Muongozo: Je Sensa kutojumuisha masuala ya dini ya mtu ni sahihi wadau mnalionaje hili?

Boligado

Member
Jan 10, 2012
44
49
Jana katikia taarifa iliyotolewa na kamishna wa sensa imetaja kwamba dini, kabila au mambo ya kisiasa ni mambo ambayo hayatakuwamo wakati wa sensa ya Mwaka huu. Napenda kupata ufahamu zaidi je ni sahihi? Nawasilisha.
 
dini, siasa na kabila ili iweje? Hii ni sensa ya kuhesabu watu na si sensa ya kuhesabu siasa, dini wala kabila
 
Sensa inaisaidia serikali kujua idadi ya watu wake ili iweze kupanga mipango inayoendana na idadi ya watu wake.

Tanzania haina dini,kabila wala siasa ila watu wake ndiyo wana dini,kabila na wanasiasa,kwa mantiki hiyo hakuna haja ya SENSA kuonyesha dini ,kabila wala usiasa wa mtu.

SASA KWA HILI NA IPONGEZA TIMU YA SENSA KUYAONDOA HAYA
 
Sensa inaisaidia serikali kujua idadi ya watu wake ili iweze kupanga mipango inayoendana na idadi ya watu wake.

Tanzania haina dini,kabila wala siasa ila watu wake ndiyo wana dini,kabila na wanasiasa,kwa mantiki hiyo hakuna haja ya SENSA kuonyesha dini ,kabila wala usiasa wa mtu.

SASA KWA HILI NAIPONGEZA TIMU YA SENSA KUYAONDOA HAYA
 
Kama serekali ina panga Mipango kwa kuangalia waruguru au wamakonde wangapi? au Wapagani wangapi, rastafari wangapi basi hapo ingekuwa na umuhimu. Vinginevyo haina umuhimu. Hongera Mtakwimu kwa kuliona hilo
 
Sawa ni kweli serikali haina dini lakini kwenye mambo mengi tunayojaza tukiomba birth certificate,udahili kwenye Elimu ya juu tunataja dini. Kwa mtazamo mpana dini ingehusishwa katika sensa ili maamuzi mengine kama kuweka baraza la mawaziri libalance dini ya waislamu na wakristo yasiyowepo Bali yaangalie waislamu ni wangapi wapate percent yao hivyo hivyo na wakristo. Maana huu unafiki kuna serikali haina dini halafu decision kwenye post nyingi zinategemea percentage ya 50/50.
Waweke item ya dini ya mtu ili rais awape vyeo wahusika kwa uwiano wa dini zao. Nawasilisha na niko tayari kukosolewa
 
How can we count emotions and feelings? We can't quantify everything!!!

Je unakubaliana nami mara nyingi mkulu huangalia mambo hayo anapofanya maamuzi ya kuteua wateule? Kama ni ndiyo kwa nini sensa ya 2012 isimpe majibu sahihi. Maana hata mawaziri wakiteuliwa vigezo huwa vimezingatiwa
 
Mi binafsi ningetamani kujua, ila kitaifa sioni maslahi yake, kwani wakiuliza mkristu, hilo jibu halina mshiko wowote zaidi ya umbea tu. Hawawezi kuitumia hii info kwa kitu chochote, labda mnifahamishe, mawaziri wachache sana wanatumia dini zao kufanya maamuzi hadi sasa.
 
Jana katikia taarifa iliyotolewa na kamishna wa sensa imetaja kwamba dini, kabila au mambo ya kisiasa ni mambo ambayo hayatakuwamo wakati wa sensa ya Mwaka huu. Napenda kupata ufahamu zaidi je ni sahihi? Nawasilisha.

Nina mashaka na uwezo wako wa akili, hivi unaweza ukawasilisha suala la kipuuzi kama hilo kwenye jamii.Dini na kabila lako sisi vina tuhusu nini.Nimekupa ban ya mwezi mmoja.
 
Sawa ni kweli serikali haina dini lakini kwenye mambo mengi tunayojaza tukiomba birth certificate,udahili kwenye Elimu ya juu tunataja dini. Kwa mtazamo mpana dini ingehusishwa katika sensa ili maamuzi mengine kama kuweka baraza la mawaziri libalance dini ya waislamu na wakristo yasiyowepo Bali yaangalie waislamu ni wangapi wapate percent yao hivyo hivyo na wakristo. Maana huu unafiki kuna serikali haina dini halafu decision kwenye post nyingi zinategemea percentage ya 50/50.
Waweke item ya dini ya mtu ili rais awape vyeo wahusika kwa uwiano wa dini zao. Nawasilisha na niko tayari kukosolewa

mimi bila kumungunya nakuunga mkono: hata na hiyo ya Kabila inabidi iwepo: hata kama lengo la sensa ni kujua Idadi ya watu ni sawa;
ila inabidi ni watu wa aina gani ni
- waislamu/wakristu!!!,
- wamakonde/wakurya....,!!!,
- wanawake/wanaume!!!,
- vijana /wazee!!!!
haya mambo ya kuwa tunajistukia kwamba mtu akiulizwa ni dini gani itaonekana ni kuendekeza udini au akiulizwa ni kabila gani ni kuendekeza ukabila ni upuuzi mtupu: baada ya sensa inatakiwa tu na taarifa zilizokamilika juu watu tulio nao nchini.
 
Nina mashaka na uwezo wako wa akili, hivi unaweza ukawasilisha suala la kipuuzi kama hilo kwenye jamii.Dini na kabila lako sisi vina tuhusu nini.Nimekupa ban ya mwezi mmoja.
Kaka dhihirisha uwezo wako kwa hoja si kwa style hii. Ondoa hofu ndiyo maana ukisoma encylopeadia itaonyesha percentage za watu wa nchi ikihusisha ethnity,dini zao n.k. sisi twapaswa tushinikize mambo haya yarudishwe. Tusije juta wakati ujao. Ukisema unaanzisha mahakama ya kadhi utajua unafanya kwa population kubwa kiasi gani?
 
Back
Top Bottom