Mtendaji wa Kijiji amchapa vibao Mwananchi kisa kuvuta sigara hospitali

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,033
9,920
Mkazi wa Kijiji cha Mbwemkuru mkoani Lindi, Athumani Ndumba amelalamika kitendo cha mtendaji wa kijiji hicho, Azidu Mwenda kumpiga makofi hadharani kwa madai ya kuvuta sigara katika kituo cha afya Kitomanga.

Tukio hilo limetokea Januari 31, 2021 katika kituo hicho na kushuhudiwa na waliokuwa wamekwenda kuwajulia hali wagonjwa.

Ndumba ambaye mke wake amelazwa katika kituo hicho amesema alitoka nje kwa ajili ya kuvuta sigara na ndipo alipokumbana na mtendaji huyo.

Amesema wakati akiendelea kuburudika na sigara ndipo alipovamiwa na mtendaji huyo na kupigwa vibao viwili na hakujibu lolote wala kuzusha ugomvi kwa madai kuwa alikwenda kwa ajili ya kumjulia hali mkewe ambaye ni mjamzito.

“Nilipomaliza kuvuta sigara alitokea mtendaji na kutaka kujua aliyekuwa anavuta na nilipojibu alinishambulia kwa kunipiga makofi. Alinipiga la kwanza kabla sijakaa sawa akanipiga la pili. Waliokuwa karibu walimtaka aache kunipiga ndio akaacha,” amesema Ndumba huku Sharifa Rashid aliyeshuhudia tukio hilo akisema kitendo kilichofanywa na mtendaji huyo sio cha kiungwana.

Kwa upande wake Mwenda alikiri kufanya hivyo kwa madai kuwa alipomuuliza Ndumba alikana kuvuta sigara.

"Nilipofika Kituo cha Afya nikasikia harufu ya sigara na nikamuona Athumani anazimia sigara yake chini nilipomuita akaleta ubishi ndio tukaanza kuvutana" amesema Mwenda.

Mganga mfawidhi wa kituo hicho, Gidion Edward amesema hajapata taarifa zozote za malalamiko kutoka kwa Ndumba kauli iliyotolewa pia na mkurugenzi wa manispaa ya Lindi, Jomari Satura.

“Tukio hilo silijui lakini kama limetokea mtu aliyeshambuliwa anatakiwa akaripoti polisi ili hatua za kisheria zichukue mkondo wake,” amesema Satura.

Chanzo: Mwananchi
 
Safi.

Wavuta sigara ni watu wasio na akili kabisa, wako kama bata, bata akijisikia kunya hata kwenye sufuria ya ugali anakunya. Mvuta sigara akishikwa kiu popote tu anavuta.

Wanasayansi wanasema wavuta sigara ni binadamu wenye kiwango kidogo sana cha akili.

 
Safi.

Wavuta sigara ni watu wasio na akili kabisa, wako kama bata, bata akijisikia kunya hata kwenye sufuria ya ugali anakunya. Mvuta sigara akishikwa kiu popote tu anavuta.

Wanasayansi wanasema wavuta sigara ni binadamu wenye kiwango kidogo sana cha akili.


Unaweza kukuta eneo Hilo halina bango la kuzuia uvutaji wa sigara... Japo kuvuta sigara ktk jumuiya ya watu sio uungwana...
 
Back
Top Bottom