Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 302
kobelloKitu mnachoshindwa kuelewa ni kuwa hata wanaCCM wapo wanaoupinga huu muswada,kwa hiyo cha muhimu ni kutoupitisha huu muswada.
Kuna swali ambalo baadhi yetu tunakwepa kujibu na naomba nijbiwe hapa ili nione wenzangu mnaonaje process hii anayoitumia rais.
Je,tunakubali kuwa serikali iliyopo ni serikali iliyoundwa kidemokrasia?Nikimaanisha,wabunge waliopo wamechaguliwa kidemokrasia?....na rais aliyepo amechaguliwa kidemokrasia?(mnaamini watanzania wengi walimpa kura ya ndio kikwete kuliko Slaa?
Hapa hatujadili nani rais wa kweli na yupi si wa kweli hiyo ni story nyingine kabisa haihusiani na muswada uliopo, tunachoangalia hapa ni je yaliyomo kwenye muswada yanakidhi matarajio ya watanzania walio wengi?