Habari wakuu,
Kuna wadogo zetu walimaliza kidato cha sita na matokeo yao yametoka karibuni, kwa sasa wapo kwenye mchakato wa kujaza vyuo na uchaguzi wa shahada watazochukua. Ni ngwe muhimu sana kwenye maisha yao, kwa sababu ndio itayochagua awe nani baadae kitaaluma.
Shahada gani na chuo gani anaweza kwenda ni changamoto nyingine hasa kipindi hiki ambacho ushindani umekuwa mkubwa hadi kwa kozi za sayansi kinyume sana na kipindi cha nyuma. Kwa sasa kuna changamoto kubwa ya watu kwenda kusoma vitu wasivyotarajia dakika za mwisho na wengine kuahirisha kabisa masomo mpaka mwaka unaofata.
Hapa jukwaani kuna wanavyuo wengi ambao kwa sasa wanasoma vyuo na shahada ambazo wengine wangependa kwenda, kuna wahitimu wa hivyo vyuo na wanajua mazingira ya vyuo husika pia changamoto gani wamezipata kwenye hivyo vyuo na kuelekea kwenye ajira kulingana na shahada walizosoma.
Kwa pamoja naamini tunaweza kuwapa mwanga hawa wadogo zetu wapunguze idadi ya makosa yanayotokana na kutokuwa na ufahamu. Kwa heshima ningependa kuwaita LORDVILLE LISANDIME tzhumoally CDG Marco Polo mchepukomatope Chungu cha bibi na wengine wote katika kufikisha lengo la mada hii.
Karibuni!
Kitabu cha Mwongozo wa Vyuo na kozi cha TCU 2015/16