Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,331
- 33,147
INNOCENT NGARULA [40] amejikuta akidhlilishwa na mke wake usiku wa kuamkia jana baada ya mke huyo kuamua kutoa siri ya malumbano kati yao na kubainisha mume wake alikuwa akihitaji kumuingilia kinyume na maumbile. |
Mwanaume huyo alikuwa akimsumbua mke wake huyo aliyetambulika kwa jina moja la Jojina [23] kufanya naye mapenzi kinyume na maumbile huku Jojina akipinga kitendo hicho na kutoa ahadi hewa kwa mumewe. Jojina amedai kuwa mume huyo alikuwa akimsumbua sana hali iliyopelekea na awe anamuongopea na kumpa kalenda kila siku. Siku hiyo mume wake huyo alichoshwa na kalenda hizo na mkewe na ndipo ugomvi ulianza kati yao na kupelekea mwanamke huyo kutakiwa kuondoka. Innocent aliuchukua uamuzi wa kumfukuza mkewe huyo usiku majira ya saa 5 usiku lakini Jojina aligoma kuondoka na ndipo alianza kushushiwa kichapo na mumewe. Kelele za kuomba msaada za Jojina ziliwaamusha baadhi ya wapangaji wa nyumba hiypo kuamua kumuuliza Jojina nini kimemsibu. Jojina alikuwa akishinikizwa na mume wake aondoke na baadhi ya majirani waliamua kumuuliza mumewe ni kwanini alikuwa akimfukuza mkewe usiku huo na kutoa sababu kuwa mwanamke huyo alikuwa ni jeuri na alichukua fedha bila idhini yake. Hata hivyo baba mwenye nyumba huyo alimsihi mume huyo amvumilie mke mke wake hadi asubuhi ndipo aondoke kwa kuwa ule ulikuwa usiku. Lakini Innocent hakuhitaji ushauri huo na alianza kumshambulia kwa makofi Jojina akimtaka aondoke na ndipo Jojina alipoamua kutoa siri hiyo kwa wanawake wenzake mbele ya mwenye nyumba na mwanamume huyo kupatwa na aibu kubwa. Baada ya mwanamke huyo kutoa siri hiyo mwanaume huyo kwa jazba alitaka kuendeleza kipigo na watu kumsaidia mwanamke huyo kumsitiri ili kukicha ajue ustarabu wa kufanya. Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana huko maeneno ya Kigogo jijini Dar es Salaam. chanzo Mume Alazimisha Kumlawiti Mkewe, Apata Aibu Kubwa |