Selemani Rehani
Member
- Aug 31, 2010
- 9
- 13
Serikali imewasilisha Bungeni kwa mara ya kwanza muswada wa marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa. Muswada huu unahitaji mjadala mpana ukiwashirikisha wadau wote ili tuweze kutataua baadhi ya changamoto zilizojitokeza katika uwanja wa siasa, na muhimu zaidi tuweze kusonga mbele na kuimarisha demokrasia nchini.
Muswada huu una mapendekezo machache mazuri, lakini kwa kiwango kikubwa una mapendekezo ambayo yatafifisha demokrasia iwapo mapendekezo haya yatapitishwa na Bunge.
Dhumuni la andishi hili ni kujaribu kuainisha baadhi tu ya mapungufu makubwa ambayo yanaweza kupelekea kuua mfumo wa vyama vingi ambao tumekuwa tukiendelea kuujenga na kuuimarisha.
Ni muhimu tukumbuke kuwa jukumu la kujenga demokrasia ya vyama vingi, ni jukumu la Watanzania, na si la nchi wahisani wala wafadhili na wala watawala. Ni sisi ndio tuna wajibu wa kupiga kelele pale tunapoona misingi ya demokrasia na utawala bora inaminywa.
Kama ambavyo tuna matatizo katika sheria nyingine, mapendekezo ya mabadiliko ya sheria hii yanampa madaraka makubwa sana Msajili wa vyama vya siasa.
Nitajaribu kueleza. Ila kabla ya kueleza, tujiulize maswali yafuatayo: Hivi ni kweli ana madaraka makubwa? Na je kuna ubaya gani kumpa mtu mmoja madaraka makubwa sana? Kuna athari gani kwa Msajili wa Vyama Siasa kuwa na madaraka makubwa sana? Na swali linguine muhimu, je Msajili tuliye naye anapatikana vipi? Je, anakubalika na wadau wote wanaoshiriki katika siasa? yupo huru na haegemei au kupendelea upande wowote? Je, tunaweza sote tukasema bila unafiki kuwa Msajili tuliye naye ni ‘neutra’, ‘impartial’? na independent?
Nianze na swali la kwanza : Kwa mujibu wa mapendekezo haya, ni maoni yangu kuwa Msajili wa vyama vya siasa amepewa madaraka makubwa sana. Katika kifungu cha nne kwa mfano, kinapendekeza kurekebishwa ili kubainisha majukumu ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Kipengele ‘C’ kinasema kuwa Msajili ataangalia chaguzi za ndani za vyama na mchakato wa uchaguzi. Haya ni madaraka makubwa sana na yanaingilia uhuru wa vyama vya siasa katika kuendesha mambo yao ya ndani kwa mujibu wa katiba zao. Itakuwa ni vyema sana tukipata ufafanuzi ya mantiki na faida za kumpa Msajili madaraka haya. Tunataka tupate matokeo gani? Ni jambo gani jema litapatikana kwa kumpa Msajili madaraka haya?
Ni sababu zipi zilizopelekea Msajili wa Vyama kupewa jukumu hili? Unaweza kusema labda ni kwa sababu chaguzi nyingi za baadhi ya vyama vya siasa hugubikwa na mizengwe, ukiukaji wa sheria, kanuni na katiba za vyama. Hili si jukumu la Msajili, bali ni jukumu la wanachama husika kuhakikisha kuwa chama chao kinafuata katiba na kanuni za uchaguzi walizojiwekea. Na Msajili ana mamlaka ya kuingilia kuona haki inatendeka pale wanachama wa chama cha siasa wanapohitaji Msajili kuingilia kati mgogoro uliopo ndani ya chama na kutoa haki. Kazi ya kulinda katiba, kanuni na kuhakikisha kuwa chaguzi zinafanyika kwa mujibu wa katiba na kanuni na uchaguzi ni wa haki na huru, ni kazi na wajibu wa wanachama wenyewe na sio Msajili wa Vyama vya Siasa. Mathalani, ni jukumu la wana CCM kuhakikisha kuwa utaratibu wa kura za maoni za kuwapata wagombea wa nafasi mbalimbali ama za Ubunge au Udiwani, zinafuatwa kwa mujibu wa katiba ya chama chao na kanuni zao.
Lipo swali la msingi sana: Je, Ofisi ya Msajili itaangalia chaguzi za vyama katika chaguzi za ngazi zote? Kama jibu ni ndio, je Ofisi hii ina rasilimali watu na fedha za kutosha kuweza kuangalia chaguzi zote za vyama vyote katika ngazi zote? Na kama jibu ni hapana, labda wataangalia chaguzi za ngazi ya Kitaifa, au Mkoa au Wilaya, je kuna faida gani kufanya hivyo na kuacha chaguzi katika ngazi za chini?
Kipengele ‘D’ kinampa Msajili mamlaka makubwa sana ya kusimamia utoaji wa elimu ya uraia kwa vyama vya siasa. Aidha kinaendelea kusema kuwa mtu yeyote au taasisi yoyote ya ndani au nje ambayo inataka kutoa elimu ya uraia au kujenga uwezo kwa chama cha siasa, kabla ya kufanya hivyo, mtu au taasisi hiyo italazimika kumtaarifu kwa maandishi Msajili na kueleza malengo na aina ya mafunzo, washiriki katika mafunzo hayo, zana za kufundishia (teaching aids) na matokeo tarajiwa.Msajili akipokea taarifa hiyo anaweza kukataa kutolewa mafunzo hayo au program yoyote ya kuwajengea uwezo na kutoa sababu.
Taasisi au mtu yeyote atakayekiuka kifungu hiki atahukumiwa, kupigwa faini sio chini ya milioni moja lakini isizidi milioni tano au kwenda jela sio chini ya miezi sita lakini isizidi miezi kumi na mbili au vyote viwili.Kipengele hiki kitaleta ugumu sana kwa vyama vyenye mashirikiano (sister parties) kutoka katika nchi mbalimbali kuweza kuwa na program za kujengeana uwezo, na kuendesha mafunzo kwa watendaji wake.
Piaasasi mbalimbali, wafadhili nao watakumbana na kikwazo katika kuendesha programu za mafunzo kwa vyama vya siasa. Kinachotia mashaka zaidi ni adhabu zinazotolewa kwa kuendesha mafunzo bila kibali cha Msajili wa Vyama. Hapa tena tunaona madaraka makubwa sana ambayo amepewa Msajili ya ama kukubali au kukataa utoaji wa elimu ya uraia na chama cha siasa ama kupata au kutopata mafunzo. Madaraka haya yamewekwa kwa mtu mmoja. Na maamuzi yake ni ya mwisho!
Kipengele 5B kinampa mamlaka Msajili kuwa anaweza kudai kupewa taarifa na kiongozi wa chama cha cha siasa au mwanachama kama zitakavyohitajika. Iwapo Kiongozi wa chama au mwanachama atakiuka kifungu hiki basi naye atakuwa ametenda kosa na atapewa adhabu ambazo nazo zimetajwa ikiwa ni pamoja na faini au kifungu au vyote viwili. Kipengele hiki kinaminya uhuru wa chama cha siasa, kwani baadhi ya taarifa zinaweza kuwa zinahusiana na masuala ya binafsi ya kichama ambayo chama husika wanaweza kuwa wasipende kuitoa kwa Msajili. Katiba yetu ya sasa inatambua haki ya faragha na usiri. Matahalani, taarifa iliyosheheni mikakati halali ya kupata ushindi kwa chama cha siasa, taarifa hii inaweza kuwa sio muafaka kwa chama husika kuiwasilisha kwa Msajili na hasa katika mazingira haya ambayo uhuru wa Ofisi ya Msajili bado unahojiwa na mazingira ya kutoaminiana katika medani ya siasa.
Yawezekana kuwa kipengele hiki kimependekezwa kulenga taarifa za fedha na hasa misaada ya fedha ambayo vyama hupokea kutoka kwa wafadhili wa ndani na nje nchi. Kuna uoga kuwa misaada hii yawezekana huwa inaliwa na wajanja wachache ndani ya vyama vya siasa au baadhi ya wafadhili wanaweza kutumia fedha zao ili tu kuondoa utangamano uliopo nchini. Hivyo, ni vyema kuwabaini ni kina nani hao wanaotoa fedha kwa vyama vya siasa na kwa malengo gani. Yawezekana kipengele hiki kinajaribu kuziba mwanya huu.
Kwa mfano, iwapo CCM imepokea msaada wa fedha kutoka China, kwa mfano, Msajili ana mamlaka ya kudai kupewa hizi taarifa kutoka kwa Mwenyekiti au Mwanachama na endapo wawili hao hawatatoa taarifa hizo basi wakabiliwe na adhabu kali kabisa.Nadhani hili ndio lengo ambalo si baya, ila tu kinachokosekana hapa ni kuaminiana. Swali la kujiuliza : Je, Msajili ataweza kutenda haki na sawasawa kwa chama tawala na vyama vya upinzani? Je, Vyama vya upinzani vina imani na Msajili? Vyama vya upinzani vina sababu za msingi kuamini kuwa Msajili anaweza asitende haki.
Kama ni hivyo, basi tutafute utaratibu wa kumpata Msajili ambaye atakubalika na kuonekana miongoni mwa wadau wote kuwa ana uhuru na hawezi kuegemea upande wowote. Pia kama lengo ni kuwa na uwazi kuhusiana na vyanzo vya mapato vya vyama, basi tuweke utaratibu wa kuwa timu maalum ya wakaguzi wa mahesabu ambao miongoni mwao watoke katika vyama vya siasa, kwa maana chama tawala na vyama vya upinzani. Aidha hali hii inaoyesha umuhimu mkubwa wa kukamilisha suala zima la kukamilisha mchakato wa kuandika katiba mpya na kuzipitia upya baadhi ya sheria kadhaa kama vile sheria ya gharama za uchaguzi n.k.
Itaendelea… hapa Muswada wa Marekebisho katika Sheria ya Vyama vya Siasa: Tunahitaji mjadala mpana (Sehemu ya Mwisho) - JamiiForums