Muendelezo wa ufisadi ;pensheni za wafanyakazi wa veta zakutwa account binafsi

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,148
Kamati ya bunge imekutana na muendelezo wa vioja vingine baada ya kukutana na kustaajabu vya musa
huko lapf wakayaona ya firauni huko veta;leo gazeti zimepambwa na vituko vya veta ati pensheni wanazokatwa
wafanyakazi baadhi yao zimekuwa zikipelekwa kwenye account ya mtu binafsi huko klabu ya finance

wakisikitika na kushindwa kuelewa wabunge wa kamati ya fedha wamesema wameshtushwa na wamepata nguvu
wakisema wanatarajia vituko vingi sana sana huko waendako..mkurugenzi wa veta alipoulizwa amesema hata yeye
ameshtuka na kusema anafwatilia huku akirudishiwa mafaili yake na kuambiwa akajpange na hao majambazi wake
warudi kabla ya jumanne ijayo wakiwa na maelezo ya uchafu waliouona

jamani kumbe huko kwenye mashirika kuna vituko hivii????embu fwatilieni zaidi wapendwa tupate uhalisia nini
kimeendeleaa huko yawezekana watu wanabadilisha majumba magari kwa pesa za babazetu za walipa kodi\
loh
 
Wamempa mafaili akayaweke sawa eeh!Hivi ndivyo tunavyofanya kazi,hapo ilikuwa hakuna mjadala jamaa alitakiwa kujiuzulu na kupisha uchunguzi na baadae mahakamani,hivi kazi ya askari upelelezi ni ipi na watu wa taarifa za kiintelijensia wapo wapi??????
 
Kwa mtindo huu unategemea maeneleo yapi? kama fedha zimekutwa kwenye akaunti ya mtu binafsi uchunguzi unaotakiwa hapa ni kwa jinsi gani hizi fedha ziliingizwa kwenye akaunti ile lakini alieziweka sioni kama kuna uchunguzi. sasa wakajipange upya,maana yake ni ni? wakarekebishe kumbukumbu? jamani naona hata aibu kumweleza mtu asiye mtanzania kwani nami niwekwa kwenye kundi hili la wezi. lakini ukumbukwe kuwa muda wa kuishi ni mfupi sana (miaka 70 kama umejaliwa) hivyo sioni umuhimu wowote wa mtu kufanya unyama kama huu, Mungu ....!
 
Back
Top Bottom