Mungu ameumba!!!!

Meritta

JF-Expert Member
Apr 26, 2011
1,303
293
jamani mi ninachoamini ni kuwa Mungu kaumba vitu kwa mfano wake, pia kaumba vitu ili mwanadamu atumie na kufurahia.
ila katika suala zima la mapenz sijui nini kinatokea na ndo maana naomba msaada kwenu. Katika iman yangu mi naamin kuwa hata suala la mapenzi na ndoa mungu ameifanya na kuibariki ili watu wafuraie na kuzaliana waongezeke waijaze dunia. Tatizo linakuja ni pale mapenz
yanapokuwa chungu na kuharibu utaratibu mzima wa maisha, sasa wanajamvi tusaidiane nini tatizo linalopelekea mapenz kuwa si furaha tena
bali machungu. Nawasilisha
 
Usaliti
uaminifu kukosekana
tamaa
hali ngumu ya maisha n.k
 
Tatizo ni kuita uasherati/umalaya 'NGONO' ,kwa maana kwa Mungu iwe ngono,iwe ngomo,iwe ng'ono yote ni umalaya ama uasherati,lakini pia tumeelekezwa ni akina nani wafanye tendo la ndoa na si 'kufanya mapenzi' kama mnavyoita nyinyi siku hizi

Mungu anataja 'tendo la ndoa' kwa maana liwe ni tendo kwa wanandoa TU,sasa leo wakwale nao wanafanya hili tendo,ni sawa?mbali ya hivyo tumeambiwa hili tendo ni la siri,sasa leo ni wapi kuna siri?make watu mna...kama mbwa nje nje

sasa kama mnaamua kuliita tendo LA NDOA ni kufanya MAPENZI tayari hilo ni kosa kubwa sana,kwa maana tumelitia najisi

Nionavyo mimi!
 
Ni kweli Mungu alimuumba mke na mme na akawafungia ndoa pale Bustanini mwa Eden na akaibariki ndoa na akaitakasa
Ndoa ni takatifu na imeletwa ili watu waweze kuifurahia na kuishi kwa amani ila baada ya anguko la mwanadamu dhambini
ndo chanzo cha haya yanayotokea leo
kumekuwa na kutokuwa waaminifu
tamaa
ukatili
usaliti
uongo nk
Na pia kufuata tamaa za miili yetu unakutana na mtu unampendea maybe sura umbo kazi mwonekano ila tabia hatuangalii tunataka material thing
UKIMSHIRIKISHA MUNGU WAKATI WA KUMTAFUTA MWENZA WAKO HUTAJUTIA KUOA AU KUOLEWA ILA SISI WALA TUNAINGIA TUU BILA HATA KUFUNGA NA KUSALI HUKU TUKIOMBA MWONGOZO WA ROHO MTAKATIFU
 
hutakiwi kufanya tendo la ndoa kama huajoa/lewa, na hutakiwi kufanya nje ya ndoa. kinyume cha hapo, ndio chanzo cha matatizo unayoyazungumza.
 
Ni kweli Mungu alimuumba mke na mme na akawafungia ndoa pale Bustanini mwa Eden na akaibariki ndoa na akaitakasa
Ndoa ni takatifu na imeletwa ili watu waweze kuifurahia na kuishi kwa amani ila baada ya anguko la mwanadamu dhambini
ndo chanzo cha haya yanayotokea leo
kumekuwa na kutokuwa waaminifu
tamaa
ukatili
usaliti
uongo nk
Na pia kufuata tamaa za miili yetu unakutana na mtu unampendea maybe sura umbo kazi mwonekano ila tabia hatuangalii tunataka material thing
UKIMSHIRIKISHA MUNGU WAKATI WA KUMTAFUTA MWENZA WAKO HUTAJUTIA KUOA AU KUOLEWA ILA SISI WALA TUNAINGIA TUU BILA HATA KUFUNGA NA KUSALI HUKU TUKIOMBA MWONGOZO WA ROHO MTAKATIFU
hili suala la kumshirikisha mungu ss wanadamu tunaona ushamba,ndo maana tunalia na mapenz
 
Tatizo ni kuita uasherati/umalaya 'NGONO' ,kwa maana kwa Mungu iwe ngono,iwe ngomo,iwe ng'ono yote ni umalaya ama uasherati,lakini pia tumeelekezwa ni akina nani wafanye tendo la ndoa na si 'kufanya mapenzi' kama mnavyoita nyinyi siku hizi

Mungu anataja 'tendo la ndoa' kwa maana liwe ni tendo kwa wanandoa TU,sasa leo wakwale nao wanafanya hili tendo,ni sawa?mbali ya hivyo tumeambiwa hili tendo ni la siri,sasa leo ni wapi kuna siri?make watu mna...kama mbwa nje nje

sasa kama mnaamua kuliita tendo LA NDOA ni kufanya MAPENZI tayari hilo ni kosa kubwa sana,kwa maana tumelitia najisi

Nionavyo mimi!
Ni kweli ndugu yangu maana sisi tumeyageuza mambo yote ya mchana tunafanya usiku na ya usiku tunafanya mchana
 
Tunamshirikisha Mungu kwa kuomba hivi "ninaomba unibadirishie huyu awe kama upendavyo" tayari mshaingia ktk mahusiano hapo,
 
100 thanks
u hv spoken ma mind, be blessed.
Usipokuwa na hofu ya Mungu kila chafu utafanya
Na asilimia kubwa a wanadamu wanajiamulia mambo yao bila Mungu ndio maana yanakwenda kombo
 
hiv kwa maisha ya vijana hili linawezekana kweli

Nini kilichopelekea vijana wa siku hizi wasiweze??

Kwa sasa hivi tumeamua kubadilisha mambo na kuwa kinyume chake.. Sasa hivi mtu anasifiwa kwa idadi ya wanaume au wanawake aliolala nao.

watu wanatoa sababu za tamaa, tabia, n.k

lakini ni nani ambaye hana tamaa; ni nani anayependa kuona au kuolewa na mwenye tabia mbaya?

Ninachokiona mimi ni kuwa

1.kwa sasa, kadiri siku zinavyokwenda ndoa inazidi kuwa ni gharama, nikimaanisha kwamba mchakato mzima wa kuoa umekuwa ni mgumu kutokana na masharti kama vile mahari, na gharama nyingine za harusi.
Hiyo inapelekea wengi watafute njia mbadala - (yaani kupunguza hamu tu )

2.elimu na uelewa umekuwa mwingi, sana sana kwa upande wa wanawake ambao sasa wamekuwa makini kutokuingia ndoa kichwa kichwa.
3.utandawazi pia umechangia kwa namna fulani; kwani kila mtu anataka "kujaribu" kile anachokiona au kusikia aone kuna nini

4. Kwa sasa mafundisho kutoka kwa mabibi na mababu hayapo tena. Pia mafundisho ya dini mbali mbali hayajatiliwa msisitizo na wafundishaji -

Pia kwa maisha ya sasa wengi tumeacha mahudhurio kwenye nyumba za ibada, kwa hiyo hakuna tena hofu ya Mungu - ya kusubiri ndoa.
 
Tunamshirikisha Mungu kwa kuomba hivi "ninaomba unibadirishie huyu awe kama upendavyo" tayari mshaingia ktk mahusiano hapo,
Hapo ndo tunapo kosea sasa sisi tunakutana na mtu mnaingia kwenye uhusiano ukiona anaenda sivyo ndivyo unaanza kumwomba Mungu ambadilishe ila tungemshirikisha kwanzia mwanzo tusingekuwa na shida
 
Uwe umeoa, au haujaoa, uwe na mpenzi au rafiki......Tatizo kubwa ni ubinafsi.. Selfishness.. ubinafsi.. either kwa mwanume au kwa mwanamke unakufanya usahau ahadi zetu, Pepo la ubinafsi likikuingia linakufanya upate tamaa, udanganye, utafute nyumba ndogo, n.k. Hivyo vingine vyote ni matokeo au outcomes ubinafsi wetu....Ukiweza kushinda ubinafsi..utamfikiria mwenzako, utahisi machungu yake, utathamini mchango wake, utajiweka nyuma badala ya kimbelembele..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom