Mtwara: Maafisa Saba(7) wa Polisi wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Kijana aliyekuwa akiwadai zaidi ya Tsh milioni 33.7

Wakafie jela wajinga sana
Inaonekana ndio michezo yao ila damu za binadamu ni nzito na ilitakiwa iundwe Tume kuchunguza mauaji mengine mpaka hata ya huyo askari tunaeambiwa kajinyonga inawezekana nae kachezeshwa ili kufuta baadhi ya ushahidi kwa hao wengine maana wanatoa majibu ya kujinyonga haraka mno wakidhani vichwa vyetu vimelala...
 
mtu mwovu hupanda magugu katika ngano safi.

Watanzania tuache chuki kisa watu wachache wanaochafua jeshi la polisi maana hata huku mitaani kwetu kunawezi ambao ni watoto wa baba flani na mama flani ambao watoto wao wametuachia ulemavu pia wameua ndugu zetu na kupora mali zao.

Ubaya wa mtu mmoja usichafue taswira ya mtaa ama ya taasisi flani, tujiepushe na chuki zisizo na tija.
Sawa hatukatai, kwa upande Wang nawachukia polis pamoja na kitengo Chao kiujumla yaan 90% ya polis hawana ubinadam. polis wanaroho na tabia za kipekee sana
 
Jamani hii ni tamaa ya pesa Damu ya mtu huwa hapotei bure
KUTOKA KWA VYANZO MBALIMBALI, Huu ni mtiririko wa matukio ya Mauji hayo.

NACHINGWEA.....
Kijana mmoja ambaye ni mkazi wa NACHINGWEA, LINDI ambaye pia anajihusisha na biashara ya madini, mwishoni mwa mwaka uliopita yaani 2021, alipata bahati ya kupata madini yenye thamani kadhaa, hali hii ilimpelekea kupata connection moja na mzungu ambaye alimuuzia madini hayo na kupata Dola za kimarekani Elfu kadhaa.

Mara baada ya kupata kiasi hicho cha fedha, ilibainika wazi kuwa asingeweza badilisha pesa zile ktk wilaya ya Nachingwea, hivyo akaona bora aende MKOANI MTWARA ambako ndio makao makuu ya benki karibia zote kwa Mikoa ya Kusini. Mkoa ambao pia wanapatikana ndugu zake kadhaa pia ambapo mjomba wake anayejishughilisha na ukatishaji wa tiketi za magari katika stendi ya Mkanaledi Mjini hapo.

Mkoani MTWARA...
Mara baada ya kuwasili mjini hapo, alimjulisha Mjomba wake huyo juu ya kile kilichompeleka hapo ili awe msaada wake. Hapo wakachagua Benki ya NMB kwenda kubadilishia Fedha hizo.

NMB MTWARA....
Mara baada ya kufika benki hapo, alipokelewa na Mhudumu wa benki mmoja wa kike, ambapo alimshughulikia kama mteja mpaka kufanikisha kupata fedha zinazokadiriwa kufikia au kuvuka mil 70 za Tanzania.

TATIZO LINAANZA....
Mara baada ya kuchukua Fedha hizo, mhudumu huyo wa NMB alimuuliza kijana yule kuwa anataka kurudi LINDI siku ile ile, ambapo alijibiwa na kijana huyo kuwa ndio anataka kurudi kwao.
Hapa sasa yule mhudumu wa BENKI akamshauri yule kijana asiondoke na pesa zote zile kwa siku ile, ni bora atafute Lodge nzuri apumzike ili kesho yake aweze kuondoka kwa amani zaidi. Kijana yule alikubali na kwa ugeni wake akaamua kumuuliza Mhudumu yule ni Lodge ipi nzuri kwake, ndipo akaelelezwa na akaenda huko ambapo pia alimjulisha mjomba wake.

INASEMEKANA SASA YULE MHUDUMU WA NMB ALIWATONYA MAMWELA (POLISI) KUWA KUNA ISHU YA PESA NDEFU NA MUHUSIKA YULE YUPO LODGE FULANI MJINI PALE.

LODGE....
Mara baada ya kuwasili Lodge hiyo, hapo ndipo tatizo lilianza rasmi, usiku alifuatwa na Polisi kadhaa ambapo walimtishia na kuchukua vitu vyake vyote. Waliondoka nae mpaka kituo kikuu cha polisi mjini hapo. Huku akipewa masharti ya kuwa akiulizwa kwanini amekamatwa aseme alikuwa anendesha pikipiki hivyo alivunja sheria za barabarani. Inasemekana sasa alipewa Laki moja aondoke na atarudi tar 6 mwezi huu. Lakini inasemekana askari wale kutokana na tamaa zaidi ya fedha walimchukua mpaka NACHINGWEA na wakamchukulia pesa zake zingine na kumuacha.

ANARUDI KITUONI...
Kama alivyoambiwa arudi kituoni hapo, alirudi kituoni hapo akiwa na mjomba wake ambapo sasa alikuja kufuata vitu vyake alivyoporwa ikiwa sambamba na pesa zake. Mara baada ya kufika askari wale walimchukua kwa madai wanaenda kumhoji. Wakati huo mjomba wake akiwa nje ya kituo hiko akimsubiri mpwawe huyo.
Dakika zikapita, masaa yakapita, hatimaye siku ikaisha bila kumuona mpwa wake huyo.

Siku ya pili, mjomba alirudi polisi kujua hasa mpwa wake alikopelekwa, lkn hakupata majibu sahihi. Hali hii ilipelekea kutoa taarifa NACHINGWEA na hapo familia ikaenda kwa Mkuu wa wilaya ya NACHINGWEA ili wapatiwe msaada wa kumpata ndugu yao huyo. Taarifa zilifika mbali zaidi ambapo sasa uchunguzi ulifanyika kubaini nini tatizo halisi.

YAGUNDULIKA KUUAWA...
Watoa taarifa wanadai ikagundulika kuwa kumbe alichukuliwa na kwenda kuuawa tena kwa kupigwa sindano ya Sumu, kisha mwili wake kwenda kufukiwa kusikojulikana.

ASKARI WASAKWA WAKAMATWA.
Maafisa waandamizi wa Polisi mkoani hapo wamekamatwa wapo gereza laLILUNGU mjini hapo, MKUU WA KITUO, OC-CID na askari kadhaa, pia yupo askari amekimbia lkn taarifa zinadai pia mhudumu wa NMB anasakwa kuunganishwa kwenye kesi hiyo ya kikatili zaidi.

Askari mmoja ajiua...
Inasemekana mara baada ya kesi hii kujulikana, basi askari mmoja wapo mara baada ya kukamwatwa na kuwekwa mahabusu alijiua kwa kujinyonga kwa kutumia shati lake.

Hadi sasa bado familia hawajakabidhiwa mwili wa kijana wao.
KUTOKA KWA WASIMULIAJI WA MKONI MTWARA NA VYANZO VYA HABARI KAMA ITV, MWANANCHI NK
 
Kila siku mauaji ya raia yanayofanywa na polisi yanaongezeka . Na imekuwa too much maana hatuoni IGP akichukua hatua.

=====

View attachment 2095921

JESHI la Polisi Mkoani Mtwara limewakamata na kuwafikisha mahakamani Maafisa wa Polisi saba kwa tuhuma za mauaji ya Mussa Hamisi Hamisi (25) mkazi wa Kijiji cha Ruponda wilayani Nachingwea Mkoani Lindi aliyekuwa akiwadai askari hao zaidi ya Sh milioni 33.7.

Inadaiwa maafisa hao wa polisi walijipatia kiasi hicho cha pesa wakati wakimfanyia upekuzi mfanyabiashara huyo. Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Marck Njera imesema mauaji hayo yalifanyika Januari 5, 2022 na mwili wa marehemu ulitupwa kitongoji cha Majengo kijiji cha Hiari Wilayani Mtwara.

Maafisa wanaoshikiriwa ni Mrakibu wa Polisi Gilbert Kalanje -Mkuu wa Upelelezi wa wilaya ya Mtwara, Mrakibu Msaidizi wa Polisi Charles Onyango - Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara, Mrakibu wa Polisi Msaidizi Nicholaus Kisinza - Mkuu wa Kikosi cha Intelejensia ya Jinai mkoa wa Mtwara, Mkaguzi wa Polisi John Msuya Mganga - Mkuu wa Zahanati ya Polisi Mtwara, Mkaguzi wa Polisi Msaidizi Marco Mbuta, Mkaguzi wa Polisi Shirazi Mkupa na Koplo Salimu Juma Mbalu.

Uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea.

Chanzo: Habari leo

Pia soma: Mtwara: Askari Polisi mmoja kati watuhumiwa wa mauaji ya mfanyabiashara alikutwa mahabusu akiwa amejinyonga tarehe 22 Jan 2022
MAAFISA wa cheo cha Inspector, wanafanya mauaji na kupora.
IGP Sirro hana jeshi.
 
Tatizo ni huyo karani hakumshauri vizuri kijana alitakuwa afunguliwe account maana Nachingwea ipo NMB
Nalaani hilo tukio, lakini pia tujifunze kutokutembea na pesa nyingi kwa ajili ya usalama.

Unatembeaje na milioni thelathini na tatu cash ni hatari sana.
 
hapo umeshindwa kutambua kwamba matokeo ya magumu yao tunayalipa sisi maraia Kama ilivyotokea kwa huyo jamaa wa Mtwara. Mambo yakiwa tight kwao wanatupress zaid raia ili kuziba Hilo gap. Leta hoja nyingine
Polis hata alipwe 4m kwa wiki hawez acha dhulumaaa. Narudia Tena POLISI HATA ALIPWE 4M KWA WIKI HAWEZI ACHA DHULUMAI.
 
Utai-enjoy vipi pesa uliyopata kwa kumwaga damu ya mtu?
Polisi inahitaji reform kubwa kuanzia kwenye mitalaa yao ccp hadi uongozi makao makuu.
 
Ishu tangu tarehe tano ni kwa vipi RPC anakosekana kuwa ndani? Jee OCD Yuki wapi? Kiufupi hao wote ni wahusika wanatakiwa kuwa ndani mahabusu na kesi yao iendeshwe mapema na haraka wanyongwe ili kuleta nidhamu kwa jeshi la polisi.
Kabisa wote lao ni moja,hawapaswi kuwa uraiani, tangu tarehe 5 wamepiga kimya huku wakingojea mgao wao, police wamekuja ni hatari sana kwa usalama wa raia
 
Maafisa wanaoshikiriwa ni Mrakibu wa Polisi Gilbert Kalanje -Mkuu wa Upelelezi wa wilaya ya Mtwara, Mrakibu Msaidizi wa Polisi Charles Onyango - Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara, Mrakibu wa Polisi Msaidizi Nicholaus Kisinza - Mkuu wa Kikosi cha Intelejensia ya Jinai mkoa wa Mtwara, Mkaguzi wa Polisi John Msuya Mganga - Mkuu wa Zahanati ya Polisi Mtwara, Mkaguzi wa Polisi Msaidizi Marco Mbuta, Mkaguzi wa Polisi Shirazi Mkupa na Koplo Salimu Juma Mbalu.
Yaani nilipoona hadi mkuu wa Intelejensia yuko nyavuni kw eligible kisu kimekuta mfupa

Hawa ndo "monitors" kwa mambo ya ndani ya jeshi na ndio huwa wanasaidia watu pale "mpelelezi anapotembea na ushahidi mfukoni"
 
Hawawezi kuwa wapumbavu kiasi hiki,kwamba wamuue mtu kwa milioni tano kila mtu.

There is something behind that amount of money.
Halafu watu wengi wanapiga hesabu rahisi kwamba ukigawanya kwa 7 inakuja mil4.8 hivi wanashau hiyo chain hawako 7 tu. Kuna ambao wamepenya chekeche(washirika wengine) wanaolamba vimilion au laki5 hivi kwahiyo inapungua

Hao watendaji wenyewe pengine walikua na Mil 2 tu kila mmoja
 
Mbona hela zenyewe kidogo?
Au tayari chakacha lishapita
Kidogo kwako, wenzako wasiojua kutafuta pesa wao wameona ni nyingi sana kumaliza shida zao! Kumbe Sasa ndiyo wameongeza tatizo zaidi!! Tuombe Mungu tu Waendesha mashitaka wasiharibu kesi, maana wao na Wapelelezi kazi zao zinategemeana sana!!
 
Kila siku mauaji ya raia yanayofanywa na polisi yanaongezeka . Na imekuwa too much maana hatuoni IGP akichukua hatua.

=====

View attachment 2095921

JESHI la Polisi Mkoani Mtwara limewakamata na kuwafikisha mahakamani Maafisa wa Polisi saba kwa tuhuma za mauaji ya Mussa Hamisi Hamisi (25) mkazi wa Kijiji cha Ruponda wilayani Nachingwea Mkoani Lindi aliyekuwa akiwadai askari hao zaidi ya Sh milioni 33.7.

Inadaiwa maafisa hao wa polisi walijipatia kiasi hicho cha pesa wakati wakimfanyia upekuzi mfanyabiashara huyo. Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Marck Njera imesema mauaji hayo yalifanyika Januari 5, 2022 na mwili wa marehemu ulitupwa kitongoji cha Majengo kijiji cha Hiari Wilayani Mtwara.

Maafisa wanaoshikiriwa ni Mrakibu wa Polisi Gilbert Kalanje -Mkuu wa Upelelezi wa wilaya ya Mtwara, Mrakibu Msaidizi wa Polisi Charles Onyango - Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara, Mrakibu wa Polisi Msaidizi Nicholaus Kisinza - Mkuu wa Kikosi cha Intelejensia ya Jinai mkoa wa Mtwara, Mkaguzi wa Polisi John Msuya Mganga - Mkuu wa Zahanati ya Polisi Mtwara, Mkaguzi wa Polisi Msaidizi Marco Mbuta, Mkaguzi wa Polisi Shirazi Mkupa na Koplo Salimu Juma Mbalu.

Uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea.

Chanzo: Habari leo

Pia soma: Mtwara: Askari Polisi mmoja kati watuhumiwa wa mauaji ya mfanyabiashara alikutwa mahabusu akiwa amejinyonga tarehe 22 Jan 2022
Ni aibu sana kwa Jeshi zima la Polisi na IGP.Ni wakati muafaka sasa wa IGP kujitafakari kama kweli anafaa kuwa IGP.Polisi wanawaibia na kuwaua raia badala ya kuwalinda! IGP go,go,go,kazi imekushinda. Please tender your resignation to the President.
 
Back
Top Bottom