Musoma: Baba na mwana wahukumiwa kunyongwa hadi kufa

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Mahakamani Kuu Kanda ya Musoma kupitia Mahakama ya Wilaya Tarime Mkoani Mara imewahukumu baba na mtoto wake wa Kijiji cha Genkuru kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya mauaji.

Waliohukumiwa ni Matinde Keranganyi (baba) na Mwita Matinde (mtoto) ambao walishtakiwa kwa kumpiga mawe, kumkata mapanga na kumchoma mkuki Chacha Nyamhaga, wakigombea ardhi.

Hukumu hiyo ilisomwa na Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, Frank Moshi.

Awali, Mwanasheria wa Serikali, Yese Temba, alidai kuwa washtakiwa Mei 25, 2019 kwa makusudi wakiwa na silaha za jadi walimvamia Nyamhanga akiwa shambani kwake kumshambulia kwa kumpiga mawe na kuanguka chini na kisha kumchoma mkuki na kumkata mapanga kichwani hali iliyosababisha kifo chake.

Chanzo cha mauaji hayo kimedaiwa kuwa ni mgogoro wa ardhi kati ya marehemu na washtakiwa hao.

Upande wa mashtaka ukiongozwa na Mwanasheria wa Serikali Temba ulileta mashahidi saba vikiwamo vielelezo na PF3, mganga aliyefanya uchunguzi wa mwili wa marehemu na upande wa utetezi ulileta mashahidi wanne.

Msajili wa Mhakama Kuu, Moshi alisema Mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka bila kuwapo shaka lolote.

Chanzo: Nipashe
 
Hawa watu wa hiyo kanda ni kweli wana ubabe ila mara nyingi huwa unawaponza mara nyingi wanakurupuka


Bora ndugu zao wanaouza mayai hapa jijini
 
Hiyo ndio faida ya kuchukua maamuzi huku ukiwa na hasira!

Mgombea hiyo ardhi mmoja kisha kufa kwa kuuawa na hao wawili Baba na mtoto wake wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa ila Ardhi inayo gombaniwa ipo pale pale na itaendelea kua pale pale.
 
Mwita Waitara alishika shilingi Jana pale Dom leo kaiachia kisa kilikuwa wajumbe 8 wa kamati kuishia ktk ofisi ya Rc na siyo kutembekea maeneo yenye migogoro hii injii hii
 
Back
Top Bottom