Mtwara: Maafisa Saba(7) wa Polisi wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Kijana aliyekuwa akiwadai zaidi ya Tsh milioni 33.7

Kuna watu hapo wameharibu taaluma na maisha yao kwa ujumla kutokana na tamaa za kijinga kabisa na saa hizi wanajuta (Though it's too late).
 
unawachukia ila wenzako wanaishi vizuri kisa wao, Usimchukie mtu ambaye huwezi hata muumba chukia tabia zake mbaya tu
sasa wewe nisimchukie mtu aliyetaka kunimaliza kisa ziwezi kumuumba ?
hao wanaoishi vizuri kisa wao labda hawaishi Tanzania hii nayoijua mimi
 
Kidogo kwako, wenzako wasiojua kutafuta pesa wao wameona ni nyingi sana kumaliza shida zao! Kumbe Sasa ndiyo wameongeza tatizo zaidi!! Tuombe Mungu tu Waendesha mashitaka wasiharibu kesi, maana wao na Wapelelezi kazi zao zinategemeana sana!!
Sasa 33.7 kwa watu saba si ni sawa na kama 4.5
Hivi kweli udhamirie kuuwa kwa 4.5?
 
Sasa 33.7 kwa watu saba si ni sawa na kama 4.5
Hivi kweli udhamirie kuuwa kwa 4.5?
Ndg Chang shen kuna watu wanauwa hata kwa laki tano tu, ambayo hiyo kwako wwe ukiitaka kwa haraka naamini ukipiga simu moja au mbili kwa connection yako Mzigo huo unaingia kwa simu hapo hapo! Wakati wenzako akili hizo hawana,wao wanawaza matumizi ya nguvu tu kujipatia fedha!!
 
Nazidi kuamini kuwa huku duniani kuna binadamu wana roho mbaya sana:

- Kijana kahangaika kuchimba madini kapata hela inajitokeza mibaba yenye familia zao tena imeshafanya kazi miaka mingi polisi na ukute yana.

heshima zao kuanzia ndani ya familia zao, koo zao, mitaani kwao, misikitini/makanisani kwao, kwenye jamii kwa ujumla n.k. inaenda
kumnyang'anya pesa zake. Na kwa kuwa tamaa imezidi inaenda mpaka nyumbani kwa kijana Nachingwea kuchukua hata kile kidogo
kilichobaki.

- Kama hiyo haitoshi wanaenda kufanya ukatili na mateso yasiyosemekana kwa kijana wa watu kwa kumpiga sindano ya sumu ili kupoteza.

ushahidi. Haki ya Mungu hakuna kitu kimeniumiza na kuniharibia siku yangu kama kujua huyu kijana aliuwawa kikatili kiasi hiki. Si
wangechukua tu hela wamwachie uhai wake basi kijana wa watu angehangaika upya na maisha? Hivi leo wanarudishaje uhai wake? Je
wategemezi wake wapo kwenye hali gani? Hivi milioni 70 kweli ziwafanye mtoe roho ya mtu? Halafu askari wenyewe wapo zaidi ya saba.

maana yake mgawo si zaidi ya milioni kumi kwa kila mmoja je ndio gharama ya kuto uhai wa mtu? Serious unamdunga mtu sindano ya sumu.

ili upate milioni kumi tu? RIP kijana mhangaikaji umepitia mateso makali kwa sababu ya tamaa na roho mbaya ya watu waovu kabisa.
- Hili limejulikana wazi je ni watru wangapi wamepoteza maisha kwa mtindo huu au zaidi ya huu?

Ukweli mchungu kwa viongozi waliopo madarakani jeshi la polisi linatakiwa kufanyiwa mageuzi (sio lazima kulivunja) makubwa sana kwani askari walio wema wanachafukliwa na askari walio waovu. Na mkiendelea kufunga macho ipo siku kama sio nyie basi hata ndugu zenu watakuja siku moja kukutana na dhaham la hawa jamaa.

Hebu mtafuteni IGP Mangu (kama sikosei mara ya mwisho alipewa ubalozi au ofisa ubalozi nje) aliyehudumu kwa muda mfupi sana kwenye nafasi yake awasaide kuwavusha kwenye kipindi cha mpito.

Huyu Mangu mimi namkubali binafsi kwa sababu alikataa kupelekeshwa na wakuu wake tenda kile kipindi kigumu hasa ili atende kinyume na sheria badala yaje alisimamia taaluma yake wakaishia kumnyang'anya cheo chake.
Huwezi fanya mageuzi while bila wao kufanya namna cc haiwez kuwa madarakani... Same wanavyochinja na kuuwa kwenye uchaguz ndio wao wanaiga. Yani msingi wa haki ni katiba mpya tu. + Uchaguz wa uhuru na haki. End
 
Heshima ya jeshi la polisi inategemea IGP anayeliongoza kwa wakati husika.
Kipindi Cha Mahita ilikua Bora ukutana na shetani kuliko ukutane na polisi.
Kipindi Cha Said Mwema jeshi hili lilianza kua jeshi la kiraia na watu wengi walilipenda jeshi letu.
Kwa Sasa hivi hata hao polisi wenyewe kwa wenyewe hawapendani na wanaogopana. Ukikutana nao usiku pita mbali, Kama Ni trafik ndio kabisaa especially trafik wa mkoa wa pwani.
RTO Pwani, pull up your socks.
Haaa bro kama nakuona vile.
Nimetembea nchi hii sijawahi kuona trafiki wana njaa kali kama mkoa wa pwani hasa wale wa maeneo ya kibiti,mkuranga na rufiji pale muhoro.

Nihatari sana . Askari wamejipanga wanalazimisha rushwa tena wanataka kuanzia elfu kumi.

Najua dawa yao ipo jikoni.
 
Huyo alieuliwa huenda ni mtoto, ndugu au rafiki wa polisi mwenye cheo kizito sana kama rpc au ocd ndio maana jambo limekuwa zito hivi, na hao waliomuua hawachomoki hapo. ila ingekua ni kivingine ingepita tu fasta
Muuliwaji anatokea kwa mh.namba 3,.na kwa jins ilivyo yeye ndo atakua yuko nyuma ya hili baada ya kutonywa na wananchi wake,bila hivo
Lingepita hili kama mengine.
 
Kila siku mauaji ya raia yanayofanywa na polisi yanaongezeka . Na imekuwa too much maana hatuoni IGP akichukua hatua.

=====

View attachment 2095921

JESHI la Polisi Mkoani Mtwara limewakamata na kuwafikisha mahakamani Maafisa wa Polisi saba kwa tuhuma za mauaji ya Mussa Hamisi Hamisi (25) mkazi wa Kijiji cha Ruponda wilayani Nachingwea Mkoani Lindi aliyekuwa akiwadai askari hao zaidi ya Sh milioni 33.7.

Inadaiwa maafisa hao wa polisi walijipatia kiasi hicho cha pesa wakati wakimfanyia upekuzi mfanyabiashara huyo. Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Marck Njera imesema mauaji hayo yalifanyika Januari 5, 2022 na mwili wa marehemu ulitupwa kitongoji cha Majengo kijiji cha Hiari Wilayani Mtwara.

Maafisa wanaoshikiriwa ni Mrakibu wa Polisi Gilbert Kalanje -Mkuu wa Upelelezi wa wilaya ya Mtwara, Mrakibu Msaidizi wa Polisi Charles Onyango - Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara, Mrakibu wa Polisi Msaidizi Nicholaus Kisinza - Mkuu wa Kikosi cha Intelejensia ya Jinai mkoa wa Mtwara, Mkaguzi wa Polisi John Msuya Mganga - Mkuu wa Zahanati ya Polisi Mtwara, Mkaguzi wa Polisi Msaidizi Marco Mbuta, Mkaguzi wa Polisi Shirazi Mkupa na Koplo Salimu Juma Mbalu.

Uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea.

Chanzo: Habari leo

Pia soma: Mtwara: Askari Polisi mmoja kati watuhumiwa wa mauaji ya mfanyabiashara alikutwa mahabusu akiwa amejinyonga tarehe 22 Jan 2022
Vibaka wenzio hao.Guhutufu!
 
Back
Top Bottom