Ntemi Kazwile
JF-Expert Member
- May 14, 2010
- 2,182
- 307
Naandika kwa masikitiko baada ya kukumbana na mkasa wa kushindwa kuhudumiwa katika hospitali yetu ya taifa (MNH) kwa sababu CT scan ambayo mgonjwa wangu alitakiwa kupimwa ili aendelee na matibabu, hii ni hospitali kubwa zaidi ya kitaifa na bado haina basic working tools je hizo hospitali za mikoa na wilaya zina vitendea kazi?
Katika kujaribu kujua ni kwa nini MNH wanayo CT scan machine moja mbovu nilifuatilia kwenye mtandao kujua kifaa hiki kinagharimu kiasi gani na kugundua kuwa mashine moja, 2010 Refurbished MX 8000 16 Slice IDT CT scan, inauzwa kwa kati ya US$340,000 na $355,000 (sawa na malipo ya siku tatu tuliyokuwa tunawalipa Dowans/Richmond). Kwa maana nyingine kumbe pesa tunayo ila tatizo ni namna tunavyozitumia.
Ili kuokoa maisha ya mgonjwa wangu nimelazimika kulipa takribani laki mbili zaidi kuliko vile ningelipa kama ya kwetu (MNH) ingekuwa inafanya kazi, kwa maana hiyo nimeingizwa kwenye matumizi makubwa zaidi kutokana na uzembe wa viongozi wetu kuweka vipaumbele sawa sawa