Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Katiba: Download na pitia uone kilichomo na usambaze

Mkuu,

Kwanini kila tusipokubaliana na jambo tunatishia amani? Wewe kama kiongozi unatakiwa kudiscuss makosa yaliyopo na kushauri wananchi jinsi ya kubadilisha au kuupinga muswada huu.

Kumbuka,hakuna mtu ambaye atakuja na muswaada utakaotoshelezea matakwa ya kila mtu,ila kisheria wabunge wa CDM au mbunge yoyote anaweza kusubmit muswaada binafsi bungeni na ukajadiliwa.

Serikali iliyopo madarakani ni serikali iliyochaguliwa na wananchi na ni serkali iliyoundwa na CCM ambacho ni chama kinachotetea wazi muungano wa Tanzania na Zanzibar,kwa hiyo what do you expect? They are going to protect the union, to them not protecting the union is like dividing their territory! Thats what they believe in.

Secondly, like Bagenda said, CCM as a party is cool with the status quo, so whats the big deal?Katiba mpya halikuwa lengo la CCM, kwani ulikuwa hujui? Ila, kama wananchi watataka katiba mpya basi tujadiliane, na president ametoa bill,kama ina makosa let's point out whats wrong and alert other MPs sio kutishana.

Lastly, jinsi ya kuchagua tume inabidi tuje na tume huru ambayo itasikiliza maoni ya wananchi, ila kama rais anapendekeza kuchagua tume, that's because he believes he has the right to do so, but again he can comply with the mass the same way he complied with the new constitution talks.

DON'T RESORT TO VIOLENCE!
 
Haya Watanzania Katiba hiyo imeanzwa kupikwa kama waganga wao wanavyofanya. Lengo hapa ni kufanya kila njia wazuie contribution ya watanzania na kulinda maslahi ya mafisadi na hiki chama ccm. My hope ni kwamba we raise hell to these people.

Tangulini mpata faida za hii katiba huyo huyo ajiondolee hizo faida ili wananchi wapate say? Lengo la ccm ni moja tu "to staop democratic reforms"​
 
Nimekuwa nikisema hapa JF mara kwa mara kwenye threads na comments zangu kuwa CCM na serikali yake wana mzaha na maisha ya Watanzania na hawapaswi kufumbiwa macho.............
 
na mimi najiunga na wale waliotangualia...sie huku bara hatujauona kabisa....aliye nao autumi tafadhari!!!!:disapointed:
 
Mswaada huu haujatulia hata kidogo kwani unataka kuturudisha nyuma kwenye tume mbalimbali zilizokuwa zinaundwa.

Kwa nini bado tunampa Rais mamlaka yote ya kuunda tume hizi? Ni lini Rais aliridhika na mapendekezo ya tume wanazoziunda kama siyo kuwadanganya na kuwafumba macho wananchi? Terms of references kwa nini zitolewe na Rais badala ya Bunge? Je, unafikiri Rais hawezi kuingiza terms za kulinda chama chake na masilahi ya kundi lake analolilinda?

Hapa watanzania na hasa wabunge wanatakiwa wafanye marekebisho, tume ya katiba ithibitishwe na bunge. Na kwa nini kuwe na idadi sawa ya uwakilishi kwenye tume kati ya Zanzibar na Tz bara wakati tunajua wazi kuwa Zanzibar ina watu wasiozidi milioni 1.5 na huku bara ina zaidi wa watu milioni 40?

Tuacheni siasa kwenye mambo ya msingi kama haya.
 
Nimeusoma muswada lakini nasikitika sana umempa rais madaraka makubwa utafikiri tunaandika katiba ya rais.

Rais anaunda tume
Yeye ndiye anayetoa terms of references
Yeye atakuwa analetewa kile kinachoendelea na kutoa a go ahead
Yeye ana mamlaka ya mwisho ya kuikubali au kuikataa nk nk

Kitu kingine nilichokiona
  • Kwa vile muswada umekataza vyama vya siasa na viongozi wa vyama kufanya kampeni watuambie nani atakayefanya kampeni
  • na kama mtu akiamua kufanya kampeni watatofautishaje na kampeni za kisiasa
  • kwa nini mtu afungwe jela kwa kutofautiana maoni na tume? hii si kumnyima mtu haki yake
  • je majority wakipinga watawafunga wote miaka miwili miwili?
Kitu kingine ambacho sikubaliani nacho ni Tume ya uchaguzi kukusanya kura ya maoni (referendum), sina imani na tume ya uchaguzi iundwe tume huru ya kukusanya kura ya maoni ya katiba kutoka makundi yote ya jamii.
 
Huu ni ujinga mtupu..........yaani raisi ndio anapewa majukumu ya kuchagua nani awepo kwenye tume?? Adidu za rejea?? Ripoti ya mwisho anapelekewa yeye?? Kuna nini hapo...??? Hamna kitu hapo ni changa la macho mchana kweupeeeeeeee...............na huu mchezo ukienda bungeni utapita kama wanavyotaka.......!!!! Hapa ni people's power tu hakuna njia nyingine!!!
 
Hii katiba si ya Kikwete leo yupo kesho ataondoka you never know rais ajaye kama na yeye akiamua kujilimbikizia madaraka hata yeye Kikwete anaweza asisalimike.
 
Mkuu,

Kwanini kila tusipokubaliana na jambo tunatishia amani? Wewe kama kiongozi unatakiwa kudiscuss makosa yaliyopo na kushauri wananchi jinsi ya kubadilisha au kuupinga muswada huu.

Kumbuka,hakuna mtu ambaye atakuja na muswaada utakaotoshelezea matakwa ya kila mtu,ila kisheria wabunge wa CDM au mbunge yoyote anaweza kusubmit muswaada binafsi bungeni na ukajadiliwa.

Serikali iliyopo madarakani ni serikali iliyochaguliwa na wananchi na ni serkali iliyoundwa na CCM ambacho ni chama kinachotetea wazi muungano wa Tanzania na Zanzibar,kwa hiyo what do you expect? They are going to protect the union, to them not protecting the union is like dividing their territory! Thats what they believe in.

Secondly, like Bagenda said, CCM as a party is cool with the status quo, so whats the big deal?Katiba mpya halikuwa lengo la CCM, kwani ulikuwa hujui? Ila, kama wananchi watataka katiba mpya basi tujadiliane, na president ametoa bill,kama ina makosa let's point out whats wrong and alert other MPs sio kutishana.

Lastly, jinsi ya kuchagua tume inabidi tuje na tume huru ambayo itasikiliza maoni ya wananchi, ila kama rais anapendekeza kuchagua tume, that's because he believes he has the right to do so, but again he can comply with the mass the same way he complied with the new constitution talks.

DON'T RESORT TO VIOLENCE!

Usitake kutudanganya watu wazima hapa. Kwa sheria hii ya rasimu ya katiba ni kwamba CCM have made their minds that they are not going to listen to people's demands.

Na ukweli ni kuwa hakuna kitakachowasimamisha kufanya hivyo kwa sababu wapo kulinda maslahi yao na ya chama chao kwa gharama yoyote.

Tukiendelea kucheka nao wanatumaliza hawa, nachelea kusema hapa katikati walitutoa sana kwenye ajenda za kisiasa wakatupeleka kwingineko kumbe walikuwa busy wanapika huu utumbo sio.

Hawa walazimishwe kufanya kile watanzania tukinachotaka na wala wasiombwe maana hawawezi kukubali.
 
mbona haijaandikwa kwa kiswahili, tutaelewaje sisi watz tulio wengi ambao lugha hii ndio tunaitumia
 
Nashukuru mungu nami nimeupata muswada japo kwa shiida. Nimeusoma kiasi ila naona kuna madaraka makubwa amepewa Rais Kuna issue kama ya wajumbe wa tume kutoka kila upande kwa usawa yaani Zanbibar nusu na Tanzania bara nusu, hapa hakuna uwiano.

Pia naona wanasiasa na vyama vyao wanatupwa nje ya mchakato, hii inakaaje manake katiba ni siasa na siasa ni katiba sasa kama vyama vya siasa vinatupwa nje ya mchakato itakuwaje?

Pamoja na hayo kama kuna mtu ana mswada kama huu ambao Wakenya waliutumia kujitengenezea katiba yao naomba atusaidie ili tuone wao walikuwa na Sheria ya aina gani. Mimi nilifuatilia mchakato wa Katiba ya Kenya na kukubali kuwa uliongozwa vizuri manake kampeni ziliruhusiwa hadi mawaziri wa Serikali ambao walikuwa against na Katiba pendekezwa walipiga kampeni. Nadhani walikuwa na sheria nzuri, si vibaya na waTZ tukitohoa toka huko.
 
Mkuu,

Kwanini kila tusipokubaliana na jambo tunatishia amani? Wewe kama kiongozi unatakiwa kudiscuss makosa yaliyopo na kushauri wananchi jinsi ya kubadilisha au kuupinga muswada huu.

Kumbuka,hakuna mtu ambaye atakuja na muswaada utakaotoshelezea matakwa ya kila mtu,ila kisheria wabunge wa CDM au mbunge yoyote anaweza kusubmit muswaada binafsi bungeni na ukajadiliwa.

Serikali iliyopo madarakani ni serikali iliyochaguliwa na wananchi na ni serkali iliyoundwa na CCM ambacho ni chama kinachotetea wazi muungano wa Tanzania na Zanzibar,kwa hiyo what do you expect? They are going to protect the union, to them not protecting the union is like dividing their territory! Thats what they believe in.

Secondly, like Bagenda said, CCM as a party is cool with the status quo, so whats the big deal?Katiba mpya halikuwa lengo la CCM, kwani ulikuwa hujui? Ila, kama wananchi watataka katiba mpya basi tujadiliane, na president ametoa bill,kama ina makosa let's point out whats wrong and alert other MPs sio kutishana.

Lastly, jinsi ya kuchagua tume inabidi tuje na tume huru ambayo itasikiliza maoni ya wananchi, ila kama rais anapendekeza kuchagua tume, that's because he believes he has the right to do so, but again he can comply with the mass the same way he complied with the new constitution talks.

DON'T RESORT TO VIOLENCE!

Kobello, kuna wakati watu wanafanya mzaha lakini kwa masuala nyeti na muhimu kwa mustakabali wa taifa letu kwa leo na siku zijazo mzaha ni hatua ya mwisho inayomtenganisha mwanadamu na wanyama wa porini.

Kinachojadiliwa hapa ni njia za mwanzo zitakazotuwezesha kupata katiba ya nchi. Katiba ya leo na vizazi vijavyo. Ni katiba ya Tanzania, na si katiba ya chama cha mapinduzi kama unavyotaka watu waelewe.
Mawazo ya kuwa muungano ni sera ya CCM au TANU ndiyo maana leo tuna matatizo makubwa sana kwa vile waliofikiri wakati huo hawakutofautiana na kobello kimazo. Tunataka hali hii isijirudie tena.

Kama hili halikuwa la CCM kwanini walimnya'ganya Mnyika hoja yake, na sasa unasema eti wabunge wanaweza kupeleka muswada, jiulize ule wa mnyika ulizimwaje pale bungeni.

Tunataka kuanzia sasa hizi fikra finyu 'he has the right to do so' zifikie mwisho. Hii ni nchi yetu na si mali ya mtu au familia.
Tutofautiane kwa mambo yenye mantiki sio ubishi hata kama hauna maana.

WanJF, hiki kitakuwa kipindi kigumu lakini tusimame pamoja kutafuta mstakabali wa taifa letu, tupingane kwa hoja na kwa ustaarabu, tuwapuuze wale watakaotaka kutuvuruga tukifahamu kuwa ndani ya msafara wa mamba kenge wapo pia.

Tuendelee kujadili hoja.
 
Jamani nimepitia hiyo rasimu.
Ninachoweza kusema ni kuwa hili ni changa la macho, na rasimu hii ikikubalika basi hatuna katiba mpya wala katiba huru.
Hii rasimu ni ya kuikataa kwanza hata kabla ya kufikiri katiba. Hii ndiyo itakayoamua katiba iandikweje, na ninavyoiona ni hatari kubwa.
Imempa mamlaka yote Rais, kuamua na kufanya atakalo, kuiandika peke yake, kuibadili au lolote lile.
 
The bottom line ni kuwa wapinzani watajikuta wanafanya makosa mawili makubwa:

a. Wakiendelea kupinga mswada huu bila ya kuja na wa kwao wataonekana wanategemea huruma ya serikali. Kama ilivyodokezwa hapo juu wanao wabunge Bungeni, basi waje na mswada wao wa wanavyotaka mchakato wa Katiba uweje. Miswada hiyo miwili wa serikali na wapinzani itashindanishwa na ule mzuri upite. Hili litalazimisha process ya reconciliation ya miswada ili upatikane mzuri zaidi.

b. Wasipoleta mswada wao wenyewe tofauti na ule unaoletwa na serikali, na wakabakia kulalamika na kupiga kura ya "hapana" au kutoka Bungeni haitabadilisha hali halisi, CCM itauteka rasmi mkataba wa Katiba na CCM itaanza mchakato wa Katiba mpya. Sasa ukishapitishwa ulivyo una vipengele vya kuzuia kupinga process nzima. Maana yake wapinzani hawataweza kabisa kuupinga bila kusababisha machafuko nchini.

Well, hapa wanajikuta wanalazimika kufanya maamuzi magumu.

A. Wakiendelea kuupinga nje ya Bunge wataambiwa si mje Bungeni mlete hoja zenu?
b. Wakienda Bungeni na kushindwa - yaani mswada ukipita ulivyo - kama ulivyopita ule wa Gharama za Uchaguzi - watajikuta wako katika huruma ya serikali kwani hawatoweza kuupinga na kwa vile tayari wao wameshagawanyika nina uhakika wapo watakaotaka wakubaliane na serikali na wengine watasema wasikubaliane.
c. Uchaguzi ujao utafanyika kwa Katiba Mpya itakayotungwa na kupitishwa na Wana CCM!!!
 
Kobello, kuna wakati watu wanafanya mzaha lakini kwa masuala nyeti na muhimu kwa mustakabali wa taifa letu kwa leo na siku zijazo mzaha ni hatua ya mwisho inayomtenganisha mwanadamu na wanyama wa porini.

Kinachojadiliwa hapa ni njia za mwanzo zitakazotuwezesha kupata katiba ya nchi. Katiba ya leo na vizazi vijavyo. Ni katiba ya Tanzania, na si katiba ya chama cha mapinduzi kama unavyotaka watu waelewe.
Mawazo ya kuwa muungano ni sera ya CCM au TANU ndiyo maana leo tuna matatizo makubwa sana kwa vile waliofikiri wakati huo hawakutofautiana na kobello kimazo. Tunataka hali hii isijirudie tena.

Kama hili halikuwa la CCM kwanini walimnya'ganya Mnyika hoja yake, na sasa unasema eti wabunge wanaweza kupeleka muswada, jiulize ule wa mnyika ulizimwaje pale bungeni.

Tunataka kuanzia sasa hizi fikra finyu 'he has the right to do so' zifikie mwisho. Hii ni nchi yetu na si mali ya mtu au familia.
Tutofautiane kwa mambo yenye mantiki sio ubishi hata kama hauna maana.

WanJF, hiki kitakuwa kipindi kigumu lakini tusimame pamoja kutafuta mstakabali wa taifa letu, tupingane kwa hoja na kwa ustaarabu, tuwapuuze wale watakaotaka kutuvuruga tukifahamu kuwa ndani ya msafara wa mamba kenge wapo pia.

Tuendelee kujadili hoja.
Nguruvi3

Unajua mkuu kuna watu wanafikiri tunajadili katiba ya CCM kuwa bila Makamba kukubali haitafaa mfano huyo kobello anaposema haikuwa sera ya CCM ana maana watanzania tuache kuijadili hadi hapo kamati ya CCM itakapokaa na kuipitisha.
 
Kitu mnachoshindwa kuelewa ni kuwa hata wanaCCM wapo wanaoupinga huu muswada,kwa hiyo cha muhimu ni kutoupitisha huu muswada.
Kuna swali ambalo baadhi yetu tunakwepa kujibu na naomba nijbiwe hapa ili nione wenzangu mnaonaje process hii anayoitumia rais.
Je,tunakubali kuwa serikali iliyopo ni serikali iliyoundwa kidemokrasia?Nikimaanisha,wabunge waliopo wamechaguliwa kidemokrasia?....na rais aliyepo amechaguliwa kidemokrasia?(mnaamini watanzania wengi walimpa kura ya ndio kikwete kuliko Slaa?
 
The bottom line ni kuwa wapinzani watajikuta wanafanya makosa mawili makubwa:

a. Wakiendelea kupinga mswada huu bila ya kuja na wa kwao wataonekana wanategemea huruma ya serikali. Kama ilivyodokezwa hapo juu wanao wabunge Bungeni, basi waje na mswada wao wa wanavyotaka mchakato wa Katiba uweje. Miswada hiyo miwili wa serikali na wapinzani itashindanishwa na ule mzuri upite. Hili litalazimisha process ya reconciliation ya miswada ili upatikane mzuri zaidi.

b. Wasipoleta mswada wao wenyewe tofauti na ule unaoletwa na serikali, na wakabakia kulalamika na kupiga kura ya "hapana" au kutoka Bungeni haitabadilisha hali halisi, CCM itauteka rasmi mkataba wa Katiba na CCM itaanza mchakato wa Katiba mpya. Sasa ukishapitishwa ulivyo una vipengele vya kuzuia kupinga process nzima. Maana yake wapinzani hawataweza kabisa kuupinga bila kusababisha machafuko nchini.

Well, hapa wanajikuta wanalazimika kufanya maamuzi magumu.

A. Wakiendelea kuupinga nje ya Bunge wataambiwa si mje Bungeni mlete hoja zenu?
b. Wakienda Bungeni na kushindwa - yaani mswada ukipita ulivyo - kama ulivyopita ule wa Gharama za Uchaguzi - watajikuta wako katika huruma ya serikali kwani hawatoweza kuupinga na kwa vile tayari wao wameshagawanyika nina uhakika wapo watakaotaka wakubaliane na serikali na wengine watasema wasikubaliane.
c. Uchaguzi ujao utafanyika kwa Katiba Mpya itakayotungwa na kupitishwa na Wana CCM!!!

Kwa mwendo huu wapinzani wamewekwa mtu kati! Bila ueledi na tafakuri jadidi wapinzani wataishia kuubariki muswada huu bila ya wao kupenda. Naona kama utapitishwa kuwa sheria, basi sheria itaanza rasmi June 2011, wapinzani wana muda kweli wa kuujadili huu muswada na kupata mawazo mujarabu ya kuwasilisha bungeni na bunge si ndio linaanza wiki ijayo. Kweli serikali wajanja wapinzani watakutwa pants down sijui watafanya nini kwa muda mfupi huu!!
 
Wapinzani walipotaka katiba mpya nadhani walishakuwa na katiba wanayoitaka au jinsi mchakato mzima utakavyoendeshwa.All they need ni kusubmit na kulobby wabunge waCCM either through their MPs or through the mass.Operation should start now,peaceful demos kupata support ya mass ambayo inaweza kuwainfluence MPs wa CCM kuback off.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom