Multichoice (Dstv) na Zuku hatarini kunyang'anywa leseni za kurusha matangazo Tanzania kwa kukaidi Agizo la TCRA la kutoonyesha televisheni za ndani

Hao Simbanet Zuku ndo kabisa wafungiwe milele huduma zao mbaya sana. Ukiangalia Zuku muvi Kila siku ni hizohizo hakuna mabadiliko. Langalanga, sanamu ya Sopanga, chizi kalogwa tena, tozi kikojozi, zee jinga na zingine za kishambashamba sana. Miziki yao ikiisha muvi ndo ile ya Mb Dog na Latifa, biliblaki na suma lii. Daah hawa watumbuliwe milele
 
non sense kwa manufaa a nani,au ya TBCCM?...kwani zikionyeshwa sisi walaji watanzania si ndio tunapata faida..au mnataka kutufanya tuizoee tv pekee ya kiswahili au ya nyumbani ibaki kuwa tbccm...walahi tutapata habari zilizofanyiwa multiple filtration....TCRA hata nyie hamtabaki salama..alimtumia NAPE..alipomaliza kazi akamwaga kwa aibu...Akamtumia mwigulu..Kuficha ukweli wa waliojeruhi ndugu yake...alipomaliza kazi akamtema...Akimaliza kuwatumia kufungia hizo kampuni za nje na kubaki na za ndani na kupata waste news...na nyie anafunga hio taasisi..anacontrol kila kitu ajuavyo...labda mlambe soksi zake sana mpaka zipate unyemvu....
 
Hili tangazo la Kimombo linaeleweka lakini hili la kiswahili inabidi wakaombe usaidizi BAKITA

Any way, hata Startimes ya antenna wanaonyesha TBC1 tu na wao wafungiwe hakuna namna nyingine
 
Nahisi kuna baadhi ya wachangiaji hawakuelewa kusudi la ban ya TCRA
 
Hili tangazo la Kimombo linaeleweka lakini hili la kiswahili inabidi wakaombe usaidizi BAKITA

Any way, hata Startimes ya antenna wanaonyesha TBC1 tu na wao wafungiwe hakuna namna nyingine
Nami pia nimelisoma mara nyingi nyingi bila kulielewa.
 
Sisi wazee wa Dstv ndo hivyo tushaliwa kichwa. Kuwa na Kifurushi kisicho na channel za Bongo, hakuna maana.
Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu. Inatakiwa na TBC1 wanyang'anywe hadi na wao waweke free to air baadhi ya chanel zao. Inaniuma sana Azam anapata tv zote za ndani wakati Startime huwapati Azam hata ile ya habari wameziba. Mbwaimbwai tu
 
safi this should not be double standard kama anafanya hvi awaadhibu na Azam,Dstv & Zuku, tumechoka kulipia local channel while is free of charge
Na tcra wahakikishe azamu nao wana free to air zinazopatikana ving'amuzi vingine
 
Nadhani ni issue ya leseni yao maana ving'amuzi vingine vimepewa leseni ya kuwataka kuonyesha "free to air" channels hata kama king'amuzi kitakata na DSTV yeye amepewa leseni inayowataka wasionyeshe "free to air" channel lakini yeye anazionyesha na pindi kifurushi kinapoisha na hizo channel nazo zinakata hivyo tafsiri hapo inaonekana ananufaika kibiashara na hizo channel na inamlazimisha mwenye DISH la DSTV kulipia tena ili aendelee kupata huduma ambazo kimsingi alitakiwa aangalie bure hivyo njia pekee abadilishe leseni yake ili aweze kuonyesha hizo channel kama wengine kwamba kifurushi kikikata ziendelee kuwepo kama wengine.

Ila nitafurahi kama TCRA wakija na kutoa tamko kwa ving'amuzi ambavyo bimepewa leseni ya kuonyesha hizo channel bure lakini hufika kipindi hukata na kujifanya unatakiwa ku-activate king'amuzi kwa kulipia
hapo nimeelewa vzr mkuu....
 
Tatizo kubwa ni tcra kuweka sheria, kanuni na leseni za kipuuzi ambazo hazina tija kwenye biashara hii ya kurusha matangazo ya tv. Wameweka utaratibu mbovu ambao haiwez kumnufaisha yyt kati ya mmiliki wa tv (mfn ITV) na mmilikii wa king'amuzi (mfn DStv).
Tatizo kubwa lilianza pale kwa TCRA walipotaka kujikomba kwa wananchi kwa kutaka kuwa na channel za kuonyeshwa bure wakat hizo channel hizo ziko kibiashara. Hapa ndipo kiini cha huu mkanganyiko wote. Hili likapelekea kuja kwa kwanuni na leseni za kijinga ambazo zinawaumiza wenye channel na wenye ving'amuzi. Channel iliyotakiwa kuonyeshwa bure ni moja tu TBC1 ambayo haijiendeshi kibiashara. Hiki ni kilio cha mda mrf toka kwa wamiliki wa hiz channel na wamiliki wa ving'amuzi. TCRA wameharibu kabisa huu mfumo wa digital.
Mfano: ITV watapataje hela kama matangazo yake yanaonyeshwa bure Azam TV? Hapa ITV itamlazimu amlipe Azam TV kwasababu kampatia coverage ambaye itamsaidia yy itv kupata matangazo. Hapa ITV atakuwa anatoa hela yake mfukoni ili tu huyu mtanzania aangalie bure. Inshort hela ambayo mwananchi alitakiwa alipie king'amuzi italipwa na ITZ which is not right.

Biashara hii ya matangazo ya digital iko hivi:-
King'amuzi kinarusha channel then mteja analipia kuona hizo channel. Hapa sasa ndipo biashara inapoanza na ndipo TCRA anapo ingia kuharibu hii biashara.
1. ITV kama wana wateja wengi (coverage kubwa) basi DSTV atalazimika kumlipa itv kiasi fulan watakachokubaliana maana kamsaidia kumletea wateja ambao watanunua kinga'amuzi chake na walipie kila mwezi kuiona itv. Hapa hii hela iliyolipwa na wewe mteja ndio watakayogawana itv na dstv.
2. Kama itv hawana wateja wengi (coverage kubwa) basi itv watalazimika kumlipa dstv kias fulani watakachokubaliana maana atakuwa amesaidiwa kuongeza idadi ya wateja (coverage kubwa) hivyo kumuongezea idadi na thamani ya matangazo. Kiasi kidog cha faida anayopata itv kutoka kwny matangazo atampatia dst na kiasi kidogo kingine dstv anakipata toka kwa mteja aliyelipia king'amuzi. Kama itv itaonyeshwa bure basi yy itv atalazimika kulipa kiasi alichotakiwa kulipa mteja wake mana itv ndio atakayenufaika na uwepo wake ndani ya king'amuzi cha dstv.
Suala la channel za ndani kuwa bure halina tija kwny uzalishaji. Litaua ving'amuzi vya ndani na kuua hizi channel za ndani. Channel za ndani zotashindwa kuwalipa wnyw king'amuz ili channel zao zilionyeshwe bure, vivyo hivyo ving'amuz havitaweka channel hiz kwny ving'amuz vyao kama hawalipwi na mteja wala channel husika (itv). ITV atakosa coverage, hvyo atakosa hela ya matangazo atakufa. Mwenye king'amuzi atakosa channel kwny kinga'amuzi chake, hivyo atakosa wateja wa kunua king'amuzi chake na kukosa malipo ya kila mwezi ya vifurushi vyake, atakufa.

Hakuna bure duniani. TCRA kwa hili wameweka kanuni zitakazoua hii tasnia ya television. Hapa ndipo tulipojikwaa, kwengine kote huko ni tulipoangukia.
Asante sana mkuu!
Umetufafanulia vizuri sana.
Sasa mi bado sijaelewa uhusiano wa tangazo hili na AZAM TV kuondoa local channels zote. Wanatangaza kuwa kuna tatizo la kisheria lakini hatujui nao wameingiaje katika hili la DSTV na ZUKU?
 
Kwa utaratibu mbovu na kanuni mbovu, TCRA ina leseni za ain mbili. Aina ya kwanza ni leseni ya local itakayokuwa na Free to Air channels (channel zitakazorushwa bure bila kulipia) ambazo ni ITV, TBC1, Channel 10, Clouds TV, Star Tv na EATV.
Hiz FTA channel ni decorder tatu tu zenye leseni au mamlaka ya kuonyesaha ambazo ni Star timws, Continental na TING. Ving'amuz vyote vilivyobaki kuanzia Azam Tv, DStv, Digitek n.k hazitakiwi kuonyesha hizo channel si bure wala kwa kulipia (wana leswni ya kuonyesha TBC2 tuu)
Hapo ndipo kwny shidaaaa...
Hivyo ving'amuz vyenye FTA (free to air) channel havionyeshi bure hizo channel (kifurush kikiisha hazionekani) na hizo zisizokuwa na lesen ya kuonyesha FTA (DStv, Azam TV etc) nao wanazionyesha hizo channel tena kwa kulipia..
Hapo ni mkanganyiko mtupu, ss tcra wamewavalia njuga hawa wasio na fta, wamewaacha wenye lesen ya fta lakn hawaonyeshi bure kwa wananchi. Kaupendeleo flan hv kwasababu wote ni watoto wa baba mmoja (star times vs tcra).
Hope umenipata kidogo mkuu..
 
Kweli zile zama za kufanya mambo kwa kujisikia kisa umeweka mtaji wako katika biashara flani zimeanza kupungua. SAIV NI MWENDO WA KUTII SHERIA NA KUTIMIZA MAKUBALIANO YOTE
 
Tatizo kubwa ni tcra kuweka sheria, kanuni na leseni za kipuuzi ambazo hazina tija kwenye biashara hii ya kurusha matangazo ya tv. Wameweka utaratibu mbovu ambao haiwez kumnufaisha yyt kati ya mmiliki wa tv (mfn ITV) na mmilikii wa king'amuzi (mfn DStv).
Tatizo kubwa lilianza pale kwa TCRA walipotaka kujikomba kwa wananchi kwa kutaka kuwa na channel za kuonyeshwa bure wakat hizo channel hizo ziko kibiashara. Hapa ndipo kiini cha huu mkanganyiko wote. Hili likapelekea kuja kwa kwanuni na leseni za kijinga ambazo zinawaumiza wenye channel na wenye ving'amuzi. Channel iliyotakiwa kuonyeshwa bure ni moja tu TBC1 ambayo haijiendeshi kibiashara. Hiki ni kilio cha mda mrf toka kwa wamiliki wa hiz channel na wamiliki wa ving'amuzi. TCRA wameharibu kabisa huu mfumo wa digital.
Mfano: ITV watapataje hela kama matangazo yake yanaonyeshwa bure Azam TV? Hapa ITV itamlazimu amlipe Azam TV kwasababu kampatia coverage ambaye itamsaidia yy itv kupata matangazo. Hapa ITV atakuwa anatoa hela yake mfukoni ili tu huyu mtanzania aangalie bure. Inshort hela ambayo mwananchi alitakiwa alipie king'amuzi italipwa na ITZ which is not right.

Biashara hii ya matangazo ya digital iko hivi:-
King'amuzi kinarusha channel then mteja analipia kuona hizo channel. Hapa sasa ndipo biashara inapoanza na ndipo TCRA anapo ingia kuharibu hii biashara.
1. ITV kama wana wateja wengi (coverage kubwa) basi DSTV atalazimika kumlipa itv kiasi fulan watakachokubaliana maana kamsaidia kumletea wateja ambao watanunua kinga'amuzi chake na walipie kila mwezi kuiona itv. Hapa hii hela iliyolipwa na wewe mteja ndio watakayogawana itv na dstv.
2. Kama itv hawana wateja wengi (coverage kubwa) basi itv watalazimika kumlipa dstv kias fulani watakachokubaliana maana atakuwa amesaidiwa kuongeza idadi ya wateja (coverage kubwa) hivyo kumuongezea idadi na thamani ya matangazo. Kiasi kidog cha faida anayopata itv kutoka kwny matangazo atampatia dst na kiasi kidogo kingine dstv anakipata toka kwa mteja aliyelipia king'amuzi. Kama itv itaonyeshwa bure basi yy itv atalazimika kulipa kiasi alichotakiwa kulipa mteja wake mana itv ndio atakayenufaika na uwepo wake ndani ya king'amuzi cha dstv.
Suala la channel za ndani kuwa bure halina tija kwny uzalishaji. Litaua ving'amuzi vya ndani na kuua hizi channel za ndani. Channel za ndani zotashindwa kuwalipa wnyw king'amuz ili channel zao zilionyeshwe bure, vivyo hivyo ving'amuz havitaweka channel hiz kwny ving'amuz vyao kama hawalipwi na mteja wala channel husika (itv). ITV atakosa coverage, hvyo atakosa hela ya matangazo atakufa. Mwenye king'amuzi atakosa channel kwny kinga'amuzi chake, hivyo atakosa wateja wa kunua king'amuzi chake na kukosa malipo ya kila mwezi ya vifurushi vyake, atakufa.

Hakuna bure duniani. TCRA kwa hili wameweka kanuni zitakazoua hii tasnia ya television. Hapa ndipo tulipojikwaa, kwengine kote huko ni tulipoangukia.
Mkuu,kongole na ubarikiwe kwa ufafanuzi maridhawa. Huu ndio ukweli na hali halisi ya hii biashara.
 
Back
Top Bottom