Habari nilizopata za uhakika ni kwamba amri imetoka kwa Dialo kukatisha kipindi, Sina uhakika kama naye kapata mkwara kutoka kwa kikwete au namana gani, Hili jambo linastahili kulaaniwa na kila mtu kwani uhuru wa vyombo vya habari unaanza kuminywa. Nasema hivi kwa kuwa si mara ya kwanza kipindi kukatishwa katika mazingira ya kutatanisha, ni takriban mara ya tatu !
Star TV imekuwa imeanza kujijengea heshima kama chombo ambacho kiko impartial lakini muda si mrefu itakuwa kama TBC ambao huwa wanasoma sms za kuiponda CHADEMA tu. za kuiponda CCM wanazitia kapuni. Mwishowe watangazaji wake wanapigwa mtaani
Au ile mitambo ya Serikali ya kuingilia mitambo ya TV na radio imeshaanza kufanya kazi?nakumbuka iliandikwa hapa hapa JF kwamba serikali imeugharamia kwa mabilioni!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.