Mume au mke wa mtandaoni

Kukutania mtandaoni hakuna tofauti na kukutania sehemu ingine yoyote ile. Na kanuni za mahusiano hazibadiliki kwani hata ukikutana na mtu shuleni, gengeni, kwa fundi, na kwingineko, umuhimu wa kwenda/kufanya mambo taratibu unabaki palepale. Chukua muda wako kumjua huyo mtu (ingwa huwezi kujua kila kitu) bila kukurupuka (rush).

Kwa hiyo, kwa vile mtandao umebadilisha mambo mengi ya kimaisha, ndoa za watu waliokutania kwenye mtandao nazo zinaanza kuwa ni kitu cha kawaida sana.
 
Jamani naomba ushauri,Je kuna mtu kashawahi kuolewa au kuoa mtu kutoka kwenye mitandao ya marafiki kama Twitter, face book n.k?
Nimeona kabisaaaaaaaa tena jamaa walikutana chat room! Hahaha na kwasasa wana watoto wa 3...maish yanasonga!:smiling:
 
Jamani naomba ushauri,Je kuna mtu kashawahi kuolewa au kuoa mtu kutoka kwenye mitandao ya marafiki kama Twitter, face book n.k?

hamna cha ajabu hapo...wengi tu wamekutana mitandaoni wakajenga mahusiano hadi ndoa na wengine ndoa zao zinadunda tu..... mtandaoni unakutana na aina zote za binadamu kama mitaani tu......
achana na STEREOTYPES......kuwa makini tu kama inavyotakiwa wakati wa kuchagua mke mtarajiwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom