Muhimbili kuanzisha benki ya mbegu za uzazi, kuzinduliwa na Rais Samia

"msukumo wa mataifa ya nje, kuathiri vizazi halisi, na kuleta broiler wengi huku duniani"

Hilo ndo jibu, jipange, chukua hatua.
Ni kweli, ukifikiri sana, utagundua dunia haina jema; kizazi cha kiume na kike kinateketezwa, hakuna uzao endelevu (jinsia moja kuoana); Swali, mwisho wa siku ni nini?​
 
Uwekezaji unaofanywa na Serikali ya awamu ya 6 inazidi kupaisha Hospital ya Taifa ya Muhimbili kufikia viwango vya Kimataifa kwenye tiba za kibingwa na bobezi ikiwemo upandikizaji wa mimba na Benki ya Mbegu.

---
RAIS Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua benki ya kuhifadhi mbegu za uzazi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel akizungumza leo Februari 28, 2024 amesema Rais Samia atazindua benki hiyo hivi karibuni.

Amesema MNH imeanza kuhifadhi mbegu hizo za uzazi na mtu akitaka kupata mtoto basi atafika hospitalini hapo na kupandikiziwa.

“Mbegu zitahifadhiwa kwa muda wa miaka mitano hadi 10, mtu kama hahitaji mtoto kwa wakati husika zitahifadhiwa, wakati akiona sasa anahitaji kupata mtoto basi atapandikiziwa,” amesema.

Amesema sio lazima watu waende nje kupandikiza kwani ndani ya hospitali hiyo wanapandikiza na kutunza mbegu hizo.

“Sio lazima uende Uturuki kupandikiza mimba, Muhimbili tunafanya na kama ukihitaji kuhifadhi mayai yako hutaki mtoto kwa sasa hadi hapo baadae tunakuhifadhia mayai yako hadi hapo baadae utakapokuwa tayari tutalikutanisha na kupata mtoto,”amesema Dk Mollel.
Mbunge wa Iringa mjini ataalikwa?
 
ni hatua muhimu sana ya kimaendeleo na ya kuongeza nguvu kazi ya Taifa inayohitajika si tu Tanzania bali Africa na Dunia mzima.

na haya ni miongoni mwa manufaa ya Sayansi na Technologia katika eneo la uzazi 🐒
 
Matumizi ya Benki hapo ni sahihi kweli.??
Usifikirie benki kama jengo lenye kuhusianisha na mihamala ya kifedha,fikiria neno benki kama akiba kama ilivyo benki ya damu.

Ila kwa kimombo sijui itakuwa named as "sperms bank" au hiyo benki itahusisha na mbegu KE.
Duuh
 
Zile mbegu kama za Pimbi zinaruhusiwa kuchangia?
Au watafanya vigezo gani mwanamke kuchaguwa aina ya mbegu nzr ya mwanaume anayomtaka
 
Back
Top Bottom