Mtoto wa kingoni

St. Paka Mweusi

JF-Expert Member
Sep 3, 2010
7,637
4,521
Mtoto mmoja alipakizwa kwenye basi kwa safari ya kwenda kumsalimia babu yake kijijini mbinga.Basi lilipoondoka tu kabla hata halijakaribia kimara mtoto akauliza kwa sauti kubwa jamani tumekaribia mikumi?Abiria waliokuwa karibu naye wakamjibu bado mbali tukifika tutakuambia.Hali hiyo ya kuuliza iliendelea kila baada ya nusu saa na abiria walimjibu vilevile kuwa tukifika mikumi tutakuambia.Kufika bwawani karibu na morogoro mtoto akauliza tena swali lilelile na abiria kwakuwa wamechoka na maswali yake wakamkaripia na kumwambia si tumekwambia tukifika mikumi tutakwambia usitusumbue bwanamdogo,basi mtoto akalala usingizi na basi likaendelea na safari.Walipofika mikumi hakuna aliyekumbuka kuhusu yule mtoto wa kingoni,na basi likaendelea na safari mpaka karibu na milima ya kitonga,ndipo abiria mmoja akakumbuka nakuuliza,yule mtoto aliyekuwa anaulizia mikumi ameshuka?Abiria wengine kumtazama mtoto amelala wakajiona wakosefu na wakakubaliana na dereva arudishe gari mpaka mikumi ili wamshushe mtoto yule maana si makosa yake.Gari ikageuzwa na kurudi mpaka mikumi,walipofika mikumi wakamuamsha na kumwambia dogo mikumi hapa umefika shuka sasa,Dogo huku akiwa na macho ya usingizi akakaa sawa kwenye kiti chake na kufungua mkoba wake kisha akatoa ndizi zilizotengenezwa na utumbo wa mbuzi na kuanza kula,abiria na konda huku wakiwa na hasira wakamwambia dogo unatuchelewesha mbona hushuki?Mtoto akawajibu kwani nani amewaambia mimi nashukia mikumi?Mimi naenda mbinga ila mama aliniambia nikifika mikumi nile chakula alichonifungia.
 
Back
Top Bottom