Mungu ameniponya ajali hii mbaya!!

asanteni sana kwa pole zenu,ni kuwa lorry mbovu ya container ilikosa uelekeo ikanivaa upande wangu,ilikuwa ni karibu mno hivyo kujinusuru nikakwepeshea kulia
ajali ilitokeaa Mbozi Road chang'ombe na hizo picha hazikupigwa eneo la tukio bakli ni wakati scraper hiyo imepelekwa garage..

Mkuu pole sana na shukrani nyingi zimwendee Mungu Mwenyezi.
Walimu wangu wa dini wamenifundisha kuwa Mungu anafanya mambo yasiyowezekana ili kupitia hayo tuweze kumpa yeye utukufu.Endelea kuwakumbusha watu wampende sana Mungu kwani ndiye muweza yote.
 
Pole my dear teacher,nashukuru umepona,ningepata wapi mwalimu mwingine mie???
Mshukuru sana Mungu.......:clap2:
 
Pole sana mkuu. Tunamshukuru Mungu wetu Aliye Hai kwa kukutoa salama kwenye ajali hiyo. Ni Yeye pekee Anayestahili kupewa sifa na shukrani. Ubarikiwe!
 
Pole sana mkuu dah nimechelewa sana kuona hiii thread pole zangu zikufikie popote pale ulipo
 
Mshukuru Mungu ndg yangu tena katoe sadaka unaposali whether ni kanisani au msikitini, pole na hongera
 
Mungu anaweza, huwa anafanya mambo makuu ili wanadamu tuzidi kumwamini na kutambua ukuu wake, jina la bwana libarikiwe
 
Hakika nimefarijika sana na mioyo yenu ya huruma na maneno mema ya faraja,hakika waote mlionipa pole na kunitia moyo sina namna zaidi ya kuwashukuru nawashukuru pia waliorudisha ki-senksi maana kimenifanya nipate kazi rahisi ya ya kuwashukuruni nyote na kwa niaba ya ambao kwa sababu moja ama nyingine hawajapata nafasi kupitia thread hii
Namshukuru mola wangu kwa kunijaalia uzima na nawapenda nyote
God Bless u all!!
 
Nimechelewa kuona hii. Pokea pole yangu mkuu. Tunatakiwa kushukuru kwa kila jambo. Mshukuru mungu.
 
Pole sana Inkoskazi, ni kawaida kwamba inapotokea ajali ya barabarani huwa inakuwa imesababishwa mara nyingi na makosa ya dereva mmoja, kwa hiyo humu barabarani huwa tunasalimika kwa uwezo wa Mungu, unaweza kuwa makini sana lakini akatokea mzushi akakuletea, kwa hiyo hili ni jambo la kushukuru sana,

'kesheni mkiomba maana hamjui siku wala saa'
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom