Muslim Hassanali asibezwe, amezichanga vizuri kuelekea 2020. Huyu hajanunuliwa bali amenunua!

Kuwa spika lazima uwe mbunge sasa huyu Zungu akistaafu atagombea vipi uspika?hapo mwandishi naona umechanganya madawa
Sio lazima uwe mbunge ili kugombea uspika. Mtanzania yoyote mwenye sifa ya kugombea ubunge ana sifa ya kugombea uspika.
 
Sasa hivi kuwa mpinzani ni fursa, mnaojiita wazalendo wa ccm mtasubili sana.From OPOSITION straight to Better Positon in CCM.
 
huwezi kununua kitu ambacho hakina thamani jamani. Hakuwa diwani wala mbunge so kwa nini umnunue? kila kitu kina thamani yake ila huyu alikuwa valueless
 
Ulizaliwa kutokana na kodom kupasuka ILA haikuwa mpango wa 'wafanyaji' kuzaa. una mawazo mgando sana. je walio CDM mbeya, mara, dsm, ar, iringa etc ni wachaga? acha mawazo ya kijinga yanayokufanya uonekane mpuuzi wa karne ya 13.
Hao walijiunga bila kujua ni Chama cha Wachagga
 
Kwanza kabisa nimeambiwa Muslim ndiye aliyefadhili kila kitu kuanzia ukumbi wa mkutano, press yenyewena posho zote za waliohudhuria. Amefanya hivyo kwa kusudi maalum kabisa. Anaelewa anachokifanya.

Hassanali anaelekea CCM huku kukiwa na uhakika kuwa Zungu hatogombea tena ubunge 2020 baada ya kuhakikishiwa kuwa atakikalia kile kiti cha mhimili uliomezwa ambao kila kwenye press ya ikulu lazima awepo mwenye mhimili. Hivyo Zungu anaenda kustaafu kugombea jimbo la Ilala.

Muslim Hassanali anaingia moja kwa moja kuwa mmoja wa wadhamini wapya wa CCM yeye hana mawaa hivyo JPM atamkubali kutokana na fikra zilizojengeka.Pia Hassanali hahitaji siasa za kiuana harakati ambazo zipo Chadema kwa wengi wao. Hahitaji kupigana kufa na kupona eti kuhusu katiba mpya? for what? Hahitaji kujua kama nchi ina udikteta? Ili afanye nini? Yule kwanza hana cha kufia!

Sasa Hassanali anahitaji kuwekeza, anahitaji pesa ili aendelee kutamalaki Kariakoo. Hahitaji kuwa kama kina Lissu, Mnyika, Bony, Lema na wengine. Haina maana kwake. Shida yake siyo siasa. Hivyo Chadema hapamfai katu.

Kwanza ni mtu wa kupongeza kuweza kudumu Chadema kwa muda wote huo. Labda alitegemea kuwa 2015 mambo yangeenda sawa. Akapoteza, amepima siasa za serikali hii ya awamu ya tano akaona kukaa upinzani kutahitaji nguvu na msuli kwelikweli kupata jimbo kama mbunge. Ameona nguvu zinavyowagharimu kina Lema, kina Lissu. Ameona jinsi wanavyoteseka. Sasa yeye Hassanali mabadiliko ya kimfumo sijui katiba wala hayamsaidii maana hana cha kufia. Ni sawa na Rostam Aziz eti leo umwambie aingie Chadema apiganie katiba mpya? Si utasubiri hadi Yesu arudi?

Kwa kweli na kwa dhati kabisa kumuweka Muslim ndani ya Chadema kwa sasa ni kumuonea,mwacheni aende akasake maslahi! Huyu hajanunuliwa bali amenunua! Wapo ambao wakihama wala huhitaji kutumia nguvu kujua kama wamenunuliwa ila siyo huyu.

Nenda Hassanali nenda kasake fursa! Frustrations za siasa waachie wengine wapambane wewe siyo wa aina hiyo!
Mkuu, Mgombea wetu wa Urais amekwenda IKULU kumpongeza RAIS kwamba anafanya kazi nzuri.
Una maoni gani kamanda?:D:D:D:D
 
Mkuu, Mgombea wetu wa Urais amekwenda IKULU kumpongeza RAIS kwamba anafanya kazi nzuri.
Una maoni gani kamanda?:D:D:D:D
Na rais wenu mpendwa anayechukia majizi na mafisadi asiyetaka hata yamsogelee leo kalialika hilohilo lijizi na lifisadi ikulu kisha akalisifia kuwa lilifanya mambo makubwa ndani ya nchi hii enzi za utumishi wake. Unaliongeleaje hili?
 
Na rais wenu mpendwa anayechukia majizi na mafisadi asiyetaka hata yamsogelee leo kalialika hilohilo lijizi na lifisadi ikulu kisha akalisifia kuwa lilifanya mambo makubwa ndani ya nchi hii enzi za utumishi wake. Unaliongeleaje hili?
Wakati linagombea Urais unakumbuka ulivyokuwa unajitahidi kulisafisha?
Mbona sasa unanilazimisha nianze ku-doubt kuhusu uwezo wako upstairs?
 
Wakati linagombea Urais unakumbuka ulivyokuwa unajitahidi kulisafisha?
Mbona sasa unanilazimisha nianze ku-doubt kuhusu uwezo wako upstairs?
Hujajibu swali langu kuhusu alichofanya rais wako anayechukia majizi na mafisadi
 
Back
Top Bottom