Mtoto wa kigogo akamatwa na dawa za kulevya huko China - Dr Slaa

Status
Not open for further replies.

Titans

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,459
3,366
nilikua nasikiliza WAPO radio FM kuna habari kutoka Tabora ikimnukuu doctor Slaa kuwa ana ushahidi wa kutosha kuwa mtoto wa Kigogo mmoja wa CCM alikamatwa na madawa ya kulevya huko China July mwaka huu.

mwenye ile thread kuhusu hii issue aiunganishe hapa chini..nimeitafuta sijaipata humu.

nawasilisha.
Mtoto wa kigogo akamatwa na mihadarati China.

Mtoto anayeaminika kuwa wa mmoja wa viongozi wa juu wa serikali ya JK anatuhumiwa kukamatws na madawa ya kulevya katika uwanja wa ndege nchini China zinazokisiwa kuwa na thamani y ash bilioni nne za Kitanzania.

Tukio hilo zito linalogusa moja kwa moja uadilifu wa kigogo huyo wa serikali limemsukuma jana Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa kumtaka Rais jakaya Kikwete kuwaambia ukweli Watanzania juu ya tuhuma hizo alizodai zinaigusa serikali yake.

Akihutubia umati mkubwa wa watru katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana mjini Sikonge mkoani Tabora, Dk Slaa alisema kuwa taarifa za uhakika kutoka China zinasema kuwa Julai mosi mwaka huu vijana wenye asili ya Afrika walikamatwa Uwanja wa Ndege wa Hong Kong wakiwa na madawa ya kulevya zenye thamani ya Sh bilioio 4 ambapo mkuu wa kitengo cha mihadarati uwanjani hapo Yiu-Kwong alitaja majina ya vijana hao wawili, likwemo jina la kijana anayedaiwa kuwa mtoto wa mmoja wa viongozi wa serikali ya TZ.

"Mimi nemepokea taarifa hii kutoka China moja kwa moja. Tunamtaka Rais kikwete aseme ukwewli ni upi, maana taarifa hizi sasa zimeanza kuzagaa kwenye mitandao kuwa mtoto huyo wa kigogo serikalini kwake amekamatwa na dawa za kulevya huko China," alisema Dr Slaa.

Aliongeza: "Tangu zianze kujulikana hazojakanushwa mahali popote. Tunamtaka aeleze yeye maana alishindwa kutaja majina ya wauza mihadarati………………….


Hii ni sehemu ndogo ya habari hiyo katika Tanzania Daima la leo Jumamosi ambayo ndiyo stori yake kuu ukurasa wa mbele.
 
wataficha siri lakini kuna siku wataumbuka.tutasikia mtoto wa kigogo apigwa risasi za kichwa...mauaji yahusishwa na kundi la wauza madawa wa mexico.
 
Kwa hiyo sisi tufanyaje sasa?maana anataja tu anataja tu hata hasemi ni nini cha kufanya,mwambie aweke wazi halafu pia atuambie na sisi wananchi inatufaidisha nini hiyo habari isije ikawa kama ya zito kabwe alikuwa anatishia kuwa atawataja wenye pesa uswisi ilhali kumbe na yeye ana pesa huko..aache mambo ya kuwafanya wananchi hawana akili huyo dokta slaa,hata kama nashabikia chama ila ktk udhaifu lazima kusema ili waweze kuwa vizuri zaidi
 
jamani kuna uzi humu ulikua unazungumzia hii issue..alileta jason bourne,sijui mods waliufuta??
 
Isije ikawa aliamini ile hadithi iliyowahi kuletwa hapa siku za nyuma. China iliyo mpiga risasi meya mwanamke kwa kula rushwa na Mkuu wa mamlaka ya chakula na dawa haiwezi kwa gharama yeyote kumwachia msafirisha madawa ya kulevya.
 
Naskia hata hapa nyumbani kuna facts zinaanza kuonekana wazi kutoka kwa watumiaji kwamba anahusika na mateja wameanza kumtaja live

je wataficha hata baada ya 2015????????????????
 
nilikua nasikiliza WAPO radio FM kuna habari kutoka Tabora ikimnukuu doctor Slaa kuwa ana ushahidi wa kutosha kuwa mtoto wa Kigogo mmoja wa CCM alikamatwa na madawa ya kulevya huko China July mwaka huu.


mwenye ile thread kuhusu hii issue aiunganishe hapa chini..nimeitafuta sijaipata humu.

nawasilisha.

Babu anazeeka vibaya na siasa zake za maji taka. Kulikuwa na umuhimu gani wa kuwaeleza watu habari hizo ka hawezi kutaja jina..
 
Dawa ya hawa watu ili kukata mzizi wa fitna ni kuwachapa risasi tu wala isingefichwa kabisa!!!!!
 
Kwa hiyo sisi tufanyaje sasa?maana anataja tu anataja tu hata hasemi ni nini cha kufanya,mwambie aweke wazi halafu pia atuambie na sisi wananchi inatufaidisha nini hiyo habari isije ikawa kama ya zito kabwe alikuwa anatishia kuwa atawataja wenye pesa uswisi ilhali kumbe na yeye ana pesa huko..aache mambo ya kuwafanya wananchi hawana akili huyo dokta slaa,hata kama nashabikia chama ila ktk udhaifu lazima kusema ili waweze kuwa vizuri zaidi

huyo jamaa anazeeka vibaya...habari imetokea china anaiongelea tabora.
Ampelekee J ntao huo uzushi sio hapa.
 
hii story haina ukweli na inawezekana imetungwa. Dr Slaainabidi awe makini na story kama hizi..sioni kama zina tija kwenye taifa letu...Riiziwani ndiye anayeongelewa so angakamatwa Kikwete asingekuwa na ubavu wa kumtoa
 
Wakuu hiyo kitu inaukweli mkubwa sana. Watu hawawezi kufunguka zaidi hapa JF kuogopa kufutwa kwa thread, kula ban na kufuatwafuatwa.
 
Tatizo ni kuwa tatizo la dawa za kulevya hatulipi uzito sitahiki sisi kama watu wa kawaida. Ingefaa tuandamane hadi Ikulu na tumuulize JK ili orodha ya watu wanaohusika na madawa ya kulevya iliifanyiaje kazi? Labda ni mitaa ninayopita mimi tu, dawa za kulevya zimeharibu watu jamani na hasa vijana. Fikirieni mwanamziki mzuri kama Banza stone na mwenzie Msafiri Diof walivyoharibika. vijana wa kike ukikutana nao machozi yanakulengalenga. Tatizo wauza unga wameshamkamata JK hana la kuwafanya dawa ni 2015? Waandoke na chama chao wanachokifadhili na kinawalinda
 
wataficha siri lakini kuna siku wataumbuka.tutasikia mtoto wa kigogo apigwa risasi za kichwa...mauaji yahusishwa na kundi la wauza madawa wa mexico.
Humu ndani tumekuwa vichaa??? hivi dhambi ya mtoto anachukua baba yake au chama cha baba yake?????? mbona mnjajichanganya weneywe au kwa sababu amesema slaa???? ambaye kwenu ni kama malaika kwani hata kama akikosea inakuwa sawa???? Hivi karibuni tulikuwa tunalaani kitendo cha mtoto aliyekojolea kur'ani tukasema kuwa huyo ni mtoto kulikuwa hakuna mantiki ya kuchoma makanisa wala vurugu na wale wote waliochukulia jazba tuliwalaani sana nikiwemo mimi ambaye ni mwislamu. sasa kama huyu mtoto amekamatwa na kosa la jinai ughaibuni chama cha baba yake kinahusu nini??? huyo ni mhalifu tu hata kama angekuwa mtoto wa rais bado angekuwa ni mhalifu tu. wacheni fikra mgando ambazo zinatufanya tushindwe kupambanua mambo.
 
Ngoma imeshalia sana hii bado kupasuka. Itajulikana tu kawaulizeni watoto wa Gadaf mambo yalianza hiv hiv wakaishia kukatwa viganja.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom