Multichoice (Dstv) na Zuku hatarini kunyang'anywa leseni za kurusha matangazo Tanzania kwa kukaidi Agizo la TCRA la kutoonyesha televisheni za ndani

Kwa utaratibu mbovu na kanuni mbovu, TCRA ina leseni za ain mbili. Aina ya kwanza ni leseni ya local itakayokuwa na Free to Air channels (channel zitakazorushwa bure bila kulipia) ambazo ni ITV, TBC1, Channel 10, Clouds TV, Star Tv na EATV.
Hiz FTA channel ni decorder tatu tu zenye leseni au mamlaka ya kuonyesaha ambazo ni Star timws, Continental na TING. Ving'amuz vyote vilivyobaki kuanzia Azam Tv, DStv, Digitek n.k hazitakiwi kuonyesha hizo channel si bure wala kwa kulipia (wana leswni ya kuonyesha TBC2 tuu)
Hapo ndipo kwny shidaaaa...
Hivyo ving'amuz vyenye FTA (free to air) channel havionyeshi bure hizo channel (kifurush kikiisha hazionekani) na hizo zisizokuwa na lesen ya kuonyesha FTA (DStv, Azam TV etc) nao wanazionyesha hizo channel tena kwa kulipia..
Hapo ni mkanganyiko mtupu, ss tcra wamewavalia njuga hawa wasio na fta, wamewaacha wenye lesen ya fta lakn hawaonyeshi bure kwa wananchi. Kaupendeleo flan hv kwasababu wote ni watoto wa baba mmoja (star times vs tcra).
Hope umenipata kidogo mkuu..[/QUOT

Nashukuru sana Mkuu!
Umenitoa kwenye mkanganyiko.
Kwa hiyo sasa tukitaka kuona local channels tukanunue StarTimes au Ting au Continental.
Duh! Walikuwa wapi siku zote hizi.
Watatucompansate hizo damage?
 
Nashukuru sana Mkuu!
Umenitoa kwenye mkanganyiko.
Kwa hiyo sasa tukitaka kuona local channels tukanunue StarTimes au Ting au Continental.
Duh! Walikuwa wapi siku zote hizi.
Watatucompansate hizo damage?

Kwasasa ukitaka kuona local channels ambazo ni FTA ni lazima uwe na moja kati ya hivyo ving'amuz vitatu. Na kwa jinsi hivyo ving'amuz vitatu vilovyo vya hovyo, itakulazimu tu uwe na ving'amuz viwili kimoja chenye FTA channel (coz wengi ni wapenz wa taarifa ya habar ya itv na vipind vyao) na kingine chenye ubora kisicho na FTA channel (aidha Azam Tv, DStv nk).
Ni ukiritimba flan hv umewekwa na hawa tcra wasiojielewa. Kwny hili tcra wamekuwa kama BASATA vile kufanya kaz kwa kujipendekeza pasipo kuangalia pande zote.
Sasa swali linakuja hiv, kwa watanzia tunavtopenda dezo hv ni nani ataenda kulipia star times kila mwez wakat FTA anazion bure, jibu ni kwamba hawa Ting, Star times na Continental watakosa kabisa malipo ya kila mwezi. Sasa wao watapata wapi hela za kujiendesha?? Channel zao wenyewe hazina uwezo wa kuvutia matangazo wakapata hela, ss watajiendeshaje km hizo FTA channel zinaonyeshwa bure na matangazo ya kwenye hizo fta channel yanalipwa kwa wamiliki wa hizo fta (mfn Biko anawalipa ITV hawalipi wenye king'amiz cha TING)???
Hapa ndipo mgogoro mkubwa unakuja kat ya wamilik wa ving'amuz na wamilik wa hiz fta channels. Wamilik wa ving'amuz wanataka kuwaminya wenye fta channel (itv etc) wawalipe kiasi kikubwa mpk tone la mwisho kwa wao kuwapa coverage bure, kitu ambacho si sahihi. Sasa ni inawezekana wenye ving'amuz ss hv hawalipwi ndio mana wanazifunga fta zisionekane mpk mteja afanye malipo ya mwezi.

Huu ni ukiritimba wa kizamani sana waliouweka tcra. Wenye ving'amuz na wenye channel (ITV) na channel zingine walitakiwa wawe huru kuingia mikataba baina yao na wakubaliane malipo na sio kuwalazimisha kuweka utaratibu wa fta channel tena ziwe kwny ving'amuz vitatu tu. Kitendo cha ITV, clouds, star tv na zingine kutoonekana kwny ving'amuz vya Azam na DStv kutawaumbisha kibiashara mana itashusha thaman na idadi ya matangazo yao kwani coverage zao zitakuwa zimepungua (ni obvious Azam na DStv wana coverage kubwa sana kuliko hao wazembe wa star times, ting na continental ambao mi naona wako kiprimitive sana). Kuziondoa DStv ni kuziondoa local channel zetu kwnye jukwaa la kimataifa, huku ni kuua juhud zao za kujitanua kimataifa ambapo kuna fulsa nyingi sana.

Nawakumbusha tu TCRA (kwny hili wameazima akili za BASATA), HAKUNA BURE DUNIANI.
 
MASWALI 4 KWA TCRA KUZUIA URUSHWAJI WA CHANELI ZA UMmA​
Hivi karibuni, Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekuwa kwa nyakati tofauti ilitoa nyaraka za nia ya kutengua leseni za baadhi ya watoa huduma za matangazo ya televisheni kama vile Startimes, DStv na ZUKU
Kwa uelewa wangu mdogo binafsi nimejikuta nikijiuliza maswali mengi sana hususan baada ya kusoma nyaraka hizo. Maswali hayo pia nimeyaona yakiulizwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii. Bila shaka hili ni suala pana zaidi kwani linawagusa moja kwa moja wananchi wengi.
Pamoja na maswali hayo mengi, mimi nina maswali matano tu kwa TCRA:
Je, wanachokifanya TCRA ni kuwapa watu au kuwanyima haki ya kufikiwa na mawasiliano?
Je, TCRA ni dhaifu katika kutekeleza majukumu yake?
Je huu ni utashi wa TCRA ama kuna mkono wa mtu?
Je TCRA inafahamu madhara ya maamuzi yake katika sekta ya Biashara na uchumi wa nchi?
Napenda niyachambue maswali haya matono kwa kina ili sisi wazalendo na walipa kodi wa nchi hii tuyaelewe bayana;
Haki ya kupata Habari
Haki ya uhuru wa kutoa maoni inalindwa na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 18 inayomhakikishia kila raia haki ya kupata habari, kutoa habari na kutoa maoni yake ilimradi tu havunji sheria
Sehemu ya 13 ya mkataba wa kimataifa wa haki ya mawasiliano (Universal Communications Service Access - UCSA Act 2006) inabainisha matakwa ya msingi ya huduma zinazotolewa na warusha matangazo ambapo pamoja na mambo mengine, wanatakiwa kuhakikisha kuwa huduma za matangazo ya msingi zinayotolewa na zinapaswa zipatikane kwa urahisi kwa watu wote kote nchini kwa usawa popote wanapoishi au kufanua shughuli zao.
Wakati nchi yetu ilipoamua kuhama kutoka kwenye mfumo wa analojia kwenda mfumo wa digitali, serikali, kwa nia njema kabisa iliweka mkakati wa kuhakikisha kuwa wananchi hawanyimwi haki yao ya msingi ya kupata habari na mawasiliano. Katika kufanikisha zoezi hili, ilitoa leseni za (Network Facility License – NFL) utangazaji kwa kampuni tatu – Star Media, BTL na AGAPE na kuwapa jukumu la kuweka mfumo utakaowawezesha wananchi kupata huduma za mawasiliano hususan matangazo ya televisheni popote walipo.
Kwa nia njema kabisa, serikali iliamua kutoa ruzuku kwa kampuni hizi kwa lengo la kuhakikisha kuwa ndani ya muda ziwe zimekamilisha uwekaji wa miundombinu itakayowawezesha watanzania popote walipo kupata huduma za mawasiliano bila kikwazo.
Zaidi ya hayo, kwa nia hiyo hiyo njema, serikali iliidhinisha mkataba wa TBC na Star Media kwa madhumuni hayo hayo ya kufikisha huduma za habari kwa wananchi tena kwa gharama nafuu.
Ikiwa kuna kampuni zilipewa hela za watanzania maskini walipa kodi, ili ziwapelekee mawasiliano, na kwakuwa baada ya muda ambao walipaswa kutekeleza hilo wameshindwa, Je ni kwanini TCRA leo hii inazinduka na kutaka makampuni ya setelait yasitishe kuonyesha chaneli za umma na kuwaachia wale ambao walitumia hela za walipa kodi na bado hawajawafikishia huduma hiyo?
TCRA watueleze, serikali ilitoa ruzuku ya shilingi ngapi kwa kampuni husika? Na hizo fedha za walipa kodi wamezipeleka wapi?
TCRA watueleze, walikubaliana zoezi hilo lichukue miaka mingapi? Na je makampuni hayo yametekeleza?? Kama yametekeleza, iweje leo bado kuna maeneo hawawezi kupata huduma hizo? Hii TCRA ni kwa maslahi ya nani? Ya uma au ya wajanga wachache wanaokula kuku kwa mrija kwa kutumia hela za walipa kodi wavuja jasho wa nchi hii?
Ni kina nani hao ndani ya TCRA wako nyuma ya hili pazia? Na wanafanya haya kwa maslahi ya nani??? Kwa mtazamo wangu, hapa maslahi ya wananchi yamewekwa kando na badala yake kuna maslahi binafsi.
Ifahamike kuwa chaneli za umma zimekuwa na mchango mkubwa sana kwa maisha ya kila siku ya wananchi. Katika nchi zinazoendelea kama Tanzania, chaneli za umma zimekuwa nguzo muhimu sana katika kutoa habari, elimu, burudani, utamaduni na Zaidi ya yote kuijenga na kuimarisha ushirikiano kati ya wananchi
Udhaifu wa TCRA katika kutekeleza majukumu yake;
Kwa mtazamo wa TCRA, zuio hili la kuonyesha chaneli za uma kwa baadhi ya watangazaji ni kwa mujibu wa sheria. Sheria husika ni sheria yenye mapungufu makubwa ya mwasasiliano yaelekroniki na posta (Electronic and postal Communications Act)
Kwanza ili kuonyesha kuwa hata hao TCRA wenyewe waliona madhaifu katika sheria hiyo, kwa mara kadhaa wamekuwa wakiwashurutisha watangazaji (DTH) kurusha matangazo ya FTA bila malipo kwa wateja. Mbali na uwepo wa sheria husika, TCRA wakati huo iliona sheria hiyo haifai na haina maslahi kwa uma hivyo ikawa inawasisitiza DTH kurusha chaneli hizo bila kuwalipisha wananchi.
Kwa mujibu wa Jamii forum – Juni 11, 2013, sehemu ya taarifa ya Statimes ilinukuliwa “…tulijaribu kuwasiliana na TCRA ambao waliamuru chanel zote za nyumbani zipatikane katika ving’amuzi vyote bila malipo…”
Baada ya muda, TCRA haohao wakabadili gia angani, wakawataka DTH waache kuonyesha chaneli za FTA. Swali hapa ni Je, kama kweli TCRA wanasimamia sheria, na wanaamini kuwa sheria hiyo ni nzuri, kwanini wamekuwa wakitoa maelekezo kinzani ka watangazaji wa DTH?
Kama hiyo haitoshi, mara TCRA hao hao, mwaka 2017, wakaja na rasimu ya kubadili kanuni za sheria ya mwasasiliano ya elekroniki na posta .
Kifungu cha 8 cha rasimu hiyo kilidhamiria kuzuia kurushwa kwa chaneli za FTA katika DTH.
Kifungu hicho kinasema (kwa tafsiri ya kawaida) "Mtoa huduma anayetaka kutoa huduma ya kurusha matangazo ya moja kwa moja ya setelaiti (Direct To Home - DTH) hapaswi kurusha matangazo ya chaneli za FTA katika vifurushi vyake.". swali hapa ni je, kama sheria hiyo ilikuwa inajitosheleza, ni kwanini TCRA walikuja na rasimu hii ya marekebisho na kusisitizia kipengele hicho kwa nguvu kubwa?
Wakati huo huo, TCRA ilitoa waraka kwa waendeshaji wa DTH ikimanisha (Azam, DStv, Wananchi - ZUKU) kuwaelekeza kuacha kurusha matangazo ya chanel za FTA katika mifumo yao. Waraka kama huo pia ulitumwa kwa chaneli za FTA
Pamoja na kujikanganya huko, nilishangaa sana nilipoona kampuni moja ambayo TCRA ilitangaza nia ya kufuta leseni yake, ikatoa taarifa kuwa suala hilo lipo katika Mahakama ya Usuluhishi wa Kibiashara (Fair Competition Tribunal). Hivi kweli TCRA hawajui kuwa kama suala lipo mahakamani inabidi uamuzi wa mahakama usubiriwe kwanza ndiyo hatua zichukuliwe? Huu ni udhaifu mkubwa na wa kutia shaka. Sisi wananchi tunatarajia taasisi kubwa kama TCRA ziwe mfano wa kuigwa katika kuheshimu sheria na taratibu. Badala yake wanakuwa wa kwanza kuzikengeuka. Hili ni la bahati mbaya kweli au kuna mkono wa mtu??
Je, huu ni utashi wa TCRA?
Nimetathmini matukio ya siku chache hizi, nikahisi kabisa hapa si bure. Nadhani kuna kitu kikubwa kinaendelea. Ni wiki moja tu imepita tangu TCRA watoe tishio la kufuta leseni ya Star Media kwa madai ya kushindwa kurusha bure channel za FTA!. Hivi, hawa Star Media si ndio waliopewa mabilioni ya walipa kodi ili iweze kuweka mfumo wa mawasiliano nchi nzima? TCRA watuambie kwanza, Je Star Media walipewa ruzuku ya shilingi ngapi? Na kwa ajili gani? Na walipaswa kutekeleza hilo kwa muda gani?
TCRA watujuze sie walipakodi, je hela zetu walizopewa Star Media, wamezipeleka wapi?kwanini hadi hii leo kuna maeneo hayawezi kupata huduma za matangazo ya DTT?
TCRA watuambie, ni kwanini muda wote huo Star Media walikuwa wanawalipisha wateja kulhali walipewa ruzuku ya serikali kwa ajili ya kusambaza mtandao nchi nzima?
TCRA watuambie kuhusu ving’amuzi vya teknolojia ya T1 vilivyosambazwa na Star Times, Je ni kweli TCRA walibariki Tanzania kuwa dampo la teknolojia iliopitwa na wakati? Walifanya hivyo kwa maslahi ya nani?
Baada ya miaka nenda rudi, hivi majuzi Star Media wamekuja na mchapo mpya wa kitapeli. Katika tangazo lao kwenye vyombo vya habari mapema mwezi huu wa Agosti, wamesema kuwa kuna ving’amuzi vya aina mbili. Vile ambavyo vina chanel za bure, na vyenye chanel za kulipia. Lakini ujanja waliofanya, vya chanel za kulipia vinauzwa bei chee, vya chanel za bure bei maradufu… sasa hawa si ndio wale wale walipewa ruzuku na serikali? Tena leo hii waje kuuza ving’amuzi vya FTA kwa bei ya dhahabu? Na TCRA imekaa kimya inawatazama tu…. Hii ni kwa maslahi ya nai??
Namshukuru sana rais wangu. Hivi majuzi aliwatolea uvivu kuhusu ndoa yao na TBC. Watu gani wanafanya biashara eti miaka nenda rudi hawatengenizi faida? Lakini wakati huo huo hawafungi biashara?? Je hii inaingia akilini??
Maadhara ya maamuzi ya TCRA kwa Biashara, Uwekezaji na Uchumi kwa ujumla
Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi sana tangu nilipoanza kuliona sakata hili wiki chache zilizopita. Lakini kilichonishangaza zaidi ni pale niliposoma kuwa eti suala la TCRA imetishia kufuta leseni wakati shauri lipo kwenye makakama ya usuluhishi wa kibiashara likisubiri maamuzi. Hili ni suala la kutia wasiwasi na mashaka makubwa.
Mimi binafsi sipingani na TCRA, ikiwa wanasimamia sheria,. Lakina katika kila soko, na kila nchi kote ulimwnguni, kuna mamlaka za udhibiti – kama ilivyo TCRA, EWURA, SUMATRA na kadhalika. Lakini pia, kwa hali halisi ya biashara, kutokea kwa kutoelewana kati ya pande moja na nyingine – iwe ni kati ya kampuni na kampuni, au kampuni na mamalaka ya udhibiti, ni vitu vya kawaida kabisa. Kwa msingi huo ndiyo sababu kote duniani kuna mamlaka za usuluhidhi. Kwa Bahati nzuri sana sisi hapa tanzania kwenye masuala ya biashara na uwekezaji kuna tume ya Ushindani huru wa Kibiashara (Fair Competition Commission) na pia kuna Mahakama ya Ushindani wa Kibiashara (Fair Competition Tribunal). Hizi ni mamlaka zilizoundwa kwa mujibu wa sheria
Nimeshangaa sana kuona kuwa TCRA inadharau uwepo wa taasisi hizo na diyo maana wanaweza kutoa waraka wa nia ya kufuta leseni wakati shauri hilo lipo katika mahakama ya usuluhishi wa kibiashara. Hili linatia shaka na kupunguza uaminifu kwa TCRA.
Tabia kama hizi kwa mamlaka zetu za udhibiti ni kitisho kikubwa kwa uwekezaji wa ndani nan je na ni saratani ya ukuaji wa uchumi wa nchi. Hili si suala la kufumbiwa macho hata kidogo. Katika zama hizi za kujenga tanzania ya viwanda, vikwazo kama hivi ni sharti viondolewe. Kama kuna sharia zenye walakini zibadilishwe! Lakini zibadilishew kwa manufaa ya wananchi walio wengi.
Nilipata Bahati ya kuona rasimu ya TCRA ambayo nadhani ilikwama. Kilichonishangaza zaidi, ni pale nilipoona nia ya TCRA ya kutaka pia iwe inafanya usuluhishi! Huenda nsiyo sababu hata inadharau Mahakam ya Usuluhishi wa Kibiachara kwa kutoa matamko wakati shauri lipo mahakamani.
Lakini kwanini TCRA inataka iwe kila kitu? Iwe Kepteni wa timu, Refa, na Kamisaa wa mchezo kwa wakati mmoja. Hii inawezekanaje???
Ninaamini kuwa TCRA italitafakari tena suala hili kwa kina na kukaa meza moja na wadau na kuangalia njia bora ya kulitatua badala tu ya kutishia au kutengua leseni za watangazaji. Hivi leseni ya Azam, au Zuku, au DStv ikitenguliwa ni watanzania wangapi watakosa ajira? Serikali itakosa mapato kiasi gani? Watu wangapi watakosa huduma ya mawasiliano ambayo ni haki yao ya kikatiba?
Bila shaka TCRA na serikali kwa ujumla italiona hili na kuhakikisha kuwa sisi wananchi hatuadhibiwi kwa kunyimwa haki ya habari kwa sababu zozote zile.
 
Vituo vya ITV, Clouds Tv, EATV na Channel 10 vyaomba busara kutumika ili kutatua tatizo la matangazo ya chaneli za bure.

IMG_6153.jpg IMG_6154.jpg IMG_6155.jpg IMG_6156.jpg
 
Kwasasa ukitaka kuona local channels ambazo ni FTA ni lazima uwe na moja kati ya hivyo ving'amuz vitatu. Na kwa jinsi hivyo ving'amuz vitatu vilovyo vya hovyo, itakulazimu tu uwe na ving'amuz viwili kimoja chenye FTA channel (coz wengi ni wapenz wa taarifa ya habar ya itv na vipind vyao) na kingine chenye ubora kisicho na FTA channel (aidha Azam Tv, DStv nk).
Ni ukiritimba flan hv umewekwa na hawa tcra wasiojielewa. Kwny hili tcra wamekuwa kama BASATA vile kufanya kaz kwa kujipendekeza pasipo kuangalia pande zote.
Sasa swali linakuja hiv, kwa watanzia tunavtopenda dezo hv ni nani ataenda kulipia star times kila mwez wakat FTA anazion bure, jibu ni kwamba hawa Ting, Star times na Continental watakosa kabisa malipo ya kila mwezi. Sasa wao watapata wapi hela za kujiendesha?? Channel zao wenyewe hazina uwezo wa kuvutia matangazo wakapata hela, ss watajiendeshaje km hizo FTA channel zinaonyeshwa bure na matangazo ya kwenye hizo fta channel yanalipwa kwa wamiliki wa hizo fta (mfn Biko anawalipa ITV hawalipi wenye king'amiz cha TING)???
Hapa ndipo mgogoro mkubwa unakuja kat ya wamilik wa ving'amuz na wamilik wa hiz fta channels. Wamilik wa ving'amuz wanataka kuwaminya wenye fta channel (itv etc) wawalipe kiasi kikubwa mpk tone la mwisho kwa wao kuwapa coverage bure, kitu ambacho si sahihi. Sasa ni inawezekana wenye ving'amuz ss hv hawalipwi ndio mana wanazifunga fta zisionekane mpk mteja afanye malipo ya mwezi.

Huu ni ukiritimba wa kizamani sana waliouweka tcra. Wenye ving'amuz na wenye channel (ITV) na channel zingine walitakiwa wawe huru kuingia mikataba baina yao na wakubaliane malipo na sio kuwalazimisha kuweka utaratibu wa fta channel tena ziwe kwny ving'amuz vitatu tu. Kitendo cha ITV, clouds, star tv na zingine kutoonekana kwny ving'amuz vya Azam na DStv kutawaumbisha kibiashara mana itashusha thaman na idadi ya matangazo yao kwani coverage zao zitakuwa zimepungua (ni obvious Azam na DStv wana coverage kubwa sana kuliko hao wazembe wa star times, ting na continental ambao mi naona wako kiprimitive sana). Kuziondoa DStv ni kuziondoa local channel zetu kwnye jukwaa la kimataifa, huku ni kuua juhud zao za kujitanua kimataifa ambapo kuna fulsa nyingi sana.

Nawakumbusha tu TCRA (kwny hili wameazima akili za BASATA), HAKUNA BURE DUNIANI.


Analysis nzuri sana hii mkuu
 
Bado sijaelewa... TCRA wanataka nn? Sasa sisi ili tupate LOCAL channels tufanye nn? Sawa wamewafungia Azam + Zuku wasirushe Channel za ndani, sasa ili tupate sisi channel za ndani TUFANYE NN? :mad::mad::mad::mad::mad::mad::mad::mad::oops::oops::oops::oops:
 
nashukuru Mkuu hapa nimekuelewa kuwa kumbe wamepewa notice kwanza, lakini sijaelewa pale wanapoambiwa ...

TCRA claims to have reminded the companies several times that the only free channel their decoders should broadcast is TBC 1 by The National Broadcasting Corporation but they keep disobeying the orders.

Ina maana hapa TCRA wanatutaka kutazama cherekochereko kwa lazima au?
Jamani hiyo ni biashara ,mkataba unawaruhusu starmedia,ting na continental tu ndio warushe hizo local channels na walifanya uwekezaji mkubwa sana kwenye miundo mbinu ya kurushia hayo matangazo,hao azmu,zuku na dstv wamekiuka sheria!!na ndio maana jana waziri amesema kuamua vinginevyo ni hadi sheria iliyopitishwa na bunge ibadirishwe!!labda jiwe aingilie kati!!atoe tamko lakini kama ni mfuasi wa utawala wa sheria hawezi japo ........hapa hakuna siasa ni sheria tu
 
Tatizo kubwa ni tcra kuweka sheria, kanuni na leseni za kipuuzi ambazo hazina tija kwenye biashara hii ya kurusha matangazo ya tv. Wameweka utaratibu mbovu ambao haiwez kumnufaisha yyt kati ya mmiliki wa tv (mfn ITV) na mmilikii wa king'amuzi (mfn DStv).
Tatizo kubwa lilianza pale kwa TCRA walipotaka kujikomba kwa wananchi kwa kutaka kuwa na channel za kuonyeshwa bure wakat hizo channel hizo ziko kibiashara. Hapa ndipo kiini cha huu mkanganyiko wote. Hili likapelekea kuja kwa kwanuni na leseni za kijinga ambazo zinawaumiza wenye channel na wenye ving'amuzi. Channel iliyotakiwa kuonyeshwa bure ni moja tu TBC1 ambayo haijiendeshi kibiashara. Hiki ni kilio cha mda mrf toka kwa wamiliki wa hiz channel na wamiliki wa ving'amuzi. TCRA wameharibu kabisa huu mfumo wa digital.
Mfano: ITV watapataje hela kama matangazo yake yanaonyeshwa bure Azam TV? Hapa ITV itamlazimu amlipe Azam TV kwasababu kampatia coverage ambaye itamsaidia yy itv kupata matangazo. Hapa ITV atakuwa anatoa hela yake mfukoni ili tu huyu mtanzania aangalie bure. Inshort hela ambayo mwananchi alitakiwa alipie king'amuzi italipwa na ITZ which is not right.

Biashara hii ya matangazo ya digital iko hivi:-
King'amuzi kinarusha channel then mteja analipia kuona hizo channel. Hapa sasa ndipo biashara inapoanza na ndipo TCRA anapo ingia kuharibu hii biashara.
1. ITV kama wana wateja wengi (coverage kubwa) basi DSTV atalazimika kumlipa itv kiasi fulan watakachokubaliana maana kamsaidia kumletea wateja ambao watanunua kinga'amuzi chake na walipie kila mwezi kuiona itv. Hapa hii hela iliyolipwa na wewe mteja ndio watakayogawana itv na dstv.
2. Kama itv hawana wateja wengi (coverage kubwa) basi itv watalazimika kumlipa dstv kias fulani watakachokubaliana maana atakuwa amesaidiwa kuongeza idadi ya wateja (coverage kubwa) hivyo kumuongezea idadi na thamani ya matangazo. Kiasi kidog cha faida anayopata itv kutoka kwny matangazo atampatia dst na kiasi kidogo kingine dstv anakipata toka kwa mteja aliyelipia king'amuzi. Kama itv itaonyeshwa bure basi yy itv atalazimika kulipa kiasi alichotakiwa kulipa mteja wake mana itv ndio atakayenufaika na uwepo wake ndani ya king'amuzi cha dstv.
Suala la channel za ndani kuwa bure halina tija kwny uzalishaji. Litaua ving'amuzi vya ndani na kuua hizi channel za ndani. Channel za ndani zotashindwa kuwalipa wnyw king'amuz ili channel zao zilionyeshwe bure, vivyo hivyo ving'amuz havitaweka channel hiz kwny ving'amuz vyao kama hawalipwi na mteja wala channel husika (itv). ITV atakosa coverage, hvyo atakosa hela ya matangazo atakufa. Mwenye king'amuzi atakosa channel kwny kinga'amuzi chake, hivyo atakosa wateja wa kunua king'amuzi chake na kukosa malipo ya kila mwezi ya vifurushi vyake, atakufa.

Hakuna bure duniani. TCRA kwa hili wameweka kanuni zitakazoua hii tasnia ya television. Hapa ndipo tulipojikwaa, kwengine kote huko ni tulipoangukia.
Point
 
TCRA, TRA, na madudu mengine yanayovuna bila kupanda yote yana tabia ya kuua kuku anaetaga mayai.
 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe ameagiza Makampuni ya Dstv, Azam na Zuku kurejesha fedha za wateja walizokuwa wamelipia ving'amuzi kwani Kampuni hizo zimekiuka sheria.

IMG_6204.jpg
 

Attachments

  • IMG_6204.jpg
    IMG_6204.jpg
    44.8 KB · Views: 25
Kwa utaratibu mbovu na kanuni mbovu, TCRA ina leseni za ain mbili. Aina ya kwanza ni leseni ya local itakayokuwa na Free to Air channels (channel zitakazorushwa bure bila kulipia) ambazo ni ITV, TBC1, Channel 10, Clouds TV, Star Tv na EATV.
Hiz FTA channel ni decorder tatu tu zenye leseni au mamlaka ya kuonyesaha ambazo ni Star timws, Continental na TING. Ving'amuz vyote vilivyobaki kuanzia Azam Tv, DStv, Digitek n.k hazitakiwi kuonyesha hizo channel si bure wala kwa kulipia (wana leswni ya kuonyesha TBC2 tuu)
Hapo ndipo kwny shidaaaa...
Hivyo ving'amuz vyenye FTA (free to air) channel havionyeshi bure hizo channel (kifurush kikiisha hazionekani) na hizo zisizokuwa na lesen ya kuonyesha FTA (DStv, Azam TV etc) nao wanazionyesha hizo channel tena kwa kulipia..
Hapo ni mkanganyiko mtupu, ss tcra wamewavalia njuga hawa wasio na fta, wamewaacha wenye lesen ya fta lakn hawaonyeshi bure kwa wananchi. Kaupendeleo flan hv kwasababu wote ni watoto wa baba mmoja (star times vs tcra).
Hope umenipata kidogo mkuu..
Tatizo lililopo ktk Tanzania ni kipato kidogo kiasi kwamba ukiacha channel 6 bure. Hakuna atakayelipia King'amuzi
 
Mnaotumia king'amuzi cha Continental huwa mnatazama ITV,Clouds Tv,Channel 10 bure vifurushi vikiisha muda au TCRA wao hutumia decorders zipi? Ujinga nchi hii
mwingi Sana.
 
Back
Top Bottom