzaliwa ndani ya mfumo huu. Lakini pia katika mfumo huu kuna wanaofikiria kuwaSerkali hizi mbili (ya Muungano na ya Zanzibar) zinatakiwa kuwa na hadhi sawa na maraisi wake wawe na mamlaka yanayoligana! Ukitekeleza maoni haya unatengeneza tatizo lingine kwamba Muungano unalingana na upande mmoja (na kwa bahati mbaya upande ambao ni mdogo siyo tu kwa eneo bali hata kwa idadi ya watu) wakati upande mwingine hauko waziwazi – umemezwa na muungano!
Pia wapo wanaofikiria kuwa muungano wetu unatakiwa uwe wa Serikali tatu, yaani ya muungano, ya Zanzibar na ya Tanganyika (Tanzania bara). Hii nayo ina changamoto zake na hasa ya mgawanyo wa madaraka na jinsi ya uendeshaji wa Serkali ya muungano. Isipowekwa vyema itapelekea kuvunjika muungano mapema mno kuliko matarajio ya wengi. Kuna wanaodai muungano wa mkataba (na mara kadhaa wametolea mfano wa Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki). Sijui hasa wanachokitaka katika hili lakini nafikiri katika mfumo huu hakutakuwa na muungano. Lakini wapo wachache wanaofikiria kuwa muungano wetu sasa unatakiwa upelekwe katika daraja lingine la Serikali moja yenye mamlaka kamili katika nchi moja.
Kwa bahati mbaya tofauti hii ya mawazo ya mifumo ambayo inapelea tofauti ya muundo wetu wa utawala na muungano imekuwa ikichukuliwa kuwa ni sera za vyama vya siasa. Lakini inashangaza zaidi vyama hivi vinapodai kuwa mifumo hii ni ilani zao za uchaguzi na kuwa wanaposhinda wanaweka mkataba na watanzania jinsi ya kutawaliwa.
Hii si sahihi kwani haisaidii taifa letu kuwa endelevu. Fikiria tu chama kikishinda na ilani yake inataka muungano wa Serkali tatu na au hata wa mkataba na wakafanikiwa kuweka mfumo huu. Laknini baada ya miaka mitano Chama chenye sera na ilani yaSerikali mbili kikashinda uchaguzi, wakafumua tena na kutengeneza muundio wa Serikali mbili! Itakuwa vurugu tu ambayo haisaidii kuleta utulivu. Halikadhalikahii pia ni kwa mfumo wa utawala – wa majimbo au wa utawala wa Serikali Kuu kufanya kila kitu.
Ndiyo maana ni maoni yangu kuwa mfumo wa utawala na muungano haviwezi kuwa sera au ilani ya chama cha siasa. Haya ni masuala ya msingi ya uwepo wa taifa letu na wote tukubaliane ni lazima yawe ndani ya Katiba yetu ya nchi. Lakini haiwezi kuwekwa hivi hivi bila kujenga muafaka wa kitaifa. Tunapaswa kuyajadili nakufikia muafaka wa mfumo tuutakao na baada ya hapo kuuweka katika Katiba. Kinyume chake kwenda na mtiririko huu wa kivyama vya siasa itatuwia vigumu kuufikia huomuafaka na itatugawa. Tuache vyama vishindane kwa kutueleza katika ilani zao ni jinsi gani ya kuendesha Serkali kwa gharama ndogo katika mfumo tuliokubaliana.