Mtu na wifi yake wanaswa wakijiuza

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,775
3,610
2.jpg

1.jpg

Sakata zima liko hivi, Jennipher Anthony (21) Mkazi wa Tabata jijini Dar pamoja na wifi yake Mgeni Tumaini (35) Machi 13, mwaka huu saa 9 usiku walinaswa na polisi maeneo ya Buguruni Kwa sokota jijini Dar wakiwa katika harakati za biashara yao ya ukahaba.

Mara baada ya kukamatwa na polisi, mtu na wifi mtu hao walipandishwa kizimbani katika mahakama ya Hakimu Mkazi ya Sokoine Drive kwa kosa hilo.

Ngugu wa watuhimiwa hao waliofika mahakamani kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo, walimlaumu Mgeni kwa kumpotosha wifi yake Jennipher na kumuingiza kwenye biashara hiyo haramu wakati akijua kuwa ana umri mdogo.

“Jennipher ametoka Iringa kwa ajili ya kuja kutafuta maisha na kufikia kwa wifi yake, kumbe walikuwa wakifanya biashara hiyo haramu bila sisi kujua,” walisema ndugu hao kwa masikitiko.

Mbali na Jennipher na wifi yake, wanawake wengine waliopandishwa kizimbani katika mahakama hiyo kwa kutokana na kise hiyo ni Asha Samson (25) Mkazi wa Mburahati, Aisha Mohammed (35) Mkazi wa Kigogo pamoja na Jenny Michael (19) Mkazi wa Mbagala na kusomewa shitaka la kufanya biashara haramu ya ukahaba.

Akiwasomea mashitaka yao Kaimu Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Mahakama hiyo Richard Magodi mbele ya Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Timothy Lyon alisema washitakiwa wote kwa pamoja walikana shitaka hilo.
Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo aliihairisha kesi mpaka Machi 26 mwaka huu, huku watuhumiwa wakikosa dhamana baada ya kushindwa kutimiza masharti na kupandishwa karandika kwenda katika Gereza la Segerea mpaka kesi hiyo itakapotajwa tena.
 
ni kweli mkuu maana serikali imeshindwa kuzuia uvuvi haramu kwa kupambana na wavuvi badala ya kuzuia viwanda vya kutengeneza makokoro sawia na hili la kahaba ni mwanamke tu?mbona wanawaonea?ujue ndio wanaotuzaa na wengine wamo bungeni wanasinzia kwa shibe na kazi za usiku!leo hii watakuwa wanakabidhi mali zao receiption kasoro silaha maana mara nyingi dada zetu sio majambazi wao ni mshiko tu blackberry,lap,pete,mikufu,n.k
 
Hakuna biashara isiyo na mnunuzi MAchangu wa kinondoni waliwahi kumueleza mgosi Yusuph Makamba...
 
Back
Top Bottom