Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 118,649
- 220,561
Steve Nyerere ametajwa kuwa Msemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania, haifahamiki aliyemteua kwenye cheo hicho ni nani, vigezo vilivyotumika kwenye uteuzi huo haramu havijulikani, wala malengo ya kufanya hivyo, bali ni dhahiri kwamba mteuliwa hajawahi kuonekana akiimba hata kwaya au kaswida popote nchini Tanzania, hajawahi kuonekana hata akiimba Wimbo wa Taifa lake, huyu anafahamika kama mchekeshaji wa KIWANGO CHA CHINI kabisa ambacho hakiwezi kuchekesha hata mtu mwenye mtindio wa ubongo.
Taarifa zinaonyesha kwamba karibu wanamuziki wote WANAPINGA UTEUZI WAKE, lakini yeye bila mshipa wa aibu anakataa kujiuzulu.
Hivi inawezekanaje kuteua mtu wa aina hii kuongoza muziki?
Taarifa zinaonyesha kwamba karibu wanamuziki wote WANAPINGA UTEUZI WAKE, lakini yeye bila mshipa wa aibu anakataa kujiuzulu.
Hivi inawezekanaje kuteua mtu wa aina hii kuongoza muziki?