Nashauri Kiwanja kidogo cha ndege kijengwe maeneo ya Hospitali ya Mloganzila

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,138
7,713
Kutokana na umuhimu wa hospitali hiyo ya Mloganzila kuwa ya Kimataifa, na kutokana na mahali ilipo, nashauri kutengwe eneo la kujengwa uwanja wa ndege ambao utaruhusu ndege zenye wagonjwa wa dharura kufika kwa haraka na kupatiwa matibabu.

Huu ni mpango wa muda mrefu, nimelenga miaka 50 ijayo, kwa sasa bado kuna eneo kubwa la kutosha.
 
kwa nini wasiwekeze kwanza kwwnye hospitali za wilaya? hospitali hazina hata gloves tu wewe unaongelea ndege? you are soo out of touch, unaishi nchi ya kusadikika …
 
Hospitali kubwa huwa zina eneo tengwa la kutua helikopta tu sio u wanja wa ndege na bila shaka litakuwepo huko Mlongazila
 
Hivi Apollo na hospital nyingine kule India zina viwanja vya ndege? Nafikiri kunahitajika helipad tu.
 
Kutokana na umuhimu wa hospitali hiyo ya Mloganzila kuwa ya Kimataifa, na kutokana na mahali ilipo, nashauri kutengwe eneo la kujengwa uwanja wa ndege ambao utaruhusu ndege zenye wagonjwa wa dharura kufika kwa haraka na kupatiwa matibabu.

Huu ni mpango wa muda mrefu, nimelenga miaka 50 ijayo, kwa sasa bado kuna eneo kubwa la kutosha.
Kabisa....
Unaona mbali sana...hapan'shaka ukipanda juu ya mnazi waweza iona unguja ileee.....
 
Kwa kigezo cha ukubwa hudhani ingekuwa na mantiki zaidi kujenga pale Muhimbili.

Ila kila hospitali kubwa lazima iwe na Helipad. Helicopter ni rahisi zaidi kutua na kupaa kuliko ndege.
 
Back
Top Bottom