Sisi wananchi wa Nyatwali tunaitupia lawama Serikali juu ya kutolipwa fidia zetu na tangu tufanyiwe tathmini imepita mwaka moja sasa. Haturuhusiwi kufanya maendeleo kwa kujenga makazi mapya, kuendeleza kilimo cha kisasa , kupanda miti ya kudumu kwenye maeneo yetu n.k. tukisubiri fidia ambayo mpaka sasa hatujapata malipo. Sheria ya tathmini inatamka kwamba mwananchi kama hatalipwa kwa muda muafaka na miezi sita ikapita basi huyo mwananchi anastahili kulipwa asilimia 7 zaidi ya tathmini yake aliyoiwekea saini. Hivyo kwa ucheleweshaji huu tutadai asilimia 7 zaidi ya malipo yetu. Mwaka huu pia mwaka wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Vijiji vitatu vilivyoko kwenye Kata ya Nyatwali tayari vimefutwa na wananchi bado tunaishi kwenye vijiji hivyo, Je tutafanyaje uchaguzi huo?. Tunaiomba Serikali itulipe haraka iwezekanavyo ili tujue mahali pa kwenda.