Mtoto Azinduka Kutoka Mahututi na Kuanza Kuimba 'Mamma Mia'

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,150
Mtoto Azinduka Kutoka Mahututi na Kuanza Kuimba 'Mamma Mia'


Mtoto Layla Townsey Wednesday, May 27, 2009 1:42 AM
Mtoto wa miaka mitatu nchini Uingereza ambaye alikuwa mahututi katika kitengo maalumu akipumua kwa kutumia mashine aliwashangaza madaktari na wazazi wake waliokuwa wakihesabu masaa wakijua muda wowote anaaga dunia pale alipozinduka na kuanza kuimba wimbo wa Abba unaoitwa 'Mamma Mia'.
Mtoto Layla Townsey aliugua ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo (meningitis) na baadae akapatwa na shambulio la moyo lililomfanya azimie na kuzinduka mara kwa mara na baadae kupoteza fahamu kabisa na kulazwa chumba cha watu mahututi.

Awali kabla ya siku hiyo mama yake Layla, Katy mwenye umri wa miaka 23 aliona kipele kikubwa kwenye mguu wake na kuamua kumpeleka Layla kwa dokta ambaye alisema kipele hicho kilikuwa ni kipele kilichotokana na joto.

Lakini baada ya mtoto huyo kurudi nyumbani na kuanza kujisikia vibaya huku akiongea vitu vya ajabu ajabu, mama yake aliona kwamba hapa kutakuwa na tatizo na kuamua kumwahisha hospitali.

Masaa mawili baada ya kufikishwa hospitali, Layla alikumbwa na shambulio la moyo, alipoteza fahamu kabisa na kuanza kupumua kwa kutumia mashine.

"Tuliambiwa tumpe busu la mwisho kabla mashine za kumsaidia kuishi hazijazimwa, lilikuwa tukio la huzuni sana" alisema mama yake Layla.

Layla aliondolewa kwenye mashine za kumsaidia kuishi na kupunguziwa madawa aliyokuwa akipewa awali, madaktari wakiwa hawana matumaini ya mtoto huyo kupona wakijua atafariki dakika yoyote.

Lakini cha ajabu Layla alizinduka siku tano baada ya mashine hizo kuzimwa na kuanza kuimba wimbo wa kundi la muziki la ABBA unaoitwa "Mamma Mia".

"Ulikuwa ni kama muujiza, alijifunza maneno ya wimbo huu baada ya kuangalia filamu ya Mamma Mia" alisema mama wa mtoto huyo.

Mtoto Layla anaendelea vizuri hivi sasa akiwa na mama yake kwenye nyumba yao iliyopo mashariki mwa London
 
yessir kuna mada ya mbona hii forums..mi nakusapoti kabisa naona bora tuendelee kusoma zao wanazotuma..na hata nikijaribu ku comment pale inakuwa deleted..
 
yessir kuna mada ya mbona hii forums..mi nakusapoti kabisa naona bora tuendelee kusoma zao wanazotuma..na hata nikijaribu ku comment pale inakuwa deleted..

DAH! nashukuru mkuu..ila kama hata kucomment inakua deleted sasa huo ni ufisadi na udikteta.anyways hamna tatizo. tumeelewana
 
wasije kutu burrrrrrrrrrrn ila ya moyoni tuyaseme
 
Dah! Inaweza kuwa mpango wa Mungu kuthibitisha yeye ni kiboko kuliko madaktari. Mungu apewe sifa
 
"Ulikuwa ni kama muujiza, alijifunza maneno ya wimbo huu baada ya kuangalia filamu ya Mamma Mia" alisema mama wa mtoto huyo.
Sasa hapo Mungu anaingiaje wajameni?
 
yaani kuna mambo mengine yanatokea huwezi kuamini...MIUJIZA YA MUNGU
 
abduhalim mungu anaingia kama ukiwa ndani yake else ni vigumu kujua haya........
 
Back
Top Bottom