kwa wale watanganyika ambao wameshikilia bango kwamba zanzibar hakuna matatizo basi ningewaomba kile kipindi cha kampeni na uchaguzi waelekee pemba na wakifika kule hata kama sio cuf basi wajifanye cuf, kisha warudi tena hapa ukumbini waseme zanzibar hakuna matatizo, mie ningewaomba ndugu zangu wasiongelee jambo wasilolijua. tunajua yaliotukuta na yaliowakuta wazee wetu ambao wengine ni marehemu kwa sasa mungu awalaze pema. mjue tu kwamba inakera kusema kwamba hakuna matatizo wakati sisi tunawajua watu ambao washapoteza maisha kupitia matatizo yaliokuwepo, kama mnasubiri tvz ikupeni data za waliouwawa basi mtasubiri mpaka kiama, ila kama mnataka ukweli kutoka kwa waathirika basi waathirika tupo wengi.