Muuguzi Mloganzila adaiwa kujinyonga kisa kunyimwa mshahara

Kazi bila mshahara au mshahara wake ulikuwa unatumiwa na HR??

Dah! Hivi mtu unazuiaje mshahara wa mtu na kumtaka aendelee kufanya kazi!?

Utaratibu Ni kwamba hata mtu akisimamishwa kazi inapaswa mshahara wake wote apate na sio nusu mshahara Kama zamani....

HR atakuwa na walakini, maana haiwezekani mtu asimamishiwe mshahara na aendelee kwenda kazini...

Mshahara unasimamishwa kwa mfanyakazi ambae Ni mtoro sugu...
 
Ofisa Muuguzi (II) wa Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila, Dar es Salaam, Sarwat Soluwo amedaiwa kujinyonga hadi kufa kwa kilichodaiwa mateso aliyopitia baada ya kusimamishiwa mshahara na uongozi wa hospitali hiyo.

Taarifa za ndani ya hospitali hiyo zinaeleza Sarwat alisitishiwa mshahara kwa miezi michache iliyopita kutokana na tabia ya ulevi huku akihitajika kuendelea na kazi bila ya mshahara.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro alithibitisha kutokea kwa tukio la kujinyonga kwa kijana huyo na kusema uchunguzi unaendelea.

Kwa mujibu wa taarifa, baada ya kufanya kazi kwa muda bila mshahara, adhabu hiyo ilimuathiri na kugeuka ombaomba hospitalini hapo, ili apate fedha za kula pamoja na za kumuwezesha kufika kazini.

“Hali ilizidi kuwa ngumu kwake, akaanza kuuza vyombo vya ndani, ili apate kula na nauli, kuna kochi alinunua fedha nyingi aliuza Sh60,000 kwa sababu ya ugumu wa maisha na alizidisha unywaji wa pombe zaidi.

“Baada ya kulewa kuna watu walimdhuru akaletwa hospitali, alivyorudi nyumbani kwake hali ile ikamkwaza akachukua uamuzi wa kujinyonga,” alidai mfanyakazi mwenzake.

Shuhuda huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe alidai Sarwat kabla ya kuchukua hatua hiyo, aliweka picha ya mpenzi wake kwenye mtandao wake wa kijamii huku akibadilisha muonekano wa juu akiweka kiatu.

Shuhuda huyo alidai uongozi wa hospitali hiyo umekuwa ukiwanyima haki wafanyakazi kwa kuwanyima mishahara, kutoa adhabu bila kufuata utaratibu.

Hata hivyo, Mwananchi lilizungumza na Ofisa Uhusiano wa Muhimbili, Aminieli Eligeisha aliyesema “ni kweli marehemu alikuwa mfanyakazi wetu alifariki jana (juzi) nyumbani kwake, sababu zilizopelekea kifo chake na mengine yanayosemwa polisi wanachunguza na watatupatia majibu.

“Taratibu zote za kiutawala zinaendelea kufanyika kuhakikisha tunamuaga na kwenda kumpumzisha nyumbani kwao Arusha. Kesho (leo) asubuhi itafanyika ibada Mloganzila.”

Said Joseph, dereva bodaboda eneo la Chama alidai rafiki yake huyo kabla ya umauti alichukuliwa na gari maalumu la wagonjwa na kwenda kufungiwa kwenye vyumba vya wagonjwa wa akili kwenye hospitali ya Mloganzila.

Fatma Juma, mwanamke aliyekuwa akiishi na Sarwat alisema jambo pekee alilomshirikisha ni la ndugu zake kutaka kumhamisha kituo cha kazi.

Hata hivyo, alisema sababu za ndugu hao kutaka kumhamisha hakumueleza, lakini amekuwa akipokea simu za vitisho kutoka kwa ndugu wa mwanaume huyo.

“Kabla ya kufariki kwa mume wangu nilipigiwa simu na ndugu yake mmoja akaniambia nimwambie mume wangu aniambie maneno ya mwisho, sikuelewa mpaka tukio hili lilipotokea,” alidai Fatma.

Akizungumzia tukio sakata la mumewe kubebwa na gari la wagonjwa, alikiri tukio hilo kuwepo na bado hajafahamu mambo yaliyoendelea mpaka kilipotokea kifo.

MWANANCHI
pole kwa familia.
 
Ushahidi alioutoa Fatma unatofautiana na kilichoandikwa kwenye gazeti, uchunguzi wa polisi sijui utaweza kutuletea majibu ya uhakika?
 
Keywords...."alipolewa ,walimdhuru,hali hiyo ilimkwaza akaamua kujinyonga."


Wahuni walitifua samadi nini? Maana Dar sasa hv kumejaa mamende.

Tuachane na hilo

"Marehemu inaonekana alikuwa na depression /msongo wa mawazo kutokana na hali yake ya kiuchumi ilivyokuwa. Hakuna kitu kinatia msongo wa mawazo kama kuwa bankrupt ghafla mara baada ya kuwa ulizoea kushika pesa"

Hao waliozuia mshahara wake ilitakiwa wachukuliwe hatua kali sana. Sheria za utumishi wa uma haziruhusu dhuluma hiyo juu ya mfanyakazi wa taasisi ya uma. Waeleze huo mshahara waliouzuia upo wapi?
 
Waliosababisha hayo wasimamishwe kazi nao kwa uchunguzi
Haya ya police kutoa press wangekuwa wanasubiri kwanza mbona huwa wana kiherehere sana kwa majibu mepesi ?

Wanapenda kuwa na waandishi mapema bila majibu ya maana kwanini wasiwe wanasubiri

kuuza mkuu kuuza nyago.
 
Hii habari (ya kifo) ina vyanzo vingi sana kama ukiamua kuichimba

Madaktari (watumishi wenzake)
Serikali (uongozi wa hospitali)
Mke (hawara wa marehemu)
Ndugu wa marehemu
Wahuni waliomdhuru


Gari la wagonjwa
Kipigo
Kunyimwa (kufungiwa) mshahara
Maneno ya mwisho
 
Aliyetow naamuzi ya kusimamisha mshahara nae afanye kazi bila ya mshahara kwa miezi mi3 tu
 
Back
Top Bottom