Mume amchoma mke na mtoto kwa petroli

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,510
9,299
Mke asimulia jinsi mumewe alivyofanya unyama kwa kuwalipua na mafuta ya petroli akiwa na mtoto
Mke asimulia jinsi mumewe alivyofanya unyama kwa kuwalipua na mafuta ya petroli akiwa na mtoto

Mkazi wa kijiji cha Mlazo, wilaya ya Chamwino, Mkami Mbarahi (19) na mwanaye wenye umri wa miezi mitatu wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma baada kujeruhiwa kwa moto na mumewe, kwenye maeneo mbalimbali ya mwili.

Tukio hilo lilitokea Juni, 28 mwaka huu kijijini hapo, ambapo mumewe anayejulikana kwa jina la Elias Warioba anadaiwa kumrushia chupa yenye mafuta ya petroli mkewe akiwa na mtoto mgongoni wakati akipika chakula cha usiku.

Akizungumza akiwa wodi namba 16 katika Hospitali hiyo, Mkami amesema mumewe alimpiga na chupa ya plastiki ambayo ilikuwa na mafuta ya petroli kichwani wakati akipika.

Akisimulia mkasa huo, Mama huyo amesema akiwa jikoni akiandaa chakula cha usiku huku akiwa amembeba mwanaye mgongoni alifika mume wake akiwa na chupa hiyo huku akihoji kwanini anapikia kuni.

“Aliniuliza kwa nini ninapikia kuni na je nikiunguza kibanda cha watu?nilimjibu kwani mimi sina akili mpaka niunguze. Baada ya majibu yangu alinirushia chupa yenye mafuta ambayo ilifunguka na kunimwagikia mimi na mtoto, moto ukatulipukia,”amesema.

Amefafanua kuwa baada ya hali hiyo alikimbia nje akiwa na mtoto akipiga kelele kuomba msaada kwa majirani huku mumewe akiondoka bila kutoa msaada wowote.

“Nimeungua maeneo ya kichwa hadi kifuani na mwanangu ameungua maeneo ya usoni, mikononi, tumboni na miguuni,”amesema.

Kamanda wa polisi mkoani Dodoma, Gilles muroto amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa anashikiliwa na polisi kwa mahojiano.
 
Pole kwa mama na mtoto, lakini huyo mwanamke hakumjibu vizuri kabisa mumewe. Kama jamaa alikuwa na mtu wa hasira za karibu ndio balaa hilo sasa.
 
Hakujibiwa vizur kivipi?..... Ngoja akakutane na Sheria imujibu vizuri
wewe mtu anakuuliza unamwambia ;;unaona mimi sina akili unaona ni sawa? anayway jamaa hakufikiria cha kufanya amefanya kitu cha kipumbavu ila wanawake kuna muda huwa wanajisahau na kujibu lolote linalokuja mdomoni....me kila silku nasema kama huwezi kujiheshimu kwanza wewe mwnyewe usio wala kuolewa maana ndio marokeo yake menyewe,,,afu mtu mwenyewe bado ana miaka 19 huyo mdada kwa hiyo kiburi kipo on top
 
Weeeh Wariba weeeh jela hiyo inakuita na lazima uende tuu huna namna mtani.
Mama na motto poleni sana ila kadabu kidogo ni muhimu ili kuepusha mengi.
 
Pole kwa mama na mtoto, lakini huyo mwanamke hakumjibu vizuri kabisa mumewe. Kama jamaa alikuwa na mtu wa hasira za karibu ndio balaa hilo sasa.
Majibu kama hayo kwa watu toka Kanda Maalum huwa chanzo cha mizozo katika familia. Ila mama mwenyewe katoka huko huko, sasa sijui alijisahau au ndo kafika Mjini?
 
Inaonekana chokochoko za muungano zipo nyingi sana ndani ya hiyo nyumba na huyo mke ni mhanga wa domestic violence kitambo.

Q&A
 
Imani imetoweka. Na hassa makurya wengiwao makatili sana hayana ubinadamu. Hawa dawa yao boko haram wachinjwe mammae.
 
Back
Top Bottom