Mukama aibuka, aishambulia CHADEMA!

Mukama kwa nini hamkufanyia mkutano VIJANA SOCIAL HALL kinondoni?ni wazi pameshakufa chini ya uvccm
 
watu kama Mukama wanatakiwa wawe eliminated kwenye gene pool ya watanzania asije mtu mwingine akarithi gene za mtu kama mukama!!
 
ni dhahiri ccm imepata ugonjwa wa sonona baada ya kuona kila dalili ya kupoteza uongozi wa nchi hii.mbaya zaidi mbinu za kujinasua katika janga hili zimewaishia na sasa wanabaki kuropoka na kutoa vitisho.times up ! ccm kwaheri!
 
Yeye ni wa kiwango kipi hapo? Maana hawa jamaa kwa vile wana access na media basi hata njozi zao huwa wanaziweka mle.

Je amepikika? - ki-CCM YES. Hafai popote ile CCM tu.
Je anayo maadili ya uongozi - kauli na matendo vinathibitisha hana
Je Mukama ana tija yoyote ktk maendeleo chanya ya Tanzania - HAPANA.

Hivyo ni wa kupuuza tu
 
Hivi nchi hii ukiwa na kilabu cha usiku ni 'dhambi kubwa' kiasi chama chako hakipaswi kuongoza nchi...bali ukiwa fisadi na mbadhirifu wa rasilimali za umma unakuwa umepikika 'kimaadili' na kutamba kuwa unastahili kuongoza nchi! Kama vilabu vya usiku ni vibaya kiasi hicho, walifuata nini 'Maisha Club'? Kwa nini Mukama hakukataa alipoalikwa kwenda Maisha Club ikiwa watu wanaojihusisha na hizo club hawana maadili na hawafai kushika uongozi wa nchi!?
Zee lina mawazo mgando kweli wenye baba huyu mwiteni mwambieni "baba unatokota kaa kimya" maurities waliwahi kuongozwa na dj kwa sababu chama tawala kilichokwa nguvu ya umma ikabadili utawala
 
*Asema inakabiliwa na ukame wa viongozi waliopikika kimaadili
* Hata kupata wagombea hutegemea 'iokoteze' walioshindwa michujo au chaguzi za CCM
* Asena kwa mtaji huo haiwezi kuwa chama chenye tija na hatma njema kwa taifa.


"CCM bwana ni tasisi yenye viongozi wenye chimbuko la maadili, siyo kama vyama vingine vinaongozwa na wenye vilabu vya usiku halafu eti navyo ni vyama vya kuweza kuongoza nchi", alisema Mukama. Alisema kutokana na CCM kuwa chama chenye chimbuko la maadili bora, ndiyo sababu kila kinapofanya uchaguzi wa kupata viongozi wake huwa ni wa kihistoria kwa kuwa anayepenya kuwa kiongozi huwa amepita kwenye tanuru la uchujwaji wa hali ya juu.

Katika hafla hiyo, wanachama wa Kata hiyo, waliuopongeza uongozi wa juu wa CCM kwa namna ulivyoweza kuweka taratibu zilizo wazi na za haki katika kuhakikisha uchaguzi ndani ya chama unazaa viongozi walio dhabiti. Mapema, Mukama alikabidhi hati kwa vijanan na makamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM, ambao wameshiriki katika shughuli mbali mbali za kuimarisha chama kwa namna moja au nyingine.

Ndio maadili mnayofundishana ndani ya CCM na products zenu ni Nape, Job Lusinde na Tambwe Hizza just to mention a few ambao wameiva vya kutosha. Hongera mkufunzi Mkama.
 
Hivi nchi hii ukiwa na kilabu cha usiku ni 'dhambi kubwa' kiasi chama chako hakipaswi kuongoza nchi...bali ukiwa fisadi na mbadhirifu wa rasilimali za umma unakuwa umepikika 'kimaadili' na kutamba kuwa unastahili kuongoza nchi! Kama vilabu vya usiku ni vibaya kiasi hicho, walifuata nini 'Maisha Club'? Kwa nini Mukama hakukataa alipoalikwa kwenda Maisha Club ikiwa watu wanaojihusisha na hizo club hawana maadili na hawafai kushika uongozi wa nchi!?
siku zote ukishaishiwa unakuwa mlopokaji tu, ni sawa na baba wa familia aliyefurilia uwa mlopokaji tu, mtoto akifanya hata kosa dogo ni kipigo au utapata maneno ya ajabu, wakati zamani aikuwa hivyo.
 
Angalizo lake lina sura mbili.
La kwanza ni kweli cdm hawajaweza kujipanga nchi nzima kuweka wagombea kuanzia serikali za mitaa na vitongoji, udiwani na wabunge. Labda tatizo ni mtaji mdogo walio nao maana ni lazima uwe na uwezo wa kutoa semina kwa wanachama kila sehemu na pili uwawezeshe kwa namna moja au nyingine kugombea.
La pili huyu katibu mkuu amegutuka usingizini labda baada ya kuonja moja mbili baridi kwani twaambiwa walipandisha bei ya mafuta ili wapate hela ya uchaguzi wa chama. Watanzania wote tumechangia uchaguzi wa wenye nchi bila kujua hayo ndio tanaambiwa ni maadili? Wametumia rungu kama chama tawala kujiokoa.
Cdm wajitahidi kwa hali na mali kupata wagombea kila ngazi nchi nzima na kura watapata kwani wananchi sasa wanataka mabadiliko.
 
Kama CCM ndicho hama chenye maadili basi Taifa limekuwa morally bancrupt.Anadai Chadema inaongozwa na watu wanaomiliki club za usiku?Kwa hiyo waendaji club za usiku wanavunja sheria?hawana maadili?mbona serikali inayoongozwa na chama chake(chenye maadili) ndiyo inayotoa leseni?Kwanini club za usiku zisipigwe marufuku?

Je,maadili ni kumrudisha waziri mkuu aliyelazimika kujiuzulu kwa kashfa ya Ufisadi pamoja na mwanasheria wa zamani wa serikali anayesifika kukwapua fedha na kuweka nje ya nchi?

Inaonekana Tafsiri ya neno 'Maadili' hubadilika kama ngozi ya kinyonga.Huyu ndiye katibu mkuu wa chama cha siasa kinachopanga kuwaletea watanzania maisha bora!

Si afadhali chadema yenye viongozi wachache waadilifu kuliko utitiri wa viongozi waliochafuka kwa ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.asiwafundishe watanzania kujali quantity,bali quality ya viongozi.Sijui ni kwa nini aishambulie chadema tu?Narrow minded....
 
Ninachowapendea ccm ni kwamba baada ya Mangula sasa wanateua makatibu wendawazimu, wanaokisaidia chadema kupanda chati!

Go Mukama go go goooooo!
 
Kama cdm ina ukame wa viongozi na imewadhoofisha ccm kiasi hiki je ikiwa na mafuriko itakuwaje?????? wameumia , hivi na huyo Mukama bado yupo tu, si alitaka kukimbilia mambwepande baada ya kumuogopa nape nnauye????????????
 
Nisaidieni wanyalukolo,biashara ya Klabu ya usiku na ile ya ARVs feki ni ipi inayoweza kukuingiza jehenam haraka zaidi (mimi ni mlokole)
 
Madagascar yuko Rajoelina, hamjui fani yake? jimbo la calfornia kule USA liko chini ya mcheza sinema. Urusi iko chini ya mwanajudo. Tutafute mbinu nyingine ya kupambana na hawa jamaa.
 
Tambwe Hiza, Msabaha, Shaibu Akwilombe, Dr Aman Walid Kabouru, Masumbuko Lamwai, Makongoro Nyerere... all of these have been in the opposition... and the list goes on
Chitambala, Nakaaya Sumari, Thomas Ngawaiya, Daniel Swanzugwako, Frank Magoba, Dani Makanga, Prince Bagenda, Steven Wassira, Abdallah Fundikira(Late), Gidion Cheyo nk.
 
Sh sh ssh mwambieni kimya! Nape uyo anakuja. Akimkamata , atajuta.
 
Back
Top Bottom