Muhimbili wagoma kumpokea kichaa..Hii ni haki?

Ab-Titchaz

JF-Expert Member
Jan 30, 2008
14,631
4,225
Muhimbili wagoma kumpokea kichaa...

2008-10-24 09:54:19
Na Romana Mallya

Uongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) umekataa kumpokea mshtakiwa, David Denge (21), anayekabiliwa na mashtaka ya mauaji ya wagonjwa wawili wa akili hospitalini hapo.

Aidha, hospitali hiyo imependekeza mshtakiwa huyo apelekwe katika gereza la Isanga lililopo mkoani Dodoma.

Muhimbili ilikataa kumpokea mshtakiwa huyo kutokana na ombi kupelekwa hapo na ndugu wa mshtakiwa na uongozi wa gereza la Keko baada ya Mahakama ya Wilaya ya Ilala kushauri hivyo.

Awali, uongozi wa gereza la Keko uliandika barua mahakamani hapo kuomba mshtakiwa huyo ahamishiwe katika gereza la Isanga baada ya kubainika kuwa mshtakiwa huyo akiwa gerezani huwafanyia vurugu wenzake na wakati mwingine kuwatishia.

Baada ya Hakimu Mkazi, Samwel Maweda, anayesikiliza kesi hiyo kupokea ombi hilo, aliamua kuwashauri ndugu wa mshtakiwa kukaa pamoja na uongozi wa Keko ili waweze kwenda hospitali ya Muhimbili kuomba akae hapo wakati kesi ikiendelea.

Hakimu Maweda alitoa ushauri huo kwao, ili kesi inayomkabili Denge iendelee kusikilizwa kwa muda na wakati kutokana na kwamba endapo atapelekwa gereza la Isanga itakuwa ni vigumu kufikishwa mahakamani hapo.

Hakimu huyo alisema kutokana na hospitali hiyo kukataa ombi hilo, mahakama yake haina uwezo wa kukubali au kukataa mshtakiwa apelekwe wapi na kuongeza kuwa mwenye kibali ni Jaji peke yake.

Akiwa mahakamani hapo jana, Denge alikuwa mwenye uso wa furaha na alikuwa akitabasamu kana kwamba alikuwa hana kosa lo lote.

Denge wakati akiingia mahakamani mmoja wa askari waliokuwa wakimlinda walimuamuru atoe kofia aliyokuwa amevaa tayari kwa kuanza kusikiliza kesi yake.

Mshtakiwa huyo bila ubishi aliitoa kufia hiyo na alikuwa mpole wakati wote kesi hiyo ikiendelea.

Baada ya kesi kuahirishwa, mshtakiwa huyo akiwa nje ya mahakama alikuwa akitabasamu huku akiongozwa na askari waliokuwa wamemleta awali mahakamani hapo.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 4, mwaka huu.

Siku ya kwanza mshtakiwa huyo alipofikishwa mahakamani hapo Hakimu alilazimika kusoma mashtaka yake kwenye gari la polisi kutokana na kuonekana mwenye nguvu nyingi na kitendo chake cha kuvua nguo zote wakati akiwa kwenye gari hilo akisubiri kusomewa mashtaka hayo.

Mshtakiwa huyo siku hiyo alipokuwa kwenye gari la polisi, alivua nguo zake zote na alikuwa akiongea kwa kutumia lugha ya Kipare akimaanisha kwamba, ``sitaki kuvaa nguo na nyie wote mshindwe kwa jina la Yesu, kwanza mmenizuia nisiende kuchukua ndege yangu huko Rufiji.

Mshtakiwa huyo anakabiliwa na mashtaka mawili ya mauaji ambapo katika shtaka la kwanza la mauaji anadaiwa kutenda Agosti 11, mwaka huu hospitali ya Muhimbili ambapo alidaiwa kumuua mtu aliyetambulika kwa jina la Paulo Maganga.

Shtaka la pili la mauaji, siku na wakati huo huo katika eneo hilo, mshtakiwa huyo alidaiwa kumuua mtu mwingine aliyetambulika kwa jina la Abdulkadir Abed.

SOURCE: Nipashe

Muhimbili wagoma kumpokea kichaa...
 
Back
Top Bottom